Headlines

TABIA ZA MTU MWENYE KIBURI

TABIA 10 ZA MTU MWENYE KIBURI

Kiburi ni kutokutii pia ni kuwa na ujeuri na ukaidi. 1 Petro 5:5 inasema ''...MUNGU huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.''
TABIA 10 ZA MTU MWENYE KIBURI NI;
1:Hupenda kujulikana na hapendi wengine wajulikane

2;Anapenda kusikilizwa ila yeye hapendi kusikiliza wengine. Kutoka 5:2 ''Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.'' hii ni roho ya kiburi na huyu farao alishushwa. pia Mithali 12:15 inasema ''
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.

3;Hapendi kushauriwa na wengine ila yeye anapenda kushauri wengine. Mithali 29:1-2-Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.

4;Hapendi kukosolewa ila yeye anapenda kukosoa kwa kila jambo. Mithali 13:10-
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

5;Anapenda kutiwa moyo lakini yeye hawezi kuwatia moyo wengine.Mtu kama huyu akiugua anapenda wana kanisa wakamtembelee na kumpelekea zawadi lakini yeye hajawahi kumtembelea mgonjwa hata mmoja. hii ni roho ya kiburi

6;Anapenda kulaumu wengine ila yeye hapendi kulaumiwa

7;Hupenda kudharau wengine lakini yeye hapendi kudharauliwa. Wakolosai 3:13-14-mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Pia Mithali 14:21 inasema ''Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.''

8;Hudai heshima kwa nguvu lakini yeye hataki kuheshimu wengine.Mithali 3:34-35- Hakika yake (MUNGU)huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha. Na pia Mithali29:23 inasema
Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Na pia Mithali 14:15 nayo inasema ''
Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.

9;Hupenda kumiliki mali isiyo yake. Ndugu hata fungu la kumi ni la MUNGU hivyo kuacha kutoa zaka ni kumwibia MUNGU na hiyo ni roho ya kiburi.Malaki 3:8-9 inasema ''Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.''

10;Hufurahi kuwaonea wengine na kuwasimanga lakini yeye hataki kuonewa wala kusimangwa. Obadia 1:12-Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao. Ndugu hata shetani aliangushwa kwa sababu ya kiburi maana alisema nitafanana na MUNGU . na kwa sababu ya kiburi chake alishushwa. isaya 14:14-15Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo..
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
William Mchome

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes