Add caption |
1. WENYE HAJA YA KUMJUA MUNGU NA KUMTUMIKIA: Hawa ni washirika wa kweli na ambao hawayumbishwi na chochote. Hawa ndio wanafaa kuwa Viongozi katika kanisa.
2. WATAFUTA MISAADA/FURSA: Hawa ni wale waliomfuata YESU ili wapate mikate ya bure. Kundi hili limejaa WALALAMISHI ambao mara zote wanataka kanisa liwaangalie wao na mahitaji yao basi. Wengine wanakuja ili kupata wenzi wa maisha tu au msaada fulani.
3. WATAFUTA VYEO NA KUTAMBULIWA: Hawa wakifika mahali wanataka kila kitu kisimame kwa ajili yao. Wao wanataka kuongoza kila kitu hata wasicho-kijua. Wakichelewa kutambuliwa huwa wanatafuta pengine watakapotambuliwa. Mara nyingi huwa ni “WAKOSOAJI SANA”; wanapenda kusema “kule tulikua hatufanyi hivi na vile...!!”
4. WAKIMBIZI NA WALIOUMIZWA: Hawa ni wale walioumizwa na Viongozi wao na kuamua kutafuta mahali pa kuabudu na kumtumikia Mungu kwa uhuru. Wengine huwa wamekimbia adhabu waliyopewa huko walipotoka. Kundi hili likisaidiwa kwa karibu, huwa lina watu wenye POTENTIALS na KARAMA kubwa ambazo Shetani anajaribu kuziangamiza.
5. WALIODUMAA: Hili ni kundi la watu ambao wamedumaa kiroho. Hawajishughulishi na chochote cha kuwaleta watu kwa YESU. Wao ni kuja ibadani kutimiza tu taratibu za kidini.
NB: MAKUNDI HAYA YOTE HUWA YANA MCHANGO FULANI KATIKA KAZI YA MUNGU. WENGINE WANAWEZA KUKAA KANISANI KWA MUDA MCHACHE TU NA WAKALETA CHACHU KUBWA YA MAANDELEO NA HUDUMA HALAFU WANAONDOKA.
NI WAJIBU WA KIONGOZI KUJUA NANI YUPO KUNDI GANI NA KUWEZA KUNASA POTENTIALS NA KUZITUMIA KIMKAKATI.
🔥 MUNGU ATUSAIDIE TUWE WANAFUNZI HALISI WA YESU KRISTO🔥 .
By
EV.MCHOME
0672870833
Post a Comment