Headlines

Nguvu ya Mungu juu yako

Nilipokuwa MDOGO nilikuwa namuona bibi akichambua maharage, alikuwa anaweka MAHARAGE MAZIMA kwenye sufuria ya KUPIKA, na maharage MABOVU alikuwa anayatoa kisha anayatupa mbali jalalani! -CHAKUSHANGAZA , mvua ikinyesha maharage yale yale mabovu yanaanza kuota na kuchepua..... -YALITUPWA yakiwa mabovu YASIYOFAA. lakini YANAOTA. kisha yanatoa maharage mengine mazima na bora zaidi kuliko yalivyotupwa mwanzo yakiwa mabovu. !!
-Hii inanifanya nijifunze MUNGU  anavyokuona ni tofauti kabisa na watu wanavyokuona ..inawezekana UKAONWA na watu kama maharage mabovu leo.
Lakini hakika MVUA YA MUNGU ikinyesha UTAOTA  na kuwa wa THAMANI na KUZAA na KUTENGENEZA WATU WENGINE BORA ZAIDI YA WEWE. Inahitaji wakati tuu na UVUMILIVU. -KUSUDI LA MUNGU na mawazo ya Mungu ni tafauti na yawanadamu ..Usikate tamaa wala usivunjike Moyo *YOUR RAIN SEASON IS COMING.

God's servant William s.Mchome

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes