Headlines

Mungu wa Ibrahim Isaka na yakobo

KWANINI MUNGU,  ANAITWA; MUNGU WA IBRAHIMU,ISAKA,NA YAKOBO?
===============================

MBARAKA WA YUSUFU  MTOTO WA YAKOBO;-
1. Mwa.39:21-Yusufu akiwa grezani alipata kibali kwa mkuu wa gereza na kuchaguliwa kuwa mkuu wa wafungwa wote.Yusufu alipata kibali kwa mpango wa Mungu kwasababu alimtukuza Mungu kwa kuogopa kutenda dhambi ya uzinzi na mke wa Pontifa pamoja na kwamba mke huyo alimlazimisha Yusufu aanguke kwenye dhambi hiyo.Sisi kama kanisa tunajifunza kuwa dhambi ya uzinzi ni lazima uishinde kwa kuikimbia kama alivyofanya mtu wa mbaraka Yusufu.Mtume Paulo alisisitiza kuwa ni lazima uikimbie dhambi ya uzinzi maana dhambi nyingine zote hufanyika nje ya mwili lakini ni dhambi ya uzinzi pekee ndiyo ifanyikayo ndani ya mwili a mwanadamu
2. Mwa.39:22-Yusufu apewa mamlaka ya kuwa juu ya wafungwa wote.Sisi nasi kama kanisa tumepewa vitu mbalimbali na Bwana wetu Yesu Kristo na anaweza kuvichukua wakati wowote.
3. Mwa.40:40-Yusufu kuingia gerezani ni sawa na kipawa chako kuanza kufanya kazi unapokuwa katika hali ya mapito magumu yanayofanana na kuwa gerezani ingawa wewe tayari uko huru tena huru kwelikweli katika Yesu Kristo.Yusufu alipokea kipawa cha kutafsiri ndoto akiwa katika utumwa wa gerezani.
4. Mwa.40:1- Mnyweshaji wa mfalme aliota ndto iliyomfadhaisha na kulazimka kwenda kumwoona Yusufu akiwa gerezani ili amtafsirie ndoto hiyo.Katika tukio hili ambalo walifahamishwa maakida hakika wote walifadhaika na kuonyesha nyuso zao zikiwa zimekunjamana na ndipo Yusufu alipowauliza kwanini nyuso zenu zimekunjamana?.Sisi kama kanisa tumekuwa na ndoto nyingi katika maisha yetu ya kila siku na ambazo hadi sasa bado hazijapata tafsiri tuombe sasa Roho atupe kipawa cha kutafsiri ndoto zetu mbalimbali na mipango mbali mbali ya maisha yetu ya kawaida ifanikiwe sasa.Lakini anayeweza kutafsiri ndoto zetu hizo ni Mungu peke yake kwa kutumia mmojawetu ataakaye pokea karama ya kutafsiri ndoto.

Yusufu alimtafsiria ndoto yule mnyweshaji wa mfalme na akamtaka sharti moja ya kwamba asikose kumtaja huko kwa mfalme atakaporudi.Hapa tunajifunza kuwa si lazima kulipa fedha au shukrani ya vitu unapohudumiwa na mwenye kipawa au karama kitu muhimu zaidi ni kumtaja vizuri huyo mhudumu ili iwe ushuhuda kwa mataifa nao wamjue Yesu na kuokoka hivyo kuleta utukufu kwa Mungu wa Ibrahiomu,Isaka na Yakobo.

Mwokaji wa mikate naye aliota ndoto ambayo pia ilitafsiriwa na Yusufu ingawa tafsiri hiyo haikumfurahisha huyo mwokaji mikate.Hapa tunajifunza kuwa sio tafsiri zote tutakazopewa na wenye karama ya tafsiri ya ndoto itatufurahisha, cha msingi ni kujua kuwa tafsiri inatoka kwa Mungu mwenyewe kupitia mwenye karama, kwa hiyo ni muhimu kumshukuru Mungu na kuomba akusaidie kujirekebisha kama umepewa tafsiri ya kutaka utengeze maisha yako mahali ambapo umejikwaa na kumhuzunisha Roho Mtakatifu akaaye katika hekalu takatifu yaani mioyo yetu.

Mwa.40:8-14-Yule mnyweshaji wa mfalme mkuu hatimaye alimkumbuka Yusufu na kumtaja kwa mfalme Farao ili mpango wa  Yusufu kuinuliwa utimie sawa sawa na mapenzi ya Mungu.Yusufu alikwenda kwa Farao na kutakiwa aseme ni nani aliyetafsiri ndoto hizo Yusufu akamwambie kuwa si yeye ila ni Mungu aliye ndani ya Yusufu ndiye aliyetoa tafsiri hizo.Kabla Yusufu hajaingia kwa Farao
alitaiwa fanye mambo yafuatayo:

 Kunyoa nywele
 Kubadili nguo
 Kuingia ndani.

Mwa.41:41-Yusufu alipandishwa cheo na kuwa kama waziri mkuu kwa wakati huo.Hatimaye alivalishwa vitu vifuatavyo;
1. Mavazi ya kitani safi –nasi tutavalishwa mavazi safi tutakaposhinda na kuingia mbinguni kwenye makao mazuri
2. Pete kama ishara ya mamlaka nasi tutapewa mamlaka ya kutawala pamoja na Yesu tutakapofika mbinguni kwenye kao zuri
3. Mkufu wa dhahabu ikiwa ni ishara ya ushindi wa majaribu mbalimbali aliyopitia nasi pia tutvalishwa nishani ya ushindi tutakaposhinda majaribu mbalimbali tunayopitia katika safari hii ya kuelekea mbinguni.Tahadhari tunayotakiwa kuchukua katika maisha ya kawaida ni kwamba si vizuri kuvaa mkufu bila kutakiwa kufanya hivyo na Mungu maana shetani atakwenda kushitaki kwa Mungu kuwa ni majaribu gani uliyoshinda hata ukajivalisha wewe mwenyewe hapa duniani?

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes