Headlines

Malaika Rafaeli

MALAIKA MKUU RAFAEL
===============
MALAIKA MKUU Rafael,  ni  miongoni mwa mabilioni ya MALAIKA viongozi wamaosimamia vikosi vya malaika mashujaa na wapiganaji wa mbinguni.

Maana ya Jina Rafael:
---------------------------------
Maana ya Jina  Rafael ni: MUNGU AMEPONYA.   Katika zile Nuru zinazoonekana nyuma ya kiti cha Enzi cha Mungu Baba kama Upinde wa mvua,  Malaika kiongozi au mkuu Rafael anatumika na Nuru ya Rangi ya Kijani.  Nuru hii kwa Lugha ya mbinguni inaitwa; NURU YA KWELI.    Na KWELI ya mbinguni ni Yesu Kristo.

RANGI YA KIJANI
------------------------------
 Rangi ya Kijani inawakilisha: AMANI YA YESU KRISTO. Huko mbinguni , hii ni moja ya ofisi kubwa sana inayohudumiwa na malaika wakuu na wapekee sana.

Vitengo ndani ya Ofisi ya AMANI,  mbinguni
--------------------------------
1. Amani iletayo kibali.  Luka 2:14.
2. Habari njema ni mojawapo ya kitengo Katika ofisi hii ambapo wamejaa malaika wengi waletao Habari njema za aina nyingi sana kutoka ulimwengu wa roho na wa mwili.
3. Efeso 2: 14. Amani  iletayo mahusiano mema  kati ya Mungu na wanadamu.
4. Efeso 2:17.  Injili ya Amani.  Efeso 6:15.
5. Amani ya moyo.
6. Amani ya akili.
7. Amani ya mwili= misuli.
8. Amani  ikaayo mifupani.
Mithali 3:1-8,  Ebr 4:12.

SIKU YAO MAALUMU
----------------------------------
Siku maalumu ambayo vikosi vilivyo chini ya Malaika Rafael hushuka Duniani kwa kusudi maalumu la Yehovah ni: Jumatano.

Kazi za Malaika waliochini ya Malaika mkuu Rafael:=
-------------------------------
1. Chini ya ukuu wa Yesu Kristo,  Huondoa  roho ya upweke.
2. Wanashughulikia matatizo yote ya Akili na saikolojia.
3. Kuleta Habari njema.
4. Kuhuisha uhai uliopungua ndani ya mifupa.
5. Huwasaidia waliologwa na kutupiwa majini.
6. Hushughulikia matatizo yaliyo Nafsini.
7. Wanatumika idara ya uponyaji wa maarifa kutoka mbinguni.
8. Analeta akili naugunduzi wa dawa kutoka  mbinguni  zinazotibu wanadamu magonjwa ya kimwili.
9. Wanahusika  kuzileta roho za watumishi ili zizaliwe hapa Duniani kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Luka 2:8-13.

Share this:

1 comment :

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes