MALAIKA MKUU JEREMIEL
==================
Malaika MKUU JEREMIEL ni miongoni mwa Malaika viongozi wanaosimama mbele za Mungu Mtakatifu. Maana ya jina JEREMIEL ni; Rehema za Mungu Mtakatifu. Kut 20: 6. Waebrania 9:1- 5. Kut 25:18.
---------------------------------
Ndani ya Ofisi ya Rehema ya Mungu Baba, Malaika MKUU JEREMIEL anafanya kazi kama katibu kiongozi anaye waongoza Malaika wanaohudumu Ofisi ya Rehema za Mungu.
Sawasawa na ; Ebr 9: 2-5. Mabawa ya makerubi yalikuwa yanaweka KIVULI katika eneo la KITI CHA REHEMA CHA MUNGU MTAKATIFU ili shauri lolote linaloletwa mbele ya Kiti cha Rehema kama ni gumu sana Mabawa yao yaliyojaa utukufu yanalifunika lile shauri ili mwanadamu anayehitaji Rehema Za Mungu aweze kusaidika na kusamehewa.
KAZI MALAIKA MKUU JEREMIEL NA VIKOSI VILIVYO CHINI YAKE;
---------------------------------
1. Wanafanya kazi kama watumishi wa mahakama ya rufaa ya mbinguni katika kuwasaidia wanadamu walio omba kupata Rehema za Mungu kutokana na makosa wametenda.
2. Pia hufanya kazi ya kuwatembeza wanadamu, hasa Manabii wanapotembelea ulimwengu wa roho hasa mbinguni kwa njia ya maono ya Mungu au mafunuo. Ezek 8:1-5. Efeso 1:17.
3. Anafanya kazi na watumishi hasa Makuhani wenye mamlaka ya kuombea watu Rehema au kuwakatia rufaa wale wenye kesi ngumu au wale ambao siku zao za kuishi zimeisha. 2Falme 20:1-9.
4. Popote panapohitaji Rehema za Mungu hasa Duniani, Malaika MKUU JEREMIEL anahusika pamoja na VIKOSI vyake.
5. Pia Malaika MKUU JEREMIEL anafanya kazi ya kuleta unabii Duniani kwa njia iitwayo; = Maono.
Ezek 8:3-5.
Sisi wanadamu tunahitaji Rehema za Mungu kila iitwapo Leo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment