Home > Uchungu > VITU VINAVYO FANYA MTU KUA NA UCHUNGU
VITU VINAVYO FANYA MTU KUA NA UCHUNGU
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 05, 2019 • Uchungu • Comments : 0
1.Maumivu Kutokana:
-Habari Mbaya
-Matukio Mabaya Maishani Mwake
-Kuumizwa Na Watu Wa Karibu Au Ambao Uliwaamini Na Kuwategemea
2.Hasira Iliyolimbikizwa [Iliyokaa Muda Mrefu Bila Kushughulikiwa]
Mtu Mwenye Hasira Ana Kasoro Zifuatazo:
-Hana Upendo Wa Kimungu Ndani Yake, La Sivyo Angeachilia Na Asingehifadhi Maudhi Ndani Yake.
-Hana Nguvu Ya Kusamehe, Angekuwa Anasamehe Haraka, Asingeweza Kurundika Hasira Ambayo Baada Ya Muda Italeta Uchungu Nafsini.
MADHARA YA UCHUNGU NAFSINI:
i)Inapunguza KASI YA MAISHA YA MTU (Isaya 38:15b)
ii)Inafungua Mlango Kwa MAGONJWA Kama BP, Ulcers, Matatizo Ya Moyo, Akili Nakadhalika
iii)Inafungua MLANGO KWA NGUVU ZA GIZA [Mapepo Na Roho Chafu] Yaani INAMPA IBILISI NAFASI (Waefeso 4:27).
iv)Inapunguza UWEZO WA KUFIKIRI NA KUTUMIA AKILI Kufanya MAAMUZI SAHIHI- Maamuzi Mengi yanakuwa yametwaliwa na HASIRA NA UCHUNGU
v)Inafungulia LUGHA CHAFU NA MBAYA TOKA KWA MWENYE UCHUNGU [hasira Au Maumivu], MANENO MAOVU YANAMTOKA KIRAHISI Ambayo Badala Ua Kujenga Yanabomoa, Badala Ya Kubariki Yana Laani (Waefeso 4:29).
"Iweni Na Hasira Lakini Msitende Dhambi; JUA LISICHWE NA UCHUNGU WENU HAUJAWATOKA" (Waefeso 4:26).
"Kwa Maana HASIRA YA MWANADAMU Haitendi HAKI YA MUNGU" (Yakobo 1:20).
DAWA YA UCHUNGU:
1.Mpe Ruhusa Roho Mtakatifu Akusaidie (Yohana 14:16)
2.Mweleze Mungu Kuhusu Matukio Uliyopitia YALIYOKUJERUHI NA KUKUUMIZA Na UOMBE NGUVU YA KUSAMEHE NA KUWAACHILIA WOTE WALIOKUUMIZA
3.Omba ROHO MTAKATIFU ALIMIMINE PENDO LAKE MOYONI MWAKO (Warumi 5:5)
4.JAZA NENO LA MUNGU KWA WINGI NDANI YAKO (Wakolosai 3:16)
Acha uchungu
Maana ni roho inayo kudhoofisha kimwili na kiroho.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment