Headlines

Nyota ya mafanikio

SOMO;-NYOTA YA MAFANIKIO.
Maana yake.Nyota ya mafanikio ni ile hali ya kupenya katika maisha ya mwamini au ya mtu aliyeokoka.Hapa nimejikita kufundisha NYOTA YA MAFANIKIO hasa kwa mtu aliyempokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
Wapendwa kila mtu anapozaliwa huwa ana nyota yake ya mafanikio,Mfano mzuri tunajifunza kwa Bwana wetu Yesu Kristo katika kile kitabu cha Mathayo2:1-2Yesu alipozaliwa katika Bethlehem ya Uyahudi zamani za mfalme Herode,tazama mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu,wakisema,yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki,nasi tumekuja kumsujudia.

MAELEKEZO YAKE AU MAFAFANUZI YA MAANDIKO HAYO.
Baada ya Yesu kuzaliwa katika mji wa Bethlehem ya Uyahudi,Mamajusi wa mashariki warifika Yerusalemu ili kumuona yeye aliyezaliwa.Je! unadhani ni kipi kilichowasukuma kwenda Yerusalemu?,Biblia inaweka wazi swala hili kuwa ni kwasababu waliiona NYOTA yake huko mashariki.

Hawa mamajusi wamo katika kundi la watu wenye mali na wenye hekima na wataalamu.Baadhi yao walikuwemo watu watawa,waliojifunza na kuchunguza mambo ya asili.Katika kundi la watu wa tabia hii ndimo mamajusi hao walitoka kuja kumuona Yesu.

UNADHANI NI KWA NINI MAMAJUSI WALIIONA NYOTA MASHARIKI NA WALA SI PANDE NYINGINE?.
Ukisoma Mathayo2:2 "Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki........".Ukisoma vizuri mstari huu utagundua kuna siri kubwa mahali pale.Siri mojawapo ni kuwa NYOTA YA MAFANIKIO YA MWANADAMU AWAYE YEYOTE HUWA INAANZIA MASHARIKI KUONEKANA.Kwa sababu ili mwanadamu aweze kufanya shughuli zake,anategemea mashsriki iachilie nuru yake au mwanga wake wa jua ili afanikishe mambo yake.Kuna usemi mmoja unasema hivi"SIKU NJEMA UONEKANA ASUBUHI" inamaanisha kuwa bila kuliona jua asubuhi likiachilia mwanga(nuru) wake bado haijawa siku njema.

ELEWA HILI LITAKUSAIDIA KWAMBA NYOTA YA MAFANIKIO YA MTU HUWA INASHANGAZA WATU WENGINE.
Ukisoma Mathayo2:3,4 tunamuona Mfalme Herode anafadhaika sana na kuamua kukusanya waandishi na watu mbalimbali ili kutafuta habari kwao,kwamba Yesu alizaliwa wapi,hii inamaanisha kuwa nyota Yesu Kristo ilikuwa inaweza kutishia watu wakubwa na wenye vyeo.

Wapendwa nyota ya mtu aliye okoka inaweza sababisha watu wenye vyeo kutikisika sana na kuchanganyikiwa sana kwa sababu nyota yako iking'aa katika huduma yako utaanza kufanya mambo makubwa na yakutisha,Nyota yako iking'aa ni lazima mambo makubwa yatokee haijalishi ulisoma au haukusoma Mfano mzuri Daudi aliyekuwa mchunga kondoo nyota yake ilipong'aa haikujalisha mazingira aliyokuwa nayo bali ilipong'aa akawa mfalme(Zab113:6-7).

NYOTA YA MAFANIKIO YA MTU ALIYE OKOKA HUWA IMEMTANGULIA .
Katika Mathayo2:9-10"Nao waliposikia maneno ya mfalme walishika njia,na tazama ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia,hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.Nao walipoiona ile nyota, wakafurahi furaha kubwa mno".

Ndugu zangu ni maombi yangu kuona leo nyota yako ya mafanikio ikisimama mbele yako katika maeneo yote:-
-Ikisimama katika ndoa yako,
-Ikisimama katika huduma yako,
-Ikisimama katika kazi yako,
-Ikisimama katika watoto wako,
-Ikisimama katika elimu yako,
-Ikisimama katika biashara yako na katika kila utakalo tia mkono wako kulitenda ni lazima kufanikiwa kwa jina la Yesu.

ZIFUATAZO NI DALILI ZA MTU MWENYE NYOTA YA MAFANIKIO.
1.Kuwa na kibali kwa watu wote,
2.Kuwa na furaha wakati wote,
3.Mtu mwenye kuthamini watu wote,
4.Kuwa mkarimu kwa watu wote,
5.Kuwa ni mtu mwenye bidii na kujali mambo yenye utukufu wa Bwana,
6.Mtu mwenye huruma kwa watu wote,
7.Mpenda haki na mtenda mema,
8.Mtu wa rehema na msamaha,
9.Kuwa na ushirikiano na wengine bila kujali elimu nakadhalika,
10.Ni mtu mwenye maono makubwa,
11.Mtu mwenye kujitoa sana kwa kazi ya Bwana na kwa watu wote pia.
12.Mtu mwenye kumtegemea sana MUNGU na kujiamini sana bila kuwategemea wanadamu.
13.Mtu mwenye msimamo na yale anayoyafanya.....................
UNADHANI NI KWA NINI WAKRISTO WENGI LEO WANATESEKA NA MAISHA MAGUMU?.Hii ni kwa sababu nyota zao za mafanikio zimeibiwa.Ni kweli wameokoka vizuri sana lakini kwa kukosa maarifa nyota zao za mafanikio zimeibiwa, na hakuna asemae rudisha,watumishi wengi wa Mungu kwa sababu hawana macho ya kiroho hawataki mafundisho ya namna hii ya Nyota,Ndio maana kanisa la leo linaendelea kuteseka.
Wadada wengi wamekuwa wakilia sana na kuangua vilio vikuu makanisani hawana msaada maana nyota zao zimeibiwa kwa mantiki hiyo kuolewa limekuwa jambo gumu.Ushuhuda Dada mmoja akaniambia mtumishi umri wangu umekwenda sana nimekuwa nikiombea hitaji la kupata mme lakini mpaka sasa sijaona dalili yoyote ya kupata mme,na nimefanya maombi ya aina zote lakini hakuna chochote,na ninahisi kuacha wokovu hayo ni maneno ya binti.Dada huyu alikuwa na kazi yake nzuri lakini kwa sababu ya kuibiwa na kufungiwa nyota yake ya mafanikio juu ya swala la kuolewa kwa hiyolilikuwa swala gumu sana kwake kumpata mme mwema.Ushuuda wa pili ni Binti mmoja baada ya kusumbuliwa sana na shida hiyo ilifikia kipindi akaanza kuwahonga wanaume pesa ili wamuowe kwa maana alikuwa ameomba kwa muda mrefu kwa habari ya kumpata mme mwema lakini jambo hili lilikuwa gumu kwake maana nyota yake ilikuwa imezikwa makaburini.Ashukuriwe Mungu watu hawa walipokutana na mafundisho haya wote walifunguliwa na wakaolewa.

Vijana wengi wa kiume na wakike nyota zao za mafanikio zimeibiwa bila wao kujua.Ndugu zangu kazi ya kanisa ni kuwafungua watu kutoka katika nguvu za giza kwa jina la Yesu Mathayo10:8 & Luka10:19.

DALILI ZA MTU ALIYEIBIWA NYOTA.
1.Roho za kukataliwa,
2.Roho za uharibifu wa vitu,
3.Roho za ugomvi,
4.Roho za chuki,
5.Roho za kutokusamehe,
6.Roho za uchoyo,
7.Roho za hasira,
8.Roho za uonevu,
9.Roho za umasikini,
10.Roho za kutojiamini,
11.Roho za ubinafsi pamoja na kila kitu ambacho kinazuia usiende mbele kwa namna zote.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes