ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAENEO MAKUU(MAANGA) MATATU.
I. ANGA LA KWANZA(FIRST SPHERE) - MALAIKA WALIOPO KATIKA ANGA LA KWANZA NI WALE WANAOTUMIKA KAMA WAJUMBE WA HALMASHAURI YA MBINGUNI - (THE HEAVENLY COUNSELORS.)
1) MASERAFI(SERAPHIM, WAWAKAO MOTO, WAUNGUZAO)
Hawa ni malaika wa ngazi ya juu sana. Hukizunguka kiti cha enzi. Ni waangalizi/watumishi wa kiti cha enzi cha Mungu, ni daraja la juu sana la malaika. Wanamsifu Mungu kwa kupaza sauti bila kukoma wakisema: "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA Mungu wa majeshi, mbingu na nchi zimejaa utukufu wako!"
Kulingana na "Isaya 6:1 Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona BWANA AMEKETI KATIKA KITI CHA ENZI, KILICHO JUU SANA NA KUINULIWA SANA, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. 2 JUU YAKE WALISIMAMA MASERAFI; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. 3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. 4 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi. 5 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi. 6 Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu; 7 akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa. 8 Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi."
Maserafi ni viumbe wenye mabawa sita, kwa mawili hufunika nyuso zao na kwa mawili huifunika miguu yao, na kwa mengine mawili huyatumia kwa kuruka. Ni viumbe wenye moto.
2) MAKERUBI(CHERUBIM)
Makerubi ni cheo cha chini ya Maserafi, na cheo cha pili kati ya vyeo tisa au kwaya tisa za malaika. Ni viumbe hai wane Ni viumbe hai wane, Ezekieli 1:5; "Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu". Kiti cha enzi cha Mungu kipo juu ya Makerubi, Ezekieli 10:1; "Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi." Merubi ni viumbe wenye sura nne: ya binadamu, ng'ombe, simba, na tai. Wana mabawa manne yaliyoungana yaliyojawa na macho, mwili kama wa umbile la simba, na wana miguu kama ya ng'ombe. Wanailinda njia inayoelekea kwenye mti wa uzima ulio katika bustani ya edeni. (Mwanzo 3:24) na kiti cha enzi cha Mungu(Ezekieli 28:14-16). Ni viumbe wenye moto, wana magurudumu yaliyojaa moto Ezekieli 10:2; Wanatembe juu ya mawe yenye moto, Ezekieli 28:14. Ni waimbaji na wapiga vyombo vya kwaya ya mbinguni, Ezekieli 28:13. Mabawa yao yanatoa sauti kama sauti ya Mungu Mwenyezi(unabii?)-Ezekieli 10:5; Shetani ni kerubi aliyenguka Ezekieli 28:13-19. Wametajwa katika Mwanzo 3:24; Kutoka 25:17-22; 2 Nyakati 3:7-14; Ezekieli 10:12-14, 28:14-16; 1 Wafalme 6:23-28; na Ufunuo 4:6-8. Makerubi ni alama ya nguvu za Mungu na kutembea kwa Nguvu za Mungu. Katika Agano Jipya, wanaitwa ni viumbe wa mbinguni, katika kitabu cha Ufunuo sura ya 4-6. Ni malaika wenye uelewa wa ndani sana kuhusu Mungu, na hivyo ni wanaomsifu sana Mungu daima. (Kerubi ni kiti cha Mungu? Ni wenye kujazwa sana na Roho Mtakatifu-Ezekieli 28:14 "Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.")
3) WAZEE WAANGALIZI(WAHUDUMU WA SIFA) WA MBELE YA KITI CHA ENZI(THRONES OR OPHANIM)]
Kiti cha enzi(Kiyunani: thronoi, wingi wa thronos) au Wazee, pia hujulikana kama Erelim au Ophanim, ni daraja la viumbe vya mbinguni vilivyotajwa na mtume Paulo katika Wakolosai 1:16 "16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.". Ni alama hai ya mamlaka na haki ya Mungu, na wana kuwa kama moja ya alama ya kiti cha enzi.
Ophanim (Kiebrania ofanim: ni magurudumu; ofanim pia hufahamika kama viti vya enzi, tunaona hivyo kutoka katika maono ya Danieli 7:9 "Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao"). Wana muonekano usio wa kawaida ikilinganishwa na viumbe wengine wa mbinguni; wanaonekana kama gurudumu lenye rangi ya zabarajadi(kioo angavu) ndani ya gurudumu, sehemu ya ukingo wa nje ya magurudumu hayo imejaa macho. Wanahusiana sana na makerubi: Ezekieli 10:17 "Waliposimama hao, hayo nayo yalisimama; na walipopaa juu hao, hayo nayo yalipaa juu pamoja nao; maana roho ya huyo kiumbe hai ilikuwa ndani yao. Ni malaika wenye unyenyekevu safi, amani, na utii. Wanakaa katika eneo la ulimwenguni mahali vitu vya kimwili vinapoanza kufanyika katika maumbile. (They reside in the area of the cosmos where material form begins to take shape). Malaika wa ngazi ya chini wanawahitaji malaika hawa kuwasaidia ili waweze kumkaribia Mungu.
II. ANGA LA PILI(SECOND SPHERE) - MALAIKA WANAOFANYA KAZI KAMA MAGAVANA/BARAZA LA VIONGOZI WA MBINGUNI (HEAVENLY GOVERNORS).
4) MASULTANI AU MABWANA(DOMINIONS OR LORDSHIPS)
"Usultani" (Efe. 1:21; Kol. 1:16) (Kilatini ni dominatio, wingi ni dominationes; Kigiriki neno kyriot?tes, wingi wa kyriot?s, kama "Ubwana" au "Usultani" - maneno haya yanawasilishwa kama cheo cha viumbe wa mbinguni). Usultani pia huitwa "Hashmallim", ni kazi ya kurekebisha kazi za malaika wa ngazi ya chini. Ni mara chache sana hawa malaika wa ngazi ya usultani hujidhihirisha kimwili kufahamika na wanadamu. Ni malaika ambao pia wanatawala juu ya maeneo ya anga au mataifa au nchi. Wanatofautishwa na malaika wengine kwa kuonekana kwao, kwani wanaonekana katika maumbile ya wanadamu wenye mabawa mawili na wenye miili mizuri ya kupendeza, wana fimbo za mamlaka, na wana duara ya mwangaza kuzunguka vichwa vya fimbo zao za mamlaka au mipini ya panga zao. Hawa ni malaika wa uongozi, wanarekebisha au kupanga zamu za malaika, kwa kuwaelewesha amri za Mungu.
5) MAJESHI YA ANGA AU NGOME (VIRTUES OR STRONGHOLDS)
Wanaitwa pia "waangazao." Wanaongoza mambo yote ya asili. Kazi yao ya msingi ni kusimamia na kuangalia mienendo ya viumbe vya angani; yaani, majira, sayari, nyota, jua, mwezi, vimondo, … ili kuhakikisha kuwa dunia inakuwa katika utaratibu na mpangilio unaotakiwa. Ni wenye kuongoza miujiza na kuleta ujasiri, neema na kutia moyo ili kuleta uhodari kwa mwamini. Waefeso 1:21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;.
6) WENYE MAMLAKA MAMLAKA NA NGUVU(POWERS OR AUTHORITIES OR POTENTATES)
(" Nguvu, Powers" Kilatini potestas , wingi potestates, au "Mamlaka, Authorities", kutoka Kiyunani exousiai, wingi wa exousia, kwa mfano katika Waefeso 3:10), huonekana kusaidiana, katika nguvu na mamlaka, pamoja na wakuu, watawala. Ni malaika wanaobeba dhamiri na kutunza kumbukumbu ya historia. Ni malaika mashujaa walio kamili katika uaminifu wao kwa Mungu, wengine wanaamini kuwa kati ya daraja hili hakuna malaika aliyeanguka katika uasi na shetani, ukilinganisha na madaraja mengine; lakini wengine wanasema shetani kabla ya kuasi alikuwa katika daraja hili. (Waefeso 6:12). Wajibu wao ni kuangalia mgawanyo wa nguvu kati ya wanadamu, na ndivyo lilivyo jina lao. Katika Waefeso 1:21, mtume Paulo anatumia neno "utawala" "mamlaka" na neno "watawala" na "wenye mamlaka" katika Waefeso 3:10. Alimaanisha pia watawala na mamlaka ya wanadamu badala ya malaika.
III. ANGA LA TATU(THIRD SPHERE) - MALAIKA WANAOFANYA KAZI KAMA WAJUMBE AU ASKARI KUTOKA MBINGUNI(MESSENGERS OR SOLDIERS).
7) WAFALME AU WATAWALA (PRINCIPALITIES OR RULERS).
"Wenye mamlaka" kwa kilatini ni principatus, wingi principat?s pia hutafsiriwa kama "Ufalme, Princedoms" na "Watawala, Rulers", kutoka neno la kiyunani archai, wingi wa arch? (Efe 3:10), likiwa na neno katika nguvu na mamaka, pamoja na nguvu(mamlaka). Malaika hawa wanaonekana wakiwa wamevaa taji na wameshika fimbo ya kifalme. Wajibu wao ni kutimiza amri zilizotolewa na masultani na kuleta baraka katika ulimwengu wa kimwili. Kazi yao ni kuangalia makundi ya watu. Ni waelimishaji na walinzi wa muhimili wa dunia. Kama viumbe wanaohusiana na ulimwengu wa chanzo au mbegu ya mawazo, wanahusika na kuvuvia viumbe hai kwa mambo mengi kama vile sanaa au sayansi. Mtume Paulo alitumia neno "utawala" na "mamlaka" katika waefeso 1:21 na "watawala" na "wenye mamlaka" katika Waefeso 3:10. Katika Agano Jipya, wafalme wananukuliwa kuwa ni mojawapo ya aina ya viumbe vya kiroho ambavyo sasa ni maadui kwa Mungu na wanadamu. (Rum 8:38; 1 Kor 15:24; Efe 1:21; 3:10; 6:12; Kol 1:16; 2:10, 15) Wakiwa pamoja na wenye mamlaka, ni:
a. Nguvu, Powers (Rum 8:38; 1 Kor 15:24; Efe 1:21; 1 Pet 3:22; 2 Thes 1:7); na Nguvu za anga au wakuu wa anga (cosmological powers) (1 Kor 15:24; Efe 1:21; 3:10; Kol 2:15);
b. Masultani, Dominions (Efe 1:21; Col 1:16) and Enzi (Col1:16). Uelewa wa ushuhuda kutoka katika Agano Jipya unatusaidia kutambua ya kuwa viumbe hawa waliumbwa kupitia Kristo Yesu, na kwa ajili yake waliumbwa. (Kol 1:16). Kupewa kwao uadui kwa Mungu na kwa wanadamu kwa sababu ya dhambi, utawala wa ubora wa hali ya juu sana kwa viumbe hawa, inaonyesha ukuu wa utawala wake BWANA juu ya anga zote. Huu ni Ubwana wa Kristo, unaodhihirisha Wokovu wa ajabu kuu sana wa Mungu katika kuishinda dhambi na mauti pale msalabani, na sasa wokovu huo unachukua nafasi katika Kanisa. (Waefeso 3:10)
8 ) MALAIKA WAKUU (ARCHANGELS)
Neno "malaika mkuu" linatokana na neno la Kiyunani archangelos, lenye maana ya mkuu wa malaika(chief angel), kwa tafsiri ya Krania rav-mal'ákh, linatokana na neno la Kiyunani archein, linalomaanisha kuwa wa kwanza katika cheo au nguvu(to be first in rank or power); na neno angelos linalokaanisha mjumbe(messenger), au muwakilishi wa balozi (envoy). Neno hili limetumika mara mbili tu katika Agano Jipya katika 1Wathesalonke 4:16 na katika Yuda 1:9. Ni malaika Waku Gabrieli na Mikaeli tu ambao wametajwa kwa majina katika Agano Jipya. Katika desturi nyingi za kikristo, malaika Gabrieli anatambuliwa kuwa ni malaika mkuu, lakini hakuna maandiko ya moja kwa moja yanayoonyesha jambo hili. Ni vema kutambua ya kwamba, neno "malaika mkuu" linaonekana kutumika tu kwa umoja, na si katika wingi, na pia hutumika tu kumtaja malaika Mikaeli kuwa ndiye Malaika Mkuu. Imani za wakristo wengine humchukulia Mikaeli tu kuwa ndiye malaika mkuu. Jina Malaika Mkuu Rafaeli linaonekana katika kitabu cha Tobiti (Tobias). Tobiti ni kitabu kinachotambulika kama kitabu cha mapokeo (Deuterocanonical) kwa Wakatoliki wa Roma), Wakristo wa Ki-Orthodox wa mashariki, na Waanglikana. Kiatabu cha Tobiti pia husomwa na Waluteri, lakini sio na Waprotestanti wa madhebu mengi, Wakristo wa madhebebu ya matengenezo ikiwemo na Wabaptisti. Rafaeli analezwa katika kitabu cha Tobiti(Tobias) kuwa ni mmojawapo wa malaika saba wasimamao mbele za BWANA", na inaaminika kuwa Mikaeli na Gabrieli ni wawili kati ya wengine. Malaika Mkuu wanne ni Urieli, ambaye jina lake linamaanisha "Nuru ya Mungu, Light of God." Jina la Urieli ndilo pekee linalotajwa katika Biblia ya Kiluteri, Anglikana na Wakristo wa Ki-Orthodox wa Urusi. Tafsiri nyingine ya malaika Wakuu saba ni kuwa wao ni Roho Saba za Mungu zinazosimama mbele za Mungu, na zilizotajwa katika kitabu cha Ufunuo 1:4; 3:1; 4:5; 5:6; Malaika Wakuu Saba wanasemekana ni walinzi wa mataifa nan chi, na wanahusika na masuala na matukio yanayozizunguka, ikiwa ni pamoja na siasa, masuala ya kijeshi, na biashara na uchumi. (Yoshua 5:13-15) Kwa makundi mengine ya wakristo, huamini ya kuwa Malaika Mkuu Mikaeli, ni jina jingine la BWANA Yesu Kristo; mfano, Wasabato na Mashahidi wa Yehova.
9) MALAIKA WATUMISHI WATUMIKAO(ANGELS).
The "Malaika, angels" au malakhim, yaani, "malaika wa kawaida "plain" angels"(angeloi, wingi wa angelos, i.e. mjumbe (messenger) au wakili wa balozi, ubalozi (envoy), ni daraja la chini sana la malaika, na ndilo linalofahamika sana kwa watu wengi. Wanahusiana sana na mambo ya viumbe hai. Katika aina hii ya malaika, wapo wa namna nyingi tofauti tofauti, wakiwa na kazi mbali mbali. Hutumwa kama wajumbe kwa wanadamu. Malaika hawa ni wa karibu sana kwa ulimwengu wa vitu na wanadamu. Wana peleka maombi kwa Mungu na Majibu ya Mungu na ujumbe mwingine toka kwa Mungu kwa wanadamu. Malaika wanao uwezo wa kuwakaribia malaika wengine wa ngazi yoyote ile na kwa wakati wotote ule. Ni wanaojishughulisha sana na jamii kuwasaidia wale wanaoomba msaada katika mazingira magumu ya kimwili; mfano, katika ajali, vizuizi au vikwazo vya kutoka mahali kwenda mahali pengine(gerezani), …. .
Post a Comment