Headlines

Kuketi na wakuu


UNATAKA KUKETI NA WAKUU??

Una omba MUNGU akuketishe na wakuu, umejiandaa kukaa na hao wakuu?? Wakuu ni akina nani?? Sifa za watu wakuu ni zipi?? Kwanini unataka kukaa na watu wakuu??

Tena hapa mtu ana omba na kunukuu Zaburi 113:7-8 vizuri kabisa, utamsikia anasema imeandikwa:

"Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani. Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake".

Ngoja tuitafute maana ya "WAKUU", wakuu wanaweza kuwa viongozi, watu wanao miliki na kutawala, watu wenye nafasi kubwa ya kiuchumi na ushawishi kwenye jamii fulani.

Ukisoma kitabu cha Kutoka 18:25, neno la MUNGU linasema:

"Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi". (Maana ndogo tu ya watu wakuu ina anzia hapa).

TATIZO SIYO KUKETI NA WAKUU, ILA UNAFANYA NINI UKIWA NA HAO WAKUU??

Kwanza kabisa kuna vitu lazima uvifahamu kuhusu wewe mwenyewe kabla ya hao wakuu. Wewe ni nani?? Ni mtu wa tabia zipi?? Uko wapi na unataka kwenda wapi?? Kihuduma, kiuchumi au kiuongozi upo daraja lipi na unahitaji watu wa aina ipi kukuvusha hapo ulipo. Baada ya maswali hayo, sasa endelea na haya:

1. Una ongea nini?? Unawasema wengine vipi?? Kuna tabia zinamfanya MUNGU asikupe kibali cha kuketi na hao wakuu. Kwa mfano: tabia za kinafiki, kuketi na wakuu ili uwaseme wengine vibaya. Kutumia nafasi yako vibaya kwa hao wakuu. Muulize Hamani kilimkuta nini kwa Esta. Soma biblia yako vizuri kwenye kitabu cha Esta.

2. Hao wakuu wanapo ongea na wewe, una jibu nini?? Unakuta mtu ana maelezo marefu kama gazeti la udaku!! maneno mengi ya nini?? Watu wakuu wanapenda kusikiliza "hoja" na "agenda" za msingi siyo maneno mengi. Wana penda points na maelezo mafupi yanayo eleweka. Siyo swali moja alafu una jibu kwa kusimulia hadithi, utakwama!! Kuwa mtu wa points na agenda.

3. Una hitaji kusaidiwa nini?? Mwingine anapenda kuketi na wakuu kama "fashion" hajui ana hitaji nini hasa kutoka kwa hao wakuu. Hao wakuu unataka wakusaidie nini?? Omba msaada ambao utakufanya usiwe omba omba tena. Simaanishi uombe fungu la fedha, hata msaada wa mawazo na "connection" inatosha kukuinua.

4. Sasa ukiketi nao hao wakuu wasiwe miungu kwako. Usiwafanye wao kuwa ndiyo tumaini lako la mwisho, utamkosea MUNGU. Zaburi 118:9, neno la MUNGU linasema:

"Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu" na Yeremia 17:5 inasema: "BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,
Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA".

5. Wengine hukaa na wakuu kama wasaliti. Marko 14:10 ina sema:

"Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao". Kuna watu wana hitaji kuketi na wakuu ili kuhukumu na kusaliti wengine.

MWISHO: Hapa nimetoa tu mwanga, watu wakuu ni nani na jinsi gani ya kukaa nao au kuhitaji msaada kwao. Naamini nimesema na roho ya mtu ili ipone. Nimesema kwa kiasi, yapo mengi lakini nimejitahidi sana kufundisha kwa ufupi. Fanyia kazi ulicho jifunza mahali hapa.

NB: Ukielewa na ukimaliza kufanyia kazi ulicho jifunza, sema "sitakuwa nilivyo kuwa, Roho wa MUNGU ana nibadilisha".

EV.MCHOME
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes