Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu
haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu.
Marko 10:27
Ni wazi kua hakuna jambo lolote lililo gumu la
kumshinda Mungu.
Watu wengi wamekua wakikosa kutendewa miujiza kwa
sababu tu wamekosa kumwamini Mungu kua anazo nguvu za kuwaokoa katika misiba
waliyo mayo.
Ngoja nikufundishe kidogo imani ni nini?
Ni kua na uhakika kabisa,kwa asilimia zote.
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni
bayana ya mambo yasiyoonekana.
Waebrania
11:1
Unapo kosa kua na imani amefunga mlango wa kumruhusu
Mungu ,kutenda jambo kwako.
Mungu anataka moyo wako.kitu unacho kiamini ni kwamba
kitu hicho umekipa moyo wako.
Na kukipa kitu Moyo ni kuanza kukitegemea hicho.
Ndio maana Mungu akawa mkali akisema amelaaniwa
mtu yule amtegemeaye Mwanadamu.
Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Yesu aliponya watu kwa kua walikua na imani.Hata alipo
kwisha kuwaponya alisema Imani yako imekuponya.
Imani inamruhusu Mungu kukufanyia jambo.
Imani yako ukiiweka kwa Mungu ni wazi hakuna litakalo
shindikana .
Ndio maana neno linasema
Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake
aaminiye.
Marko 9:23
Ukiwa na imani Nguvu ya Mungu inafanya kazi ndani
yako.
Wanafunzi wa Yesu walikua wakipitishwa na Yesu katika
fundisho la imani, kama funguo ya kufanya mambo ambayo wengine wasije weza
kufanya.
Wanafunzi wa Yesu walipo kosea mahesabu Yesu
alikasirika
Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha
wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu.
Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali
mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako
neno lisilowezekana kwenu.
Mathayo 17:19-20
Kitu ambacho kili fanya wanafunzi wa Yesu kushindwa
kumtoa pepo ni? Upungufu wa imani zao.
Kitu kinacho kufanya uendelee kukaa katika hali uliyo
nayo ni upungufu wa imani.
Usipo weka imani kwa Mungu mambo mengine hayata
wezekana kwako.
Weka imani kwa Mungu, hakuna litakalo shindikana
kwako.
Post a Comment