Headlines

Hatua za imani


HATUA TATU ZA IMANI
1. Usitulie wakati umechoka, ila tulia ukiwa umemaliza.
Hii inamaanisha shikilia ahadi za Mungu (hiki ni kiwango cha tumaini).
2. Usitazame saa, bali fanya kile saa inafanya.
Hii inamaanisha usilitazame jua, bali fanya kile linafanya. Maana jua likichwa halibaki pale pale bali linaenda kunako kutua na litarejea kesho. Hivyo usiiangalie tu siku ikipita bali fanya kitu.

UWE NA MWENDO

3. Fanya kile unapaswa kufanya pasipo hofu, uwe hodari na mwenye ushujaa. Vitisho vipo tu hivyo usivitizame bali uwe hodari.

Kwasababu Mungu hawezi kwenda na wewe kama sio hodari na mwenye ushujaa, maana Mungu hawezi kwenda na mtu ambaye anaweza kuishia njiani maana Mungu hawezi kuzimia.

Washindi hawaogopi yoyote na hawataki kumuua yoyote bali wanataka wasaidie watu na waone wengine wakishinda.

ENDELEA KUSONGA MBELE NA USIANGALIE MAZINGIRA YANASEMA AU KUFANYA NINI, KAZANA KWENDA

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes