Headlines

Jifunze kutoka kwa tai mambo 7

MISINGI SABA YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA NDEGE TAI....*

_*bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. (Isaya 40:31)*_

1. *Tai hupaa juu sana angani akiwa peke yake*
Hawaruki pamoja na mbayuwayu, kunguru, wala na ndege wengine wadogo.

_*Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana. (Obadia 1:4)*_

*MAANA;*; Kaa mbali na watu wenye mawazo mafupi, wale wanao kuangusha. Tai huruka na tai wenzake. Ambatana na wale wenye tabia njema.

_*Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? (2 Wakorintho 6:14)*_

_*Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?(Amosi 3:3)*_

*2. Tai wana macho yanayoona vizuri na kwa usahihi sana.* Wanao uwezo wa kukiona kitu umbali kufikia kilomita hata tano.  Haijalishi kipo kikwazo gani, tai haondoi macho yake chini kwenye shabaha mawindo yake.

_*Katika habari za kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana. (Yeremia 49:16)*_

*MAANA;* Uwe na maono na ubakie katika maono hayo, haijalishi unakumbana na vikwazo gani,  5 utafanikiwa.

*3. Tai hawali vitu vilivyokufa. Wanakula mawindo mabichi.*

*MAANA;*  Usiyategemee mafanikio yako yaliyopita, bali uendelee kuyatafuta mapambano mapya ya kuyashinda.

_*Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele (Wafilipi 3:13)*_

4. *Tai hupenda dhoruba.*
Wakati mawingu yanapokusanyika, tai husisimka, tai huutumia upepo wa dhoruba kujinyanyua kwa upepo huo ili kupaa juu sana kupita mawingu.  Hii humpa tai huyo nafasi ya kutanua mbawa zake kujieneza na kupumzika akiwa hewani. Wakati huo wa dhoruba ndege wengine wote hujificha matawi na majani ya miti.

_*Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake. (Yeremia 49:22)*_

*MAANA;* Pambana na changamoto kwa kifua mbele, ukijua ya kuwa changamoto hizo zitatumika kukuimarisha na kukufanya uibukie ukiwa bora zaidi ya ulivyokuwa awali. Twaweza kuitumia nafasi ya dhoruba katika maisha yetu ili kuibuka kileleni juu. Wanaotaka kufanikiwa hawaogopi kuibuka juu. Wanaofanikiwa hawaogopi changamoto, bali wanazifurahia na kuzitumia kwa faida.

*5. Tai hujiandaa kwa mafunzo;*
Huyaondoa manyoya na nyasi laini katika kiota ili vifaranga vyake visijisikie vizuri, kwa maandalizi ya kuwafanya waanze kuruka, na hatimaye waruke pale watakapo ona mazingira si rafiki tena kukaa katika kiota hicho.

_*Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu. (1 Petro 5:10)*_

*MAANA;* Ondoka eneo la kujifariji na kuridhika, kwani hapo hakuna kukua.

  _*Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. (1 Wakorintho 9:24-27)*_

*6. Kipindi tai anapozeeka;*
Manyoya yake huwa dhaifu na hayawezi kumsaidia tena kwa haraka wepesi na juu sana kama inavyotakiwa.
Hii humfanya kuwa dhaifu na hata kumfanya afe, hivyo huenda shehemu mbali katika milima, na kukaa juu ya jiwe juani, tangu asubuhi hadi jioni; chakula chake si bora cha mawindo kama mwanzo, bali anakula wadudu na mijusi; huku akijinyonyoa manyoya yake ambayo sasa yalikuwa dhaifu na kujikata mdomo wake na kucha zake kutoka mwilini mwake pale kwenye jiwe /mwamba;  hadi anabakia kuwa mtupu na mwenye upaa mwili wote; hiyo ni kazi ngumu inavyouma na inapelekea kutokwa damu.
Kisha, hukaa mafichoni, pangoni, hadi pale atakapo ota manyoya mapya, mdomo mpya na kucha mpya, na ndipo hutoka tena nje  na kuruka akipaa juu sana zaidi ya mwanzo.

_*Katika habari za kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana. (Yeremia 49:16)*_

_*Jifanyie upaa, jikate nywele zako, Kwa ajili ya watoto waliokufurahisha; Panua upaa wako kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nawe utumwani.(Mika 1:16)*_

*MAANA;* Mara nyingine unahitaji kuuvua utu wako wa kale(mazoea ya mwanzo), haijalishi ni vigumu jinsi gani mambo yanavyokulemea, au livyo, yasivyo na thamani katika maisha yako, lazima uyaachilie kuondoka!

*7. Tai hufanikiwa kuruka juu sana karibu maili 10 angani, lakini hubakia akiwa makini kuangalia vitu vidogo, naam, hata sindano, vilivyo chini ardhini !*

_*Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa. (Isaya 51:1)*_

*MAANA:*
Ukifanikiwa kuyafikia mafanikio ya juu, kumbuka kule chini ulikotokea, usividharau vitu vidogo vidogo, wala usije ukawasahau na wengine waliotumiwa na Mungu kukufanya ufanikiwe.

*KAMWE USIJE KATA TAMAA*

*NA UWE KAMA TAI*

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes