USIPITE BILA KUSOMA, HAKIKA UTAJIFUNZA MENGI...!!
Ktk nchi moja palikuwa na mfalme dwaalimu,akiwaongoza wananchi wake kwa kuwanyanyasa na kuwaonea.
Hamjali mtu wala kumuhurumia yeyote yule,,,
Siku moja usiku alipokuwa amelala aliota mwezi umegawanyika sehm mbili unatembea pmj nae.
Alipoamka asbh ile ndoto ilikuwa ikijirudia kichwani kwake,lkn ikawa kila anapolala iwe mchana ama usiku ndoto ile humjia.
Mfalme akapatwa na hofu akawauliza washauri wake nn afanye,,wakamshauri awaite watu wenye kufasiri ndoto ( wanajimu )
Ili wamfasirie juu ya hiyo ndoto yake inayojirudia kila anapolala.
Mfalme akaagiza watafutwe wanajimu wote nchini wapelekwe kwake.
Wakatafutwa wakachukuliwa wale wakubwa wao wakapelekwa kwa mfalme.
Mfalme akawasimulia ndoto yake na akawataka awafasirie inamaana gani ndoto yake.
Wale wanajimu wote kwa umoja wao wakamuambia ya kuwa ndoto yake ina maanisha ya kuwa atakufa baada ya siku thelathini.
Mfalme akapatwa na hofu na akaogopa sana,,,akawaambia wale wanajimu kuwa atawafunga jela.
Lkn mfalme ikawa anahofu kila siku zinavyoenda akazidi kuhuzunika na kunyong'onyea.
Zilipoisha zile siku thelathini yule mfalme akafa.
Siku chache baadae akaingia mfalme mwingine ktk mji ule ikabidi awaite wale wanajimu ili awaulize wanajuaje mambo ya siri.
Wale wanajimu wakaitwa wote na wakaulizwa walijuaje kuwa mfalme atakufa baada ya siku thelathini.
Lkn ktk kikao hiko alikuwepo mmoja wa matabibu wanaojua tiba ( dokta ) ikabidi aingilie kati mjadala ule.
Yule tabibu akawaambia kuwa wanajimu ni waongo kwani hawajui mambo ya siri,,,anaejua mambo ya siri ni m/mungu peke yake.
Ila kilichosababisha mfalme afe ni huzuni juu ya maneno aliyoambiwa ikapelekea mpk akawa hali chakula hivyo akafa kwa njaa........
............................. ................................
Chakujifunza ktk hadithi hii ni kuwa mawazo mabaya juu yako uyafikiriayo mpk ukawa na huzuni yatakuathiri kidogo kidogo
Na hatimae unaweza ukafa kwa kuwaza pmj na kuhuzunika,,,
Hivyo usimsikilize kila mtu kwa analokuambia mtegemee m/mungu pekee angalia ni nani anaekushauri juu ya maisha yako.
Home > Hadithi > Hadidhi tamu usikayishwe tamaa
Hadidhi tamu usikayishwe tamaa
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • December 03, 2019 • Hadithi • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment