Headlines

Kwanini masikini wanabaki kama walivyo

KWANINI MASKINI WANABAKI HIVYO....

Mtu mmoja aliwahi kusema, "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?

Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji.

Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.

Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.

Kuwa MWANAUME sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.

Lazima uchuku maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.

Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.

Watu wasiofaa kabisa kuhudumiwa hapa duniani ni WATU MASKINI.

UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.

Angalia sababu hizi
1)  ukiwapa bure, watahisi ni mtego.

2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida

3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela

4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?

5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo

6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?

7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.

8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.

9) ukimuuliza ni ni anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"

10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko takatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.

11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.

Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua

Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao mdogo.

Kumbuka: kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kuvichukua hatua.
By
EV.MCHOME
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes