Nasema kua agano la kale linahusu Mungu kutubeba na kutuokoa wanadamu .. Agano jipya linahusu Mwanadamu kumbeba Mungu kwa maana ya kutangaza neno lake na kueneza injili yake .
Nasema ila binadamu hatuishi hivyo siku hizi bado tunaishi na kuabudu tukiomba huruma ya Mungu watu wanaenda nyumba za ibada kufata huruma ya mungu na kutatuliwa matatizo yao.
Sio vibaya kufanya hivi ila kwa wakati tuliopo hatukua tunapaswa kuishi kwa kumkimbilia yeye ikiwa kama lengo kuu la kumuabudu .. hapa tunakua tunamrudisha nyuma mwenyezi Mungu na inaonesha Mungu haishi ndani yetu ndio maana tunamkimbilia alipo. Mungu alitakiwa aishi ndani yetu na hata tukiwa tunaenda nyumba za ibada tuwe tunaenda kujifunza jinsi ya kusambaza neno lake zaid kuliko kwenda kusambaziwa sisi neno lake.
Nasemakua kwa sasa hali ndio inazidi kua mbaya zaid tofauti na wakati ule wao wana mpokea Mungu kwenye maisha yao, anasema kipindi hicho cha zamani ukimpokea Mungu unakua una shauku ya wewe kusambaza neno la Mungu ila siku hizi wana wakimpokea Mungu wanataka Mungu awahurumie tu makosa yao tunapaswa kua zaidi ya hapa tunapaswa kumruhusu aishi ndani yetu.
Pia nilipata nafasi ya kumsikia Mwalimu Mwakasege Akisema Kua Mitaala Ya kielimu ya sasa hivi hasa ya kiafrica haiandai kijana kujijenga kifikra ila na kutatua shida zake mwenyewe ila inaandaa vijana kuja kuitumia serikali au taasisi na hii ni hatari kwa ukuaji wa taifa na kupata ubunifu mpya.
Course nyingi zinaanzishwa kwakua kuna uhitaji wa taaluma flani kiwandani u kwenye soko na kipindi mahitaji haya yakipungua vijana wanashindwa kujua taaluma zao wazifanyie nini.
Mitaala ya kielimu inapaswa iandaliwe kutokana na malengo yaliokuwepo kwa kila uzao nq changamoto zake zilizokuwepo vijana wafundishwe kufikiri ..
Niliposoma kuhusu alivyosema docta Ellie na alivyosema mwalimu Mwakasege nikaja kujisahihisha kwa maono yangu niliokua nayo siku zote kuhusu jamii tunayo ishi .
Nilikua nina fikiri kua ushoga, uvunjifu wa maadili ni athari za Technology ila sio ivyo ila hizi ni athari za utegemezi .. dunia hii tunaishi kwenye hali ya utegemezi sana.. Binadamu tunasubiri sana tufanyiwe kitu kuliko sisi tufanye kitu.
Kama tunatumia muda mwingi wa ibada kuomba huruma ya Mungu kuliko kumruhusu mungu aishi ndani yetu na sisi tukamtangaze kwa watu wengine basi tusitegemee kama tunaweza kusimamia mambo mengi mengine. utegemezi wetu huanzia hapa tunapo kiuka lengo kuu la agano.
Tusishangae kwanini wavulana wengi siku hizi wanapenda kulelewa na wanaume wenzao au na wamama watu wazima ... tusishangae kwanini wadada wengi siku hizi mapenzi kwao ni vile mwanaume ana muhudumia na sio yeye kuwaza yeye anajiandaaje kua mke na mama hapo baadae ataenda kuhudumia vipi familia yake .. tusishangae vijana wengi wanalia kukosa ajira ndio setup waliopata mashuleni kuja kufanyia kazi kitu kilichopo.
Kikawaida viongozi au wavumbuzi hua ni kikundi cha watu wachache ukilinganisha na jamii husika ila kwa uchache wao idadi inazidi kupungua mwisho wa siku tunakosa viongozi wa kidini na wa kisiasa waliokomaa kuongoza na tunakosa wavumbuzi wa mambo maana tunakosa kuishi maishi ya kutatua changamoto na kujijenga .
Kuna nguvu kubwa inatakiwa kufanyika ili kutoka hapa tulipo .. tunahitaji mapinduzi ya kiimani kwa kiasi kikubwa sana ..
Home >Unlabelled >
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment