Headlines

Ufunuo juu ya nyota

Somo:  Ufunuo Juu Ya Nyota:
Nyota Ni Nini?   Hesabu 24:17-18
Ni Aina Ya Neema Kutoka Mbinguni Iliyobeba Kitu Chema Cha Mungu Kutoka Mbinguni, Kinacho Ng'aa Kilichohifadhi Mbaraka Na Baraka Mbalimbali Alizokirimiwa Mwanadamu Na Mungu Aliye Hai.   1 Korintho 2:9-13

 Aina Za Nyota:
Hesabu 24:16-19 2 Petro1:19, Mwanzo 49:8-11, Zaburi 148:3, Isaya 14:12,
 Mathayo 2: 1-9, Ufunuo 8:11, Ayubu 9:7-10.
i.Nyota Ya Utawala.
ii.Nyota Ya Taifa
iii. Nyota Ya Ukoo
iv. Nyota Ya Biashara.
V. Nyota Ya Utumishi.
Vi. Nyota Kifalme.
Vii. Nyota Ya Pakanga.
Viii. Nyota Zilizopigwa Muhuri.
ix. Nyota Za Kusini.
X. Nyota Za Orion
Xi. Nyota Ya Alfajiri.
Xii. Nyota Ya Mashariki.
Xiii. Nyota Za Dubu.
Xv. Nyota Zang'aazo Sana.
Mifano Inayoonyesha Aina Za Nyota  Na Unabii Wake
Kama  Mungu  Aliye Hai  amekukirimia nyota  ya utawala; hii ni kusema kuwa; neema yako au nguvu yako ya uwezesho kutoka mbinguni, ya utawala itakuwa kubwa sana. Popote utakapoenda, utakuwa na bahati ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Kuhusu nyota ya taifa;…. Kila taifa linasifika kwa jambo Fulani la kimaendeleo na kuwapa heshima ya kimataifa. Brazil inasifika kwa umahiri wao katika soka. Tanzania tunasifika kuwa ni; kisiwa cha amani. Na katika Afrika Mashariki, sisi wa-Tanzania tumefanikiwa kulishinda tatizo la ukabila, ukilinganisha na nchi jirani ya Kenya. Hii ni mfano michache ya nguvu ya nyota ya taifa.
Kuhusu nyota ya biashara, hii ni aina ya neema ya asili waliokirimiwa wanadamu na Mungu Aliye Hai. Kimataifa, nchi ya China inaongoza hivi sasa. Kwa hapa Tanzania; kabila la Wachaga wanaongoza katika  neema kubwa ya kufanya biashara. Nabbadhi ya makabila mengine, anainuliwa mtu mmoja mmoja na kuwa kinara katika kabila au ukoo Fulani.
Kuhusu nyota ya utumishi, ukiwa nayo unafanikiwa sana katika kazi yoyote utakayomfanyia Yesu Kristo. Kuhusu nyota ya ufalme, ukiwa nayo, popote utakapoenda, watu watakunyenyekea na kukutumikia, kutokana na mvuto wa heshima yako.
Kuhusu nyota ya pakanga, ukiwa nayo, hii ni nuksi, na popote utakapokuwa, utaharibu mambo. Yaani ukiingia mahali, amani ya mahali pale inachafuka, maana pakanga ni sumu na ni chungu.
Kuhusu nyota zilizopigwa  muhuri; ni aina ya neema aliyonayo mtu inayomfanya asipingike au  asizuilike katika eneo lolote; mfano kiuchumi au kibiashara. Mtu wa aina hii hauwezi kumzuia au kumkwamisha. Watu wa aina hii; wamethibitika, wako imara thabiti katika maisha yao ya kimwili na ya kiroho. Hii ni mifano michache nimekuandikia kuhusu aina za nyota na unabii ukaao ndani yake, ili nikurithishe maarifa haya.
Kuhusu nyota ya alfajiri; mtu mwenye neema hii; anastawi haraka sana, anafanikiwa haraka sana. Na kila jambo jema analifanikisha mapema sana bila jasho au taabu. Akili ya  mtu huyu iafahamu mambo mapema kabla wengine hawajatambua, yeye ameshawahi.
Kuhusu nyota zing’aazo sana; ni aina ya neema ndani ya mtu, inayomsaidia kuwa bora sana kuliko wengine, katika maisha ya kiroho kiuchumi, kijamii au ya kimwili.
Adui Wa Nyota Yako:
Mathayo 2:7-15.
Kumbuka Kila Nyota Ina Adui Wake; Yaani Yule Asiyependa Kukuona Ukifanikiwa  Na  Kustawi. Herode Aliinuka Dhidi Ya Nyota Ya Yesu Kristo....... Epuka Kuwaeleza Watu Aina Ya Herode Siri Zako... Epuka Kushuhudia Ovyoovyo.

Adui Wa Nyota Yako Na Namna Ya Kuwaepuka Ili Wasikudhuru:       Mathayo 2: 1-15

Wako Watu Wengi Wasiopenda Maendeleo Yako Akiwemo Kiongozi Wako Wa Dini Au Familia. Wakati Mwingine Hata Ndugu Zako.... Mwanzo 37:1-9. Inawezakana Unacho Kipaji Fulani. Na Kinasababisha Unasifiwa Sanaa. Sasa Wako Watu Wasiofurahia Hili Na Wanakuchukia Sana.. Nyota Ya Yesu Kristo Ilipoonekana, Herode Aliinuka Sana Na Alitaka Kumuua Yesu Wakati Wa Biblia. Kwa Ajili Hii Epuka Kuwaeleza Watu Ovyoovyo Siri Zako. Epuka Kushuhudia Kila Wakati Jumapili Kanisani Maana Utaamsha Vita Isiyo Onekana Kutoka Kwa Wanadamu Na Shetani Hapo Kanisani. Watu Wengi Hudhani Ni Sifa Kushuhudia Kila Neno, Nakuambia Neno La Kikubwa Ujue Ni Hatari Sana. Mungu Wa Mbinguni Akusaidie Kunielewa Rafiki.
Kuna Mambo Mengine Kwa Usalama Wako Inakulazimu Kuyaficha Kwa Usalama Wa Neema Iliyo Ndani Yako.

Maneno Yaliyo Ndani Ya Nyota Yako:

Habari Zako Zote Za Kiroho, Uchumi Na Kimwili Zimeandikwa Ndani Ya Nyota Yako. Nguvu zako za kiroho, za kijamii, za kiuchumi, za kimwili, za kimwili, za kielimu, za kiutumishi za za uzao zimehifadhiwa ndani ya nyota yako. Sasa hizi ni siri za ufalme wa mbinguni. Vilevile kuwa; siku yako ya kuzaliwa ina uhusiano mkubwa sana na nguvu za nyota yako, kwa jinsi Mungu Aliye Hai Alivyokukirimia. Ayubu 3:1-9, 1Kor 2:10-13,  Mathayo 13:10-13
 Fahamu Siri Zinazokaa Ndani Ya Nyota Yako:-
- Maisha Yako Yote Ya Sasa Na Ya Baadae Yameandikwa Ndani Ya Nyota Yako.
- Uso Wako Ni Ubao Unaoonyesha Haya Kama Ubao Wa Matangazo.
- Ufunuo 7:2-3, Kipaji Cha Uso Wako Pameandikwa Kila Neno Lako.
- Ukiyajua Maneno Ya Nyota Yako Itakusaidia Kujitambua Kuwa Wewe Ni Nani?.
- Siri Ya Nyota Yako Ndio "pasword" Au (Nywila) Ya Kuingia Ndani Ya Baraka Zako.
- Nani Anajua Habari Ya Nyota Yako? Au Je Nani Wanajua Maneno Ya Nyota Yako???
- Nani Walikuwepo Ulipozaliwa??
- Tafuta Mtumishi Mwenye Kuyajua Haya Na Mwenye Nguvu Na Mamlaka Kama , Ili Akuombee Ulinzi, Halafu Umpe Sadaka Ya Shukrani.

Tunza Sana Siri Za Nyota Yako Ili Uepuke Maangamizi. Hosea 4:6 " Watu Wangu Wanaangamizwa Kwa Kukosa Maarifa. Yeremia 3:15, Nakupa Leo Maarifa Haya Ambayo Nimekuandikia haya, Uyashike Ili Upate Kuzifanikisha Njia Zako, Na Yesu Kristo Wa Nazareth Akulinde Na Kukuhifadhi..,...... Amen
 EV.MCHOME
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes