Headlines

Kanuni za maombi



ISAYA 28:13
"Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......"

Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu
Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo.

HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI:
Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi
{ i } Ni kuomba
Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako.

{ ii } Ni Mungu kusikia maombi yako.
Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi.

{ iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako.
Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yako.

{ iv } Ni Mungu kukujibu.
Mungu akishamaliza kutafakari maombi yako hatua inayofuata ni yeye kuyajibu maombi hayo.
Naamini katika hatua hizi za maombi kupitia umenielewa. Usije ukafikiri kwamba ukiomba tu Mungu atajibu maombi yako hapana ni mpaka asikie kisha atafakari hayo maombi, kisha ndipo sasa akujibu haleluyaaaa.
    MATHAYO 7:7-8
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa;

👉Nataka ujue kwamba tatizo la kutojibiwa maombi yako haliko kwa Mungu bali liko kwako mwenyewe unayeomba kwa sababu ya kutokujua KANUNI za Mungu za kuomba.

 Kuna vitu ambavyo vimejificha hutaweza kuvipata mpaka umevitafuta wewe kwa njia ya maombi. Na kuna mambo yako maishani mwako ambayo yamefungwa kwahiyo hayataweza kufunguliwa mpaka umebisha kwa Mungu kwa njia ya maombi.
Sasa ngoja nikupitishe kwenye hizo kanuni chache,

KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA:

1 Muombaji sharti usiwe mwenye dhambi.
    YOHANA 9:31
"Tunajua kwamba Mungu HAWASIKILIZI watu wenye Dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake" ( Tafsiri ya Habari Njema )
👉 Umeona kwamba Neno la Mungu limeweka wazi kabisa kwamba unapokuwa mwenye dhambi Mungu hatakusikiliza kabisa wakati unamuomba. Kwahiyo ili Mungu ajibu maombi yako ni lazima uishi maisha ya Utakatifu, achana na kufanya dhambi kwa siri/kujificha.

2 Muombaji sharti ukae ndani ya kristo Yesu.
    YOHANA 15:7
"Ninyi MKIKAA Ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, Ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"
👉 Mungu hawezi kuyajibu maombi yako kama wewe hujakaa ndani ya Yesu Kristo. Ninaposema kukaa ndani ya Yesu Kristo maana yake nilazima Uokoke sawa.

3 Muombaji sharti Uombe kwa Bidii sana.
   YAKOBO 5:17
"Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, AKAOMBA kwa BIDII mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita"
👉 Eliya aliomba kwa bidii sana kuhusu mvua kutonyesha na Mungu akajibu hayo maombi yake.
   MATENDO 12:5
"Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa LIKAMWOMBA Mungu kwa JUHUDI/BIDII kwa ajili yake"
👉 Hapa tunaliona kanisa likimuombea kwa bidii Petro wakati alipokamwatwa na mfalme Herode na kutokana na kanisa kuomba kwa bidii Mungu alisikia maombi yao akawajibu na kumtoa Perto ndani ya gereza.
👉 Kuomba kwa bidii maana yake ni kuomba bila kukata tamaa aidha kwa kukatishwa na wanadamu au mazingira.
Huwa ili Mungu ajibu maombi yako  ni lazima aione bidii yako wakati unaomba, lakini ukiomba kwa ulegevu hawezi kukujibu
0672870833
Maombi na maombezi 

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes