Jifunze kujua wakati wa kuachana na wengine unapofika,sio kila mtu utadumu naye kwa Muda wote:
.
1)Kuna watu wataanza na wewe wanakusaidia kufika mahali fulani Kisha wanaondoka kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wengine.Wape Fursa ya kuwasaidia wengine pia,usiwe mbinafsi kuwang’ang’ania.
.
2)Kuna watu walikuja ili uwasaidie,wakishaimarika wanaendelea na Safari,na wewe endelea na Safari.Usinung’unike kuwa hawako na wewe tena,Furahia mafanikio yao.Mungu alikutumia kuwasogeza hatua,usitake kuwamiliki.
.
3)Kuna watu walikuja kukufundisha Kitu fulani,ukishapata somo,wanaondoka.Inaweza kuwa kupitia maumivu ama furaha,ila somo utalipata.Wanakusaidia kukuongezea umakini katika maisha.
.
4)Kuna wengine walikuja ili wakuunganishe na watu wengine,wakishamaliza wanaondoka.Wanaweza wasikupe Kitu ila wakakuunganisha na Mtu/Fursa itakayokufanikisha.
.
5)Kuna wengine walikuja kukuharibia mwelekeo,wakishakutoa kwenye mstari,wanaondoka.Furaha yao na ushindi wao ni kuona umepoteza mwelekeo.
.
6)Kuna watu wamekuja kwa sababu kuna msimu mpya wa maisha yako,msimu huo ukishapita na wao wanakuwa wamemaliza kazi.Ni marafiki wa msimu.
.
7)Kuna watu walikuja kwa sababu kuna Kitu walitarajia kupata kutoka kwako,wakishakipata tu,wanaondoka.Hawana cha kukupa hawa,usijaribu kutarajia kutoka kwao.
.
Je,umewahi kukutana na namba ngapi?
.
See You At The Top
#TIMIZAMALENGOYAKO
EV.MCHOME
0672870833
✝️🔯
Home > Wasaka mafanikio > Jifunze kujua wakati wa kuachana na wengine
Jifunze kujua wakati wa kuachana na wengine
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • December 23, 2019 • Wasaka mafanikio • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment