Headlines

Nyakati ngumu hazidumu

NYAKATI NGUMU HAZIDUMU.

KATIKA HUDUMA KUNA NYAKATI MBILI.

1. KUNA SAA UNAKUWA MWALIMU UKIFUNDISHA WENGINE.

2. KUNA SAA UNAGEUKA UBAO AMBAO WENGINE WANAJIFUNZIA.

Kila mtu huwa anapenda hiyo sehemu ya kwanza maana ndio ina mialiko mbalimbali, zawadi na sadaka unazopewa kwa yale uliyofundisha na namna watu walivyosaidika. Unasikia shuhuda kila upande, unapigiwa simu mpaka usiku wa manane kusaidia watu kugfanya maamuzi, unazuia wengine wasijiue, unaambia wangine wasiache waume/wake zao, unawapa maandiko ya faraja waliofiwa na kukemea mapepo kwa wengine. Wengine wanakuchosha na stori ndefu na kukusimulia ndoto zisizoeleweka uwape tafsiri.

Halafu hiyo ya pili sasa ndio pale mfariji anapohitaji faraja. Wewe ndio unageuka ubao wa kufundishia na masomo yanakuwa maisha yako au matukio magumu sana yanayotokea kwenye maisha yako binafsi. Hapa kuna watu watatilia Shaka hata wito wako. Huu ni wakati ambao SIMBA wa Yuda anajitokeza kama MWANAKONDOO WA MUNGU. Anaonekana hana nguvu ya kurarua. Huu ni wakati mbingu inakaa kimya ili ufanye mtihani.

Hapa ndipo unaona maandiko yametoka kwenye kitabu na yameingia kwenye ratiba ya kawaida ya maisha yako ya kila siku. Ndipo utapata jibu kwamba Mungu aliyefufua mtoto wa Mjane wa Sarepta (1 Wafalme 17:7-24) na mtoto wa Mwanamke Mshunami (2 Wafalme 4:8-37) ndio huyo huyo Mungu aliyeruhusu watoto 10 wa Ayubu wafe kwa siku moja kwa kuangukiwa na nyumba. (Ayubu 1:13-22)

Ndipo utajua Mungu aliyezuia nguvu za moto zisiwateketeze Kina Shadraki (Daniel 3) na kumkomboa Danieli asiliwe na simba (Danieli 6:10-24) ndio huyo huyo Mungu aliyeacha Yakobo achinjwe na Herode (Matendo 12:1-3) aliyeacha Stefano apigwe mawe hadi kufa. (Matendo 7:54-60)Yaani njia zake hazichunguziki, hekima yake haielezeki.

Anamuacha Nabii Yohana Mbatizaji achinjwe (Mathayo 14:1-12) halafu anaenda kumfufua Lazaro aliyekaa kaburini siku nne. (Yohana 11:1-45)
Jambazi anatoka kuiba na kuua na anafanikiwa kukwepa risasi na kuwatoroka polisi, halafu Muhubiri anakufa kwa ajali akiwa njiani kwenda kwenye huduma.

Ndipo unagundua kuwa hata wewe ingawa unafundisha lakini bado hujamjua Mungu na bado unahitaji kujifunza.

HUYU MUNGU ANATISHA JAMANI. KUMUELEWA NI MPAKA YEYE MWENYEWE AKUSAIDIE. (Luka 24:45) MWAMINI TU ITAKUTOSHA.

EV.MCHOME
✝️🔯

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes