Headlines

UNYENYEKEVU

UNYENYEKEVU HULETA NEEMA.
   (Usipite bila kusoma)
Kwanza nimegundua ya kwamba kadri mtu anavyozidi kuwa mnyenyekevu kwa Mungu na hasa kwa watumishi wa Mungu ndivyo ambavyo Mungu humwinua na kuzidi kumpandisha.
 Na kadri mtu anavyo jikweza na kutokuwa mnyenyekevu ndivyo ambavyo anaendelea kudidimia na kukutana na wakati mgumu kadri siku zinavyozidi kuendelea.
 Biblia katika Yakobo 4:6 inasema kuwa Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa NEEMA wanyenyekevu., Kumbe siri ya kupata neema nyingi kutoka kwa Mungu ni kuwa mnyenyekevu.
 Kadri unavyozidisha kiwango cha unyenyekevu ndivyo unavyo jizidishia kiwango chako cha neema.
Kuna watu Mungu akiangalia kesho yao anachukua muda kujibu maombi yao ya kuwabariki maana anaona kabisa huyu akibarikiwa na kufanikiwa atakuwa na kiburi, maringo unyenyekevu wote utaisha na hata Mungu mwenyewe naweza kumkosa ndio maana Mungu wakati mwingine anakuwa kimya tu licha ya maombi mengi anayo ombwa maana anajua mioyo yetu kuliko tunavyo jijua sisi wenyewe.
1. Unyenyekevu ni hali ya mtu kujishusha licha ya hadhi, haki au kiwango alicho nacho.
2. Unyenyekevu ni hali ya mtu kuonyesha heshima na kujali kwake kwa watu wengine bila kujali ukubwa wala udogo wa kiwango chao cha maisha nk.
3. Unyeyekevu ni hali ya kuudhibiti moyo wako usitawaliwe na kiburi, jeuri, majivuno wala dharau kwa mtu wa aina yeyote.
4. Unyeyekevu ni hali ya kuinua kiwango cha thamani ya watu wengine na kuwaleta katika kiwango chako na kuwa ona kuwa wao pia wana thamani kubwa kama wewe ulivyo.
Wafilipi 2:3b
...bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yako.
5.kujishusha na kunyenyekea si utumwa na Wala si kujaa huzuni nyingi Bali  Ni kupondeka moyoni kwa kujali, kuheshimu na kuonyesha nidhamu kwa aliyekuzidi MAMLAKA.
Mara nyingi Mungu huguswa na moyo uliopondeka kabisa uliojaa unyenyekevu.Hata hivyo wakati Hali yako ya ndani ikiwa imetulia kabisa ,imepondeka pondeka  na ukiwa msafi kbsa yaani umefanya Toba Ni RAHISI MUNGU KUZUNGUMZA NAWEWE aidha kupitia watumishi wake yaani NABII, au kuzungumza nawewe kwa njia za mafunuo au maono,ndoto,au kusikia sauti yake ,na njia nyinginezo.
NB:
Unyenyekevu hubadili historia,huleta thamani, huinua , huleta NEEMA na mafanikio yasiyotarajiwa .
       HIVYO TUJIFUNZE KUNYENYEKEA MANA TUTAPATA THAWABU KUBWA MAISHANI.

x

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes