Headlines

Malaika wakuu

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD?
(SEHEMU YA PILI)

MALAIKA MKUU JEGUDIEL "YEHUDIEL"

Neno la Kiebrania, mjumbe (messenger) katika Agano la Kale ni Malaika na linatafsiriwa kama Malaika (angel) katika Biblia za Kingereza. Neno linatumika katika kuonyesha wajumbe wa Kiroho waliotumiwa na Mungu. (Mwanzo 32:1-2) na pia lilitumika kwa wajumbe wanadamu waliotumwa na Yakobo (Mwanzo 32:3).

YEHUDIEL:
Kwa Kiebrania יהודיאל‎‎ au Yehudiel ikimaanisha au "Mungu wa Wayahudi" ni mmoja wa Malaika Saba Wakuu.

Jina Jegudiel au Yehudiel ni muungano wa majina mawili ya "YEHUDI" na "EL".

YEHUDI:
Kwa Kiebrania neno Yehudi ndani ya Biblia inamaanisha "Kutoka katika Kabila la Yuda na au "Wayahudi". Kwa wingi ni Yehudim (plural of יהודי, Yehudi).

EL:
Mungu kwa Kiebrania ni EL. Neno EL linamaana ya "MAMLAKA" au "NGUVU" kwa Kiingereza Omnipotent, mighty, strength or power.
http://www.hebrew4christians.com/Names_of_G-d/El/el.html

Mfano:
1. El Echad inamaana ya Mungu mmoja, Malaki 2:10.
2. El Hanneeman ina maana ya "MUNGU MWAMINIFU" Soma Torati 7:9.
3. El Emet ina maana ya Mungu ni Kweli, soma Zaburi 31:5

Sasa umeona katika kila jina la Malaika Wakuu kuna sehemu ya Jina la Mungu la "EL".

Ngoja nikukumbushe. Yehudi"EL", Gabri"EL", Micha"EL", Yuri”EL” n.k. Kuna sababu kubwa sana ya Mungu kuweka sehemu ya jina lake kwa kila hawa Malaika Wakuu. LAKINI HUONI sehemu ya jina lake kwa LUSIFA. Hili somo la Lusifa ni lingine na nitalifundisha.

Yehudiel inamaana ya Mungu wa Wayahudi au kwa Kiingereza ni God of the Jews.

Elah Yisrael, Mungu wa Waisrael, soma (Ezra 5:1)
Elah Yerushelem, Mungu wa Jerusalem (Ezra 7:19)

Vivyo hivyo, Mungu alimtenga na au muumba Malaika Yehudiel kuwa Malaika atakae ilinda Taifa la Israel.

Kama mawakili wa Mungu walitumwa duniani kutoka mbinguni, kuchukua au kuleta maamuzi ya Mungu, juu ya wanadamu katika kutimiza adhabu ya Mungu kwa wanadamu, na katika kuwafundisha wanadamu (Kutoka 12:23; Zaburi 104:4; 2 Samuel 24:16; 2 Falme 19:35; 1 Nyakati 21:16; Matendo 12:23; Ebrania 11:28; 1 Kor. 10:10).

Ukiangalia matatizo kati ya Israel na Mataifa yanao izunguka, utagundua kuwa, hata itokee nini, hayo mataifa ya Kiarabu kamwe hayata weza ipiga Israel. Hebu jiulize, nchi hizi za Jordan, Syria, Lebanon, Misri, Ukanda wa Gaza na Golan Heights. Sababu ni hii, Mungu aliumba Maialka hususan kwa kuilinda Israel.

Tafsiri nyingine ya Malaika Wakuu saba ni kuwa wao ni Roho Saba za Mungu zinazosimama mbele za Mungu, na zilizotajwa katika kitabu cha Ufunuo 1:4; 3:1; 4:5; 5:6;

Malaika Wakuu Saba wanasemekana ni walinzi wa mataifa na nchi, na wanahusika, na masuala, na matukio yanayozizunguka, ikiwa ni pamoja na siasa, masuala ya kijeshi, na biashara, na uchumi. (Yoshua 5:13-15).

Vyeo mbalimbali vya Jeshi la Mbinguni

Malaika wana vyeo, uwezo na nguvu zinazotofautiana katika utendaji wa kazi mbalimbali. (Zekiel 1:7-11; Daniel 10:13; 12:1; 1Thesalonike 4:16; Yuda 1:9; Efeso 1:22; Kolosai 1:16).

MALAIKA WATUMISHI WATUMIKAO

"Malaika, angels" au malakhim, yaani, "malaika wa kawaida "plain" angels"(angeloi, wingi wa angelos, i.e. mjumbe (messenger) au wakili wa balozi, ubalozi (envoy), ni daraja la chini sana la malaika, na ndilo linalofahamika sana kwa watu wengi. Wanahusiana sana na mambo ya viumbe hai. Katika aina hii ya malaika, wapo wa namna nyingi tofauti tofauti, wakiwa na kazi mbali mbali. Hutumwa kama wajumbe kwa wanadamu. Malaika hawa ni wa karibu sana kwa ulimwengu wa vitu na wanadamu. Wana peleka maombi kwa Mungu na Majibu ya Mungu na ujumbe mwingine toka kwa Mungu kwa wanadamu. Malaika wanao uwezo wa kuwakaribia malaika wengine wa ngazi yoyote ile na kwa wakati wotote ule. Ni wanaojishughulisha sana na jamii kuwasaidia wale wanaoomba msaada katika mazingira magumu ya kimwili; mfano, katika ajali, vizuizi au vikwazo vya kutoka mahali kwenda mahali pengine (gerezani).

Usikose SEHEMU YA TATU itakayo zungumzia MALAIKA MKUU GABRIEL na kazi zake.

0672870833
Maombi na maombezi kwa watu wote

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes