Headlines

Thamani ya muda

THAMANI YA MUDA
Kla kitu kinahitaji muda
Uwepo wako duniani ni matokeo muda uliotengwa na Baba na mama yako ndipo ukapatikana.

Kipimo chako juu ya pendo lako Kwa Mungu kinapimwa na muda unaoutumia Kwa ajili yake hasa katika kumwabudu na kumtumikia.

Kila dakika unayoitumia Kwa ajili yake inamchochea kukuhurumia na hata kukuondolea hukumu ya adhabu iliyokuwa mbele yako.

Muda unaoutumia katika maombi. Ndio muda pekee unaobadilisha maisha yako.

Maana Kwa maombi tunaumba.

Kwa maombi tunafungua waliofungwa.

Kwa maombi tunawatoa watu vifungoni.

Yakobo5:13
MTU wa Kwenu amekuwa hawezi, ni mdhaifu, anaumwa hauwezi kufaulu,hawezi kuwa na ndoa, hawezi kushika mimba n.k

Neno linasema na awaite wazee wa kanisa wamwombee, na maombi yao ya Imani yatamwokoa, na hata kama alikuwa ametenda dhambi Yule mhusika atasamehewa.

Kuishi bila kuomba,Kwa mkristo wa miaka mingi kama wewe,NI KUENDELEA  kuwaacha watu wa Mungu vifungoni, utumwani na kuwafanya waishi mbali na hatma zao.

Haukuzaliwa Kwa ajili ya kazi tu ya kutafuta pesa,
Haukuzaliwa ili ufanye biashara pekee yake,
Haukuzaliwa ili uoe, uzae, au uolewe, uzae kisha ufe,

Kuna kazi ya Mungu ya kuzileta nafsi zilizopotea katika ufalme wake.

Heshima yako Kwa Mungu hautaipata kutokana na nyumba uliyojenga, magari unayomiliki, cheo chako kazini, hivi VYOTE vinaweza kuwafanya wanadamu wakuinamie ila siyo Mungu.

Yesu anasema MTU akinitumikia , Baba yangu atamheshimu.

Kuishi bila kutumika, ni kukosa heshima Kwa Mungu.

NI aibu Kwa mkristo aliyebatizwa na kujazwa Roho kutojishughulisha na mambo ya Mungu Kwa kisingizio eti vyuma vimekaza, bajeti imekataa.

Kumbuka vile ulivyo umehurumiwa.

Hata Kula chakula kisha ukaenda maliwato na kikatoka umehurumiwa.
Kuna wengine kilikataa kutoka na wakafaa.

Hiyo kazi inayokufanya ushindwe kumheshimu Mungu na kumtumikia umeipata Kwa Huruma yake tu.

Kama Mungu asingekuhurumia, ungekuwa marehemu wa miaka mingi.

WAKATI unazaliwa, kuna wale ulizaliwa nao, hata wiki haikuishi wakafa, wengine hata mwaka haukuisha wakafa,

Lakini wewe uliachwa ili umletee Mungu heshima.
Lakini mbona badala ya heshima unamletea Mungu fedhaha, mbona kazi ya Mungu inakwama na WAKATI upo.

Mbona pesa yako haiwezi kusaidia kupeleka injili, Kwa matangazo, vipeperushi na hata Kwa njia ya mikutano ya Injili au Kwa kuwasafirisha wahubiri.

Kumbuka amekuhurumia.
Wewe ni chombo chake cha sifa.

Zaburi ya 103: 4
Aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na REHEMA.

Kuna siku uliumwa ukafikiri hautapona. Ulijaa hofu, ila akaja akaukomboa uhai wako na kaburi Kwa REHEMA zake.

Kwanini leo umesahau kwamba kama siyo Yesu ungekuwa ulishaiacha hiyo ofisini na ungekuwa kaburini kitambo,

Inakuwaje unakuwa mgumu kutenga muda wako Kwa ajili ya Mungu.

Kumbuka! Mungu anasubiri umtangaze, umwinue mbele za watu ili awavute wengi kuja kwake.

Mpendwa si elimu,
Siyo cheo chako wala cha mumeo vilivyokuacha hai leo.
Ni Huruma za Mungu.

Anza upya Kwa kuhakikisha unakuwa sehemu ya hili Kongamano la siku 90 za Kukomesha Mateso Kwa kufika au kutuma michango yako ili ituwezeshe kupeleka matangazo Kwa wengi na kuhakikisha habari njema ya ufalme haimpiti MTU.

Nina uhakika , Kwa kufanya Hivyo utakuwa umewahurumia nawengine.

Neno linasema heri wenye REHEMA maana na wao watahurumiwa. Mathayo 5.

Nawapenda na nawaombea Kwa Mungu mpate muda WA kuifanya kazi yake
# EV.MCHOME
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes