Headlines

Mahusiano yaliyo kati ya sadaka ya zaka na uchumi wako

MAHUSIANO YALIYO KUWEPO KATI YA ZAKA YAKO NA .MAHUSIANO YAKO YA KIUCHUMI.
EV.MCHOME 0672870833
Mambo makuu 4 ambayo Mungu amefunga kwenye zaka.
Kila sadaka ina kazi yake katika ulimwengu wa kiroho ina maombi yake pia.
Unapo toa zaka kuna matarajio flani Mungu anatazamia uyaombe.

Malaik 3:7
Kumb 14:22
#Zaka ni Agizo la Mungu.
Mungu alisema wasiache
#Zaka sio ya kwako.
Kvp hivi kitu chako unaweza kujiibia.ukisikia umeiba inamaana sio yako umechukua bila idhini ya mhusika.
Ukiacha kutoa zaka wewe ni mwizi. Mbele za macho ya Mungu.
Hivi Mungu unaye mwibia ndiye unaye muomba akubariki akuinue akulinde akupiganie hali Unamuibia.
Malaiki 3:8
Hivi zaka ni nini? NI AINA YA SADAKA AMBAYO UTOAJI WAKE NI SEHEMU YA KUMI YA MAPATO YAKO.
hii ni sehemu ya kumi Mungu aliyo weka katika mapato yako. Hii sio yako kabisaaaa.

Unapo toa cha Mungu na ukabakiwa na chakwako .kile cha kwako unacho baki nacho ni pesa iliyo barikiwa .
Pesa iliyo barikiwa ndio inanguvu za kukufanya ufanikiwe.kwa Kua ina baraka za Mungu.

Ukiamua Kula zaka
#umeamua kuachilia laana kwenye kazi zako.
Malaika 3:9
Kuna pesa iliyo Barikiwa lakini kuna pesa iliyo laaniwa.

Kulaaniwa ni nini :-mtaitumia hiyo fedha lakini hamta fanikiwa katika hayo mliyo tazamia kuyapata.
Fikiri Mungu amekulaani kisha unamuomba akubariki. Je utabarikiwa vipi.

Hakuna wa kuiondoa laana ya Mungu juu yako mpaka pale utakapo amua kugeuka na kuyafuata magizo ya Mungu.
Kuna watu wanateseka sanaa wanafanya kazi wanapata pesa yakula tu .
Hapo hakuna pepo wala mchawi umekula fungu la kumi na Mungu amekulaani.

1.Zaka imefungwa na baraka za kazi ya mikono yako.
Tort 14:28-29.
Wakristo wakipewa maagizo na Mungu wanaacha kabisaa.
Wenzako wa giza kuna ubani udi mkaa.
Jiulize vya nini ?
Mafanikio ya mtu yapo katika zaka ukiacha kutoa zaka kazi ya mikono yako inalaaniwa.

2.Zaka imeunganishwa na MPENYO WAKO WA KIMAISHA.
Malaki 3:10
Madirisha ya mbinguni ni nini?
Huu ndio mpenyo wa mafaniko katika maisha yako. Kitendo cha kutoa zaka Mungu anabariki kazi ya mikono yako.
Mbingu zinakua wazi kwa ajili yako.hapa ni maendeleo kwenda mbele.
Kumiliki mali;kujenga;biashara;kwenye huduma.
Mpenyo .
Kuto kupiga hatua sehemu yeyote ile ni ishara kua shetani amekamata kisigino.
Mwnz 25:22-26
Taifa la esau limetoka lakini taifa la yakobo limemshika kisigino.
Ukishikwa kisigino ni unazuiwa kabisa usipige hatua.
Mwanzo 49:17
Njia za mafanikio kuna nyoka ambaye ni dani na bafe kazi yao ni kuuma visigino vya farasi yaani mwenye kasi ya maendeleo.
Farasi ni kitu kilicho kubeba wewe na kukuwezesha wewe kupiga hatua katika maisha.
Kazi yangu ni kitu kilicho nibeba ndio farasi wangu kwa kazi yangu naendesha maisha .siri ya kupiga hatua ni kazi yangu ambayo ni farasi .lakini akina dani na bafe shetani wanakiwinda .
Farasi akipogwa yani wewe upandaye utaanguaka chali.
Yani kuna watu wapo chali KIUCHUMI .

Nitaendelea
Sehemu ya 2

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes