Home > Darasa > Tujifunze kutoka kwa mti na kijiti
Tujifunze kutoka kwa mti na kijiti
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 08, 2019 • Darasa • Comments : 0
Uchunguze mti huu vizuri. Kijiti unachokiona kilifungwa wakati mti ukiwa mdogo, mti ukiwa haujiwezi, mti ukiwa tegemezi, ukaegemea na kutegemea kijiti kupata msaada wa kukua. Ilipofika wakati mti unanguvu, wakati ambao mti hauhitaji tena msaada wa kijiti, kijiti kikabaki kuwa kikwazo cha ukuaji wa mti. Mti ukaona haiwezekani nizuiliwe kukua na kuendelea kwasababu ya kijiti nilichokitegemea awali. Mti ukakivunja kijiti iliuweze kuendelea kukua. Kuna nyakati maishani mwako kamwe hautokua, hautoongezeka wala hutoendelea kama utategemea msaada, kubebwa na kuegemea wengine. Ndio, najua kunanyakati unahitaji kusaidiwa lakini usijibweteke kwenye misaada hiyo. Komaza miguu na mikono yako ili uweze kusimama na kufanya vitu mwenyewe. Na endapo ukiona kijiti kinakuzuia. Kivunje uendelee kupaaa juu. Yamkini yaliyoko mbele yako ni makubwa kuliko unayoyaona sasa. See you at the top #
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment