Home > Vijana > Vijana na uasherati/uzinzi
Vijana na uasherati/uzinzi
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 05, 2019 • Vijana • Comments : 0
1. MARAFIKI WABAYA.
🔹Ukiwa na rafiki mzinzi tegemea kuwa mzinzi, Ukiwa na rafiki mcha Mungu atakuambukiza hofu ya Mungu.
"Chuma hunoa Chuma, Ndivyo mtu Aunoavyo uso wa rafiki yake "
Mithali 27 :17
2. CHATTING ZA NGONO.
🔹Vijana wengi wa sasa huchat mambo yahusuyo Ngono kila siku, maongezi haya hupelekea wengi kuanguka kwenye uzinzi.
🔹Inbox ya Vijana wa sasa, zimekuwa kama 'Scprit za picha za ngono'.
" Msidanganyike, Mazunguzo MABAYA huharibu TABIA NJEMA "
1 Wakorintho 15 :33
3. MIZAHA
🔹Mazoea mabaya yanaambatana na tabia ya kushikana-shikana mwili hupelekea pia kwenye uzinzi kamili.
" Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio HAKI, Wala hakusimama Katika njia ya wakosaji, Wala hakuketi BARAZANI PA WENYE MIZAHA. "
Zaburi 1 :1
4. UTANDAWAZI.
🔹kuongezeka kwa kasi ya utandawazi kumeongeza kasi ya ngono kwa Vijana. Watu hutongozana kupitia mitandao ya kijamii Facebook, Instagram, Watsap groups, nk wanapanga kuonana na mwisho kufanya uzinzi.
🔹Uvaaji mbovu kwa wadada pia unachangia kiasi kikubwa Katika hili, utakuta binti kavaa kinguo kimembana tena kina mpasuo halafu katuma picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, unategemea nini kitatokea kama watu si kumfuata inbox kuomba huduma kupitia matangazo waliyoona?
🔹 Hata baadhi ya wana wa Mungu nao wapo Katika kundi hili, ingawa wanajifanya wema ukiwatazama usoni, Lakini looh..! NI SHIDA.
"Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia hii ni kuwa ADUI wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa ADUI wa Mungu "
Yakobo 4 :4
5. UANGALIAJI WA PORN (PICHA ZA NGONO).
🔹Hili nalo ni tatizo kwa Vijana wa sasa, hizi smartphone zimekuwa mjumbe mkubwa wa Vijana kuwapeleka kuzimu.
🔹Kama Vijana wasipoangalia wataelekea kuzimu wengi sana kwa mapicha ya ngono waliyojaza kwenye simu zao.
"UNIGEUZE MACHO YANGU, NISITAZAME VISIVYOFAA. Unihuishe Katika Njia yako "
Zaburi 119 :37
6. KUUZOELEA WOKOVU
🔹Kwa Vijana waliokoka nao wanaanza kuuchanganya WOKOVU wao na kuona si KITU, wanajirahisisha Katika dhambi bila kujali nafasi zao mbele ya Mungu.
🔹Unakuta Vijana wapo kwenye uhusiano tu wa awali wakiwa na malengo ya kufunga ndoa, tayari wameshaanza kuonjana bila hata Aibu na bado wanajiita WATEULE, mmmh, Aisee..! Kwa mtindo huu wa kuonjana bila UTARATIBU, labda watakuwa WATEULE WA KUZIMU .
🔹Mungu hajawahi kuwa na Ushirika, hana Ushirika na hatakuwa na Ushirika na DHAMBI. Kijana kumbuka hili. 👇
" Au1 HAMJUI YA KUWA WADHALIMU HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU? Msidanganyike WAASHERATI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU, WALA WAABUDU SANAMU, WALA WAZINZI, WALA WAFIRAJI, WALA WALAWITI "
1 WAKORINTHO 6 :9
7. KUKOSA NGUVU YA MUNGU.
🔹Vijana wengi wa sasa wanapenda sana kuchat, kuangalia movie kuliko kupenda kujifunza Neno la Mungu. Hawana muda wa faragha wa kuomba na kumtafuta Mungu hali hii hupelekea kujikuta kwenye TAMAA za mara kwa mara ya Uzinzi.
"Kwa maana Sijui Nilifanyalo, Kwa sababu lile NILIPENDALO (kuishi maisha matakatifu) silitendi, Bali lile NILICHUKIALO (kufanya uzinzi) ndilo Ninalolitenda "
Warumi 7 : 15
🔹Biblia inasema" Kesheni MKIOMBA msije mkaingia majaribuni (Mathayo 26 :41) " sio" KESHENI MKICHAT "hivyo kama ukiwa unakesha Ukichat Uzinzi lazima uwe Pacha wako.
8. KUTOKUJIHUSISHA NA KAZI YA MUNGU.
🔹Yesu alituokoa ili tuweze kumzalia MATUNDA (tuokoe wengine).. Yohana 15 :16
🔹Lakini Vijana wa sasa hawawezi hata kumshuhudia mtu habari za Yesu? Kama hata kujitambulisha tu kazin, chuoni au Nyumbani.
🔹Usipokuwa Busy na YESU hautakosa kuwa Busy na mambo ya Shetani.
"An idle mind is the workshop of the Devil "
9. VITA YA KIROHO.
🔹Vijana ndio Nguvu Kazi ya kanisa la sasa, hivyo kama Vijana ni mapooza basi hata kanisa pia litakuwa pooza (vuguvugu).
🔹Hivyo IBILISI huwapiga vita sana Vijana hasa kwenye uzinzi ili aharibu kanisa. 👇
" Mwe na kiasi na Kukesha, kwa kuwa Mshitaki Wenu Ibilisi kama Simba Angurumaye HUZUNGUKA - ZUNGUKA AKITAFUTA MTU AMMEZE (Amwangushe kwenye dhambi). "
1 PETRO 5 :8
10. KUKOSEKANA MAFUNDISHO KWA VIJANA.
🔹Kuna UMUHIMU wa Vijana kupewa Elimu ya kimahusiano kuanzia nyumbani kwenye familia zao, mashuleni /vyuoni na Katika makanisa Wanayoabudu.
🔹Elimu hii itolewe mara tu kijana anapoonekana Amepevuka pia iambatane na huduma za ushauri na maombezi.
🔹Najua haya yanafanyika hata sasa ila kasi ya upotoshwaji kwa Vijana kupitia Ibilisi na mawakala zake kupitia picha za ngono, mitandao ya kijamii, smartphone nk ni kubwa kuliko Elimu Inayotolewa.
...............
👉 "JINSI GANI KIJANA AISAFISHE NJIA (MAISHA) YAKE ❓KWA KUTII, AKILIFUATA NENO LA MUNGU.
'♥ MOYONI MWANGU NIMELIWEKA NENO LAKO, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI"
ZABURI 119 :9, 11
BWANA ATUSAIDIE VIIJANA TUNAOSOMA UJUMBE HUU..!
By
EV.MCHOME
0672870833
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment