Headlines

Siri ya sadaka


ALHAJI ALICKO DANGOTE:- BILIONEA NAMBARI 1, AFRIKA..!!

Ukisoma kitabu cha "African Apostles" kilichoandikwa na Leke Leecroft, pamoja na visa vingi vya kushangaza, kuamsha roho na kukuza imani kwa namna ya pekee:- kuna kisa kingine halisi kinachomuhusu hayati Archbishop Benson Idahosa na Alhaji Alicko Dangote, bilionea namba 67 duniani na nambari moja Afrika.

Kwa wasiofahamu ni kwamba, Hayati Archbishop Idahosa anatajwa kama "paonia"(pioneer), wa uamsho wa wokovu barani Afrika. Ni muhubiri aliehubiri injili iliyoambatana na miujiza ya ajabu ikiwemo kufufua wafu, kuponya wagonjwa na mguso uliowafanya maelfu kuokoka nchini Nigeria, Afrika Magharibi na duniani kote, miaka ya hamsini kuja juu. Huwezi kuitaja historia ya uamsho wa wokovu duniani (pentecostalism) pasipo kumtaja hayati Archbishop Benson Idahosa.

Miaka ya 1970 Archbishop Idahosa alitembelewa na wahubiri wawili wakubwa katika historia ya Upentekoste duniani, T.L na Daisy Osborn, nao wakafikia na kuhubiri katika kanisa la Miracle Centre of Church of God Mission. Siku ya mwisho, ibada ikachelewa sana kuisha na ilitakiwa waondoke siku hiyo hiyo kurudi Marekani kwa kuunganishia(kupitia) Ufaransa. Archbishop Idahosa akiwa na wageni wake hao wakafika uwanja wa ndege na kuambiwa ndege imebaki moja ya mwisho nayo imejaa na inajiandaa kuondoka.

Alichofanya, akaendesha gari yake na kwenda kuisimamisja kwenye njia ya ndege iliyokuwa imeshaanza kuruka. Ikabidi ndege isimame na marubani washuke kujua kuna nini. Archbishop Idahosa akawaambia marubani, "Kwenye gari langu kuna watumishi wawili wa Mungu, nao ni lazima wasafiri leo na ndege hii". Marubani wakamweleza Archbishop Idahosa ya kwamba ndege imejaa na haiwezekani kupakia abiria hao wawili. Yeye (Idahosa) akawaomba marubani aingie ndani ya ndege kuongea na abiria, wakamruhusu!

Alipoingia ndani ya ndege akawaambia abiria, "Naomba watu wawili washuke, ......ili wageni wangu wapate kusafiri". Dakika kadhaa zikapita hakuna aliejitokeza, huku abiria wengine wakichukizwa kupotezewa muda na wengine wakajifanya wamelala, hawasikii. Baadae kidogo kutoka siti za nyuma ya ndege, akasimama kijana mdogo na kumuamuru aliekuwa nae kiti kimoja nae kusimama, kisha wakaanza kushuka kwenye ndege. Archbishop Idahosa akamuuliza yule kijana, "Jina lako nani kijana?", kijana akajibu, "Alicko Dangote na huyu ni msaidizi wangu". Wakati huo Alicko Dangote ndio alikuwa ameanza biashara ya kununua na kuuza sementi, akiwa na mtaji mdogo tu. (Dangote na msaidizi wake, waliacha siti pasipo kudai kufidiwa nauli zao, ina maana kesho walikata tiketi upya kwa hela zao zingine)

Kitendo cha Alicko Dangote na msaidizi wake kuacha siti ili watumishi wa Mungu wasafiri, kilimfanya Archbishop Idahosa kutoa machozi, na akatamka maneno yafuatayo kwa Dangote, "Umesimama kumuheshimu Mungu, dunia itasimama kwa ajili yako kukuheshimu. Mungu wangu atakubariki. Mungu atazifanikisha biashara zako hata zivuke mipaka ya Afrika na utabarikiwa kupita maelezo(beyond measures)".

INATUFUNDISHA NINI HII?

1. Alhaji Alicko Dangote amepata kunukuliwa akisema, pamoja na mambo mengine anaamini kwamba maombi ya Archbishop Idahosa yameendelea kuwa baraka katika biashara zake. Wafuatiliaji wa mambo wanaomfahamu Archbishop Idahosa, T.L, na Disnay Osborn na nguvu walizotembea nazo kiroho, na namna Alhaji Dangote alivyowagusa kwa sadaka yake ya kuwaachia zile siti pasipo kudai kurejeshewa nauli:- hawashangai kuona kuwa leo hii dunia inasimama kwa ajili ya Alhaji Dangote, hawashangai kuona kwamba biashara za Alhaji Dangote zimevuka Afrika na hawashangai kuona kwamba Alhaji Dangote amebarikiwa beyond measures!

2. Tukiongelea mafanikio kiuchumi watu wengi hudhani kuwa msingi wa kufanikiwa kiuchumi ni kujua fursa, kupata mitaji, kufanya kazi kwa bidii na mazagazaga kama hayo. Ukweli ni kwamba siri nyingine ya mafanikio kiuchumi ipo katika masuala ya imani na kiroho. Jambo la kufahamu ni kwamba mafanikio kiuchumi yana uhusiano wa moja kwa moja na sadaka unazozitoa kwa Mungu na unavyosapoti watumishi wa Mungu.

Waliofanikiwa wanaweza wasikueleze yote, lakini wengi kufanikiwa kwao ni "traceable" katika eneo la sadaka.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes