Home > Torati > Je wajua Amri kumi na sheria 613
Je wajua Amri kumi na sheria 613
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 05, 2019 • Torati • Comments : 1
Ningependa ufahamu kuwa katika nyakati za agano la kale “first dispensation”, ilikuwa, huwezi kuwa mkamilifu kwa kushika amri kumi tu bila kushika na sheria nyingine 613 na kuzitendea kazi hukumu zake. Mtu asiyetendea kazi yote yaliyoandikwa katika torati, alikuwa amelaaniwa;
UTHIBITISHO:
Galatia 3:10 tunasoma, “Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika YOTE yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.”
Kumbe Mungu aliwaagiza wana wa Israeli washike torati yote na sio kushikilia siku moja to ya Jumamosi kama ambavyo Wasabato wa leo wanavyo fanya;
UTHIBITISHO:
Walawi 20:22 tunasoma, “Basi zishikeni amri zangu ZOTE, na hukumu zangu zote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kuiketi isiwatapike.”
UTHIBITISHO:
Pia Kitabu cha Kutoka 35:10 Biblia inasema, “Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya haya YOTE ambayo Bwana ameagiza.”
Sasa basi, Wasabato wao wanang’ang’ania sheria ya kushika sabato na makatazo ya baadhi ya vyakula katika nyakati hizi za Agano jipya, Watu hawa ni wazi kabisa, hawapo kwenye fungamano la Agano Jipya, maana tumeona bayana kwamba, sheria hii, Bwana hakuipitisha, kwa kuwa ilikuwa ni ishara, iliyokuwa ikimuashiria Yeye kama (sabato) pumziko la kweli la kiroho (Wakolosai 2:16-17).
Hivyo kushika sabato ni kukataa sheria ya Kristo na kuikubali sheria ya Musa. Na sharti la sheria ya Musa (torati) ni kwamba, ni lazima mtu ashike Amri kumi zote, sheria nyingine 613 na hukumu zake.
Mfano; sheria ya kushika sabato ilikuwa na hukumu yake, pale ambapo mtu, alionekana kutoitimiza, yaani alipaswa kuuawa;
UTHIBTISHO:
Kutoka 31:14 tunasoma, “Basi mtaishika hiyo sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa, kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.”
UTHIBITISHO:
Kitabu cha Kutoka 35:2 Biblia inasema, “Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni sabato ya kustarehe kabisa kwa Bwana; mtu awaye yote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo ATAUAWA.”
Kama Mungu alitoa agizo la kushika sabato, na pia akatoa agizo kuwa atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe; Je ni wasabato wangapi leo tunawaona wanafanya kazi Jumamosi, kama kuna usahihi wowote mbona hatuoni wakiitekeleza hukumu ya kuuana? maana ni agizo la Mungu mwenyewe.
Yakobo 2:10 inasema mtu akiishika sheria yote, akajikwaa katika neno moja tu, amekosa juu ya yote.
NDIO MAANA YESU ALIIVUNJA SABATO:
Wapendwa! hii ndiyo sababu iliyompelekea Bwana Yesu kuivunja sabato, baadhi ya sheria na hukumu zote; kwa kuwa ilikuwa ni huduma ya mauti (2 Wakorintho 3:7).
EV.MCHOME
0672870833
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Torati ni kongwa ngumu sana.Ashurukuriwe Mungu kwa upendo wake,aliyetuokoa kwa neema na hata sasa tunaishi kwa neema,hatupo chini ya sheria tena,bali chini ya neema.
ReplyDelete