Headlines

UNYENYEKEVU NA SIFA ZAKE

Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati 
wake;
1 Petro 5:6

Mtaka cha uvunguni sharti ainame. Kama unataka kua juu sharti uombe UNYENYEKEVU sio ,unapoteza Muda kuomba uinuliwe.
Unyenyekevu ni tabia ya kimungu.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29

Unyenyekevu ni kujishusha ni kuto kujihesabia haki kwa matendo ya njee.
tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wafilipi 2:8

Mungu Anatabia ya kuwapinga Wenye kiburi daima.
Kiburi ni kumpa shetani nafasi moyoni mwako.
SIFA ZA MNYENYEKEVU
1. Utiifu/utii
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wafilipi 2:8b
Utii umejificha katika UNYENYEKEVU ukiona kua wewe sio mtii jua huna unyenyekevu.
2. Uvumilivu
Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Warumi 2:4
Kama Mungu asingelikuwa mvumilivu watu wengi angesha kufa vibaya. Uvumilivu wake ni anajua ipo siku utajua makosa yako utubu uwe wake.
3. Hukwazwi
Mnyenyekevu ana amani mda wote.hata akikwazwa anasemehe haruhusu kabisa
shina la uchungu kuchipuka ndani yake.

mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Waebrania 12:15

4. Hujikwezi
Hujikwezi kabisa yeye ametulia tulii ,hataki kujihesabia haki kabisaa.
Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
Marko 10:18.
Yesu hawakutaka kabisa kukwezwa,kwanini?! alijifunga UNYENYEKEVU

5. Unatetewa Mungu anakuinua.
Unapo jifunga UNYENYEKEVU ni kazi ya Mungu kupigana na adui zako ipasavyo.

Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.
Esta 8:5

6. Kib
Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia.
1 Samweli 2:26
Mama yake Samweli hana amekua mnyenyekevu mno hata akapata kuomba Mungu apate mtoto wa kiume.
Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana.
1 Samweli 1:14-15

By
Ev.Mchome
0672870833


ali

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes