Headlines

MJUE MNYAMA NGEKEWA

#CHAKUSHANGAZA #WIKIHII.
MFAHAMU "NGEKEWA"

MNYAMA MWENYE BAHATI YA KUPENDWA NA WANYAMA WENGINE ,
KAMA UMEWAHI KUSIKIA NENO "NGEKEWA" BASI LIMETOKANA NA MNYAMA HUYO.
Mnyama anayefahamika kwa jina la kigeni Capybara ambapo kwa kiswahili huitwa Ngekewa ni mnyama mwenye ukubwa wa sentimita 134 na uzito unaokadiliwa kuwa kilo 66 anapokuwa mkubwa na mnyama huyu asili yake ni nchi ya America ya kusini.

Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha, hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.
2. Ni mnyama ambaye anapenda kukaa karibu na maji na anapojisi hatari hulazimika kukimbilia ndani ya maji na ana ujuzi mkubwa wa kuogelea.
3. Akiwa ndani ya maji anaweza kutumia dakika tano bila kuibuka ambapo hubana
pumzi ndani ya maji anapokwepa hatari ya kushambuliwa na adui yake.
4. Huyu Ngekewa ndio mnyama anayependwa na viumbe vingi vya porini na majumbani.
Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.
5. Kwenye kamusi ya lugha ya kiswahili neno Ngekewa mbali na kumzungumza huyu mnyama pia limetafsiliwa kama bahati au yenye bahati na ndio maana hata mtaani mtu mwenye bahati huambiwa ana ngekewa.
Asili ya maana ya neno ngekewa ipo katika kupendwa kwa huyu mnyama na viumbe mbali mbali hata vile vya hatari.

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

Mhubiri 9:11

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes