====================================
IMEANDIKWA: “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana TULIIONA NYOTA YAKE MASHARIKI, nasi tumekuja kumsujudia (kum’heshimu).”
๐» MATHAYO 2:1-2 «๐
====================================
Nyota ya Yesu iling’aa ikimtangaza katika nchi za mashariki, nayo ilieleza habari za neema ya cheo alichonacho iliyowekwa na Mungu Baba mwenyewe; ndiposa walikuja wakimtafuta mtoto aliyezaliwa, mwenye neema ya KIFALME.
Yaani ya kuwa mtawala mkuu katikati ya Israeli.
Nyota inayosemwa hapa sio ile ya kawaida ya angani, japo kuna namna ambayo waliopewa neema wanaweza kupewa kuziona angani; ila hata hivyo, nyota hizi zina-husu zaidi KIPAWA alichozaliwa nayo mtu kwa ajili ya kufanikisha hatua za kimaisha zake yeye aliyejaliwa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
IMEANDIKWA: “Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kila kigeukapo hufanikiwa.” ๐ » MITHALI 17:8
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
KUNA SIFA TATU ZA NYOTA MAISHANI.
``````````````````````````````````````````````````````````````````
SIFA YA KWANZA. (1)
•Nyota hutambulisha kipawa au neema ya mtu aliyozaliwa nayo, ambayo itamwinua maishani.
SIFA YA PILI. (2)
•Nyota huwavuta watu kwa ajili ya kukuijia kwa wema (ndiposa mama jusi walikuja na zawadi).
SIFA YA TATU. (3)
•Nyota ya mtu hufunua heshima yake katikati ya wanadamu, ikitiwa giza heshima hupungua au hupotea kabisa (Mungu akutetee leo hii).
```````````````````````````````````````````````````````````````````
Kumekuwepo na waganga ambao wanajinadi kuwa wanasafisha nyota za watu, kumbe kwa hila za nguvu za giza» wamekuwa wakifanya kazi ya kuwaibia; kwani baba yao» Shetani ni mwizi na baba wa uongo, wanafuata njia zake.
KWA JINA LA YESU KRISTO, NAAMURU KILA UCHAWI NA UGANGA INAYOFUATILIA KUIBA NYOTA YAKO; ISAMBARATIKE KWA MAMLAKA YA JINA KUU LA YESU KRISTO ALIYE HAI !!...
BADALA YAKE DAMU YAKE KRISTO, INENE MEMA JUU YAKO NA NYOTA YAKO; ILI UZIDI KUNG’AA KWA UTUKUFU WA MUNGU BABA.
๐ Amina!! Amina!! ๐
=====================================
#mtu aliye ibuwa nyota yake nairejesha kwa damu ya Yesu.
(ISAYA 42:22)
Post a Comment