Headlines

Mkamate sana Elimu

BIBLIA INASEMA: MKAMATE SANA ELIMU USIMWACHE AENDE ZAKE

Elimu ni nini?
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Mithali 4:13
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.

Kitabu cha Mithali kinajazwa na maagizo yaliyotolewa na Sulemani kwa wanawe. Mwana huhimizwa kujifunza kutokana na maagizo haya, na matokeo ya matumizi ya ujuzi kujifunza inaitwa hekima. Maandiko yanasema mengi juu ya mchakato wa elimu, na huanza na mzazi wa mtoto.

Biblia inaendelea kutufundisha kuwa:

Mithali 4: 10 -12
Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.

Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya msingi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, za kijamii na za kiutamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.

Inatia moyo kujua kwamba Mungu Mweza-Yote anataka kutufundisha. Anasema hivi kujihusu: “Mimi Mungu , ni Mungu wako, Yeye anayekufundisha ili ujifaidi mwenyewe, Yeye anayekufanya uende katika njia unayopaswa kutembea ndani yake.” (Isaya 48:17) Naam, Mungu ametuonyesha njia hiyo kupitia mfano na mafundisho ya Mwana wake, Yesu Kristo. Mafundisho yake yaliboresha maisha ya watu wengi waliomjua alipokuwa duniani, na yanaboresha maisha ya watu wengi leo. Kwa nini usitenge wakati ili ujifunze mengi kuhusu mafundisho hayo?

Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.
Elimu sio kwa watoto walio mashuleni tu bali hata wewe mtu mzima elimu ni kitu cha msingi kwako katika kukufanya ujue vitu vingi .

Wengine hawatakiwi kujua mambo ili wabaki kama walivyo katika hali zao.
Yani kifupi ujinga ni gereza katika maisha ya mtu. Ukiona mtu hafanikiwi jua wazi yupo katika Gereza la elimu.

Maombi na maombezi kwa watu wote
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes