Home > Maombi > Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni
Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 05, 2019 • Maombi • Comments : 0
BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze kuhusu sala maarufu sana ambayo kila Mkristo anaifahamu lakini wengi sana hawajui maana ya sala hiyo..
Mathayo 6:9-13 ''Basi ninyi salini hivi; BABA yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Kuna ndugu mmoja aliniuliza kwamba kwanini waliookoka huwa hawasali sala hii? Nikamjibu kwamba hakuna ambaye ameookoka ambaye huwa haisali sala hii. Maana wateule wa MUNGU huisali sala hii katika maana yake. maana ya hiyo sala sio kuirudiarudia bali ni mwongozo wa maombi ambapo bila hata kufundishwa ukiomba tu katika ROHO MTAKATIFU utajikuta tu unaomba kama sala hiyo ilivyo.
Maana katika maombi ya kila siku tunajikuta tu tunaanza kujitakasa, kumshukuru MUNGU, kusema hitaji letu, kuhabribu hila za adui, Kumshukuru MUNGU. Pia maombi yote sahihi huombwa kupitia katika jina la YESU KRISTO pekee(Yohana 14:13-14)
Maana ya sala hiyo ya BABA YESU ni hii.
ijue na ikusaidie kuomba hata masaa 4 bila kuchoka maana kumshukuru MUNGU tu unaweza kutumia muda mwingi, pia kupeleka hitaji unaweza kutumia muda mwingi pia na kama ukiomba katika ROHO utajikuta unaomba au unawaombea hata wale ambao hukupanga.
1. , BABA yetu uliye mbinguni: Maana yake kwanza Lazima ujue unayemuomba yeye yuko mbinguni hivyo maombi yako elekeza kwake yeye tu ambaye ndio aliyetuumba.(Mithali 3:5-6,Waebrania 13:6)
2. Jina lako litukuzwe :Unatukuza jina la MUNGU maana jina hilo ni tofauti na majina mengine au ni safi kupita yote hivyo lina dhamani kubwa kuliko yote, Unamtukuza MUNGU pia kwa kumshukuru kwa matendo makuu aliyokutendea ikiwemo kukulinda, kuwalinda ndugu zako, marafiki zako na kukubariki.(Zaburi 34:1, Zaburi 92:1, Matendo 16:25, Ufunuo 19:5b)
3. Ufalme wako uje: Maana yake unaita ufalme wa MUNGU ushuke hapo ulipo, maana yake unaita nguvu ya MUNGU ili kama adui katawala eneo hilo aondoke, unalitaka eneo ulilopo kwa kuuita ufalme wa MUNGU, Unatiisha kila kitu kwa jina la YESU.(Mathayo 6:33)
4. Mapenzi yako yatimizwe – Mapenzi yake yatimizwe jinsi yeye apendavyo na sio wewe upendavyo unajua unapoomba kitu lazima kuwe na ushawishi wa kile kitu unachohitaji hivyo kuna ushawishi wa jambo lile kwa Yule unayehitaji akupatie kwa kumsifia kumbembeleza kumuomba kwamba kweli utakitunza na kukilinda kile unachohitaji kumueleza nini madhumuni yako ya kuomba na unatarajia kufanyia nini akikupatia na jinsi kitavyokuwa na manufaa kwako. pia je utampa utukufu MUNGU baada ya kukupa ulichoomba?(Yeremia 32:27)
5. Hapa duniani kama huko mbinguni – Hayo manufaa yawe kwako hapa duniani na mbinguni je utabaki kuwa wake akikupatia je utashirikisha wengine baada ya kupata je kunafaida kwako na kwengine na watarudisha shukrani kwake na kuwa wake hao utakaofaidika nao nk. na Je utabaki na KRISTO hata ukiwa na baraka zake?(Isaya 64:8)
6. Utupe leo riziki yetu – Ukishafikia hapo unatakiwa uombe kubaki nayo au kubaki nayo hayo maombi kila siku kwa kung'ang'ania ili usinywangwaye na adui ni kama vile kuweka mambo au vizingiti vya kuzuia yasing’olewe na adui maana yeye yuko na anahitaji kuiba kutoka kwako. Ndio maana kuna Damu ya YESU kukusaidia, ndio maana kuna Malaika wa MUNGU kukusaidia, na ndio maana kuna ROHO MTAKATIFU kukujulisha pia kuna mamlaka katika neno la MUNGU ili tu kuhakikisha unapata riziki yao unayoiomba kwa BABA wa mbinguni.(1 Yohana 1:2)
7. Utusamehe dhambi zetu –Kujitakasa kwa kufanya toba juu yako na familia na jamii kwa ujumla maana hapa anaongelea dhambi zetu na sio dhambi zako kuna tofauti ya toba yako binafsi na ya jamii nzima. Kutubu ni kumruhusu MUNGU ashughurike na wewe. kutubu ni Kutaka kibali kwa MUNGU. Tunatubu kwa MUNGU kupitia YESU KRISTO pekee.(Isaya 43:25)
8. Kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye – Fanya toba ya kusamehe wale walio kukosea kwanza ili upate kibali nawe cha kuwa huru maana nira ile uliyoweka kwa mwenzako nawe imewekwa kwako leo hivyo unapoondoa nira kwa mwenzako nawe kwako inaondolewa.(Mathayo 6:14-15)
9. Na usitutie majaribuni – Omba usiingie katika majaribu maana huko kuna kushindwa kutoka hivyo ni vizuri kuweka kinga ya kutokuingia ili uweze kushinda vita hivi ambavyo adui yuko kila mara akilite majaribu juu yetu kwa kuwa yeye ni baba wa majaribu.(Yakobo 1:12-16)
10. lakini tuokoe na yule mwovu – Maana si kwa nguvu zetu tutashinda bali kwa mkono wenye nguvu wa BWANA YESU maana anasema tumtegemee yeye tu maana atatuokoa na adui na atatuvusha katika hatari na kutulinda ijapokuwa tutakula sumu lakini tutaishi maana yeye ndiye aliyefanyika laana kwa ajili yetu ili tukombolewa kwa kufa katika kifo cha laana pale msalabani ili kwa laana yake sisi tuhesabiwe haki ni kwa kumkiri tu na kumkata shetani tunapopata ule wokovu mkuu katika yeye KRISTO YESU BWANA wetu.(Warumi 16:20)
Naamini umeelewa kwa sehemu kubwa na kuanzia sasa kupitia sala hiyo ya mwongozo unaweza ukaomba hata masaa 3. Ubarikiwe sana
''Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12''
By
EV.MCHOME
0672870833
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment