MAMBO YA KUFANYA ILI UWE MTU MKUU:
Kuna mambo matatu ya msingi ya kuzingatia kama unataka kufikia ukuu, au kuwa mtu wa tofauti katika jamii yako:
1. KUJITAMBUA.
Tatizo kubwa tunalokumbana nalo katika nchi yetu ni watu wengi kutojitambua. Siku tutakapo jitambua nchi yetu haitabaki katika hali ya umaskini iliyo nayo.
Unatakiwa kujitambua ili ufiki kunako mtazamo, (focus). Hivyo, bila kujitambua, huwezi kuwa na mtazamo katika maisha.
Mfano:
Katika mashindano ya mbio za kasi kama vile za mita 100 au 400, kila mwanariadha huwekewa mistari yenye kuonyesha mipaka ya barabara anayotakiwa kukimbia. Sasa iwapo mmoja akiingia kwenye barabara ya mwenzake, atamkwamisha mwingine kuendelea mbele kukimbia. Na hili ndilo tatizo linalokumba Watanzania wengi: wanaanza mbio, lakini kila mmoja anaingia kwenye barabara ya mwenzake kutokana na kukosa kujitambua.
Hivyo,kwa kadri unavyotembea kwa adabu na nidhamu katika njia yako, inakupa kuwa na mtazamo, na mwelekeo. Siku ukijitambua, kuchanganyikiwa, mfadhaiko na kukata tamaa vinaondoka. Watumishi wa Mungu ndio wanaotengeneza njia ya kuwafikisha watu kunako kujitambua, kwa sababu pasipo Mungu hakuna kitakachotokea.
Kuna mambo matatu ya msingi ya kuzingatia kama unataka kufikia ukuu, au kuwa mtu wa tofauti katika jamii yako:
2. MTAZAMO
Mtazamo ni hali ya kutambua:
a. Umetoka wapi
b. Uko wapi
c. Unakwenda wapi
Huwezi kuwa mtu mkuu kama hujui ulipotoka. Lazima ufahamu chanzo chako ni nini? Unapobaini chanzo chako, ndipo wazo lenye kukuwezesha kufikia mafanikio huja.
Usiwadharau wazazi wako kwa kutofikia mahali ulipofikia wewe kielimu, maana kama mzazi amekuwezesha wewe kufaulu, basi hajashindwa. Hivyo, ni jukumu lako wewe mwanae kufuta ujinga wake, kwa kuenda hatua ya mbele zaidi ya ile waliyoishia wazazi wako.
Lazima ujue ni wapi ulipofika sasa. Maisha ni kama mbio za marathon. Mkimbiaji ni lazima wakati wote aangalie amefika wapi, na anahitaji kuongeza mwendo kiasi gani; maana bila kuongeza mwendo utashindwa kushinda mbio.
Kumaliza chuo kikuu haina maana kuwa ndio umeshafika, kwasababu:
- Elimu ya shule ni kwa ajili ya kukutoa ujinga
- Elimu ya maarifa ni kwa ajili ya kukufanya ufanikiwe.
Usipojua ulipotoka, sio rahisi kujua mahali ulipo.
- Yeyote aliyefeli somo la Historia, hawezi kuwa mtu mkuu au wa tofauti, bali anakuwa amechanganyikiwa na jamii yake hupata shida. Lakini yeyote anayeweza kufuatilia historia yake ndiye anayekuwa mtu wa tofauti (extraordinary) katika jamii yake.
- Historia ndiyo inayokupa lugha, na lugha hukupa kuunganisha kati ya ulipo, unapotoka na unapoenda. Mawasiliano ndiyo yanakupa kujua umbali ulipo, ulikotoka na unapokwenda. Na hapo ndipo Jiografia inapotokea.
Hivyo, kama unataka kuwa tajiri, ni lazima ujue kuwasiliana, maana lugha ndiyo inayombainisha mtu kuwa ni wa tofauti.
Kuna aina tatu za mawasiliano katika lugha:
A. Kuzungumza – Hii huashiria wapi ulipotokea,
B. Kuongea- Hii inatumika kuwaambia watu ni wapi ulipo,
C. Kusema- Hii huwaonyesha watu ubaadae wako.
Hizi namna tatu za mawasiliano ndiyo hubeba furushi zima la lugha. Ni muhimu kuzielewa, maana lugha pekee ndiyo itakutengenezea njia kwa ajili ya ubaadae wako. Lugha ndiyo inayobeba ‘chanya’ na ‘hasi’. Hivyo:
A. Unapozungumza, hakikisha ni kwa kutumia hekima
B. Ili uweze kuongea, hakikisha akili yako inafanya kazi
C. Unaposema, ruhusu maarifa kuingia kazini ili kukupa ubaadae wako
MAMBO YA KUFANYA ILI UWE MTU MKUU:
Kuna mambo matatu ya msingi ya kuzingatia kama unataka kufikia ukuu, au mtu wa tofauti katika jamii yako:
3. UTAMBULISHO
Kazi yake ni kukubainisha wewe ni nani, umetoka wapi, uko wapi na unaenda wapi.
Siku zote inabeba kusudio la moyo wako. na kwa kuwa ndio inayokupeleka mbele, ndio pekee inayokuwezesha kujua unapoenda.
Mfano:
Kuna vioo vitatu vya muhimu vya gari anavyotumia dereva katika kuendesha kwake. Kimoja ni kioo cha mbele, na viwili ni vioo vya upande wa kushoto na kulia wa gari (side mirrors). Dereva hutumia vioo vya upande wa kushoto na kulia ili kujua nyuma yake, kukoje katika upande wa kushoto na wa kulia. Lakini, ili kwenda mbele, hutumia kioo kimoja tu, cha mbele.
HIVYO: Unapokutana na visiki katika maisha, kabla ya kukata tamaa au kujiona umekwisha fika, kwanza chungulia nyuma kujua ulikotoka. Maana huwezi kujua kuwa umefika kama hujui ulikotoka. Angalia mazingira ya nyumbani kwenu, ili kubaini yale unayotaka kuyaacha kisha baada ya kuanza safari, chungulia nyuma kuona kama umeshayaacha mbali. Wakati ulipotaka kwenda mbele, wakati ulipotoka, ulitaka uwe nani, utimize malengo gani? Na hii ndiyo huitwa ‘CV’. CV haijengwi kwa kuandika shule ulizosoma, bali ili ujenge ‘CV’ yako, jiulize:
I. Umebadilisha maisha ya watu wangapi?
II. Watu wangapi wamefaidika kupitia unachofanya?
III. Umewasababisha watu wangapi kuwa watu wakuu, ambao wametoka mahali pa chini na kwenda mahali pa juu kupitia wewe?
Kwa kuweka haya mambo matatu kwenye ’CV’ yako, ndipo watu watakubali kuwa wewe kweli ni msomi. Lakini kwa sasa, jamii inalalamika kutokana na watu wengi kutokujitambua.
Hivyo, ili kufikia hapo, lazima ufanye mambo haya mawili:=
i Tengeneza ramani yako inayoonyesha wapi ulipotokea, wapi ulipo na wapi unapokwenda.
ii Andika kwenye daftari (diary) kuwa jamii itarajie nini kutokana na safari yako.
Usikate tamaa, maana aombaye hupewa, atafutaye huona na abishae hufunguliwa. Hivyo usikubali kuuza utu wako kwa kufanya ushenzi, bali tamani kuwa mtu unayeweza kuwa msaada.
Dunia imegawanywa katika makundi matatu:
a. Jamii ya watu walioshindwa
b. Jamii ya wanaochechemea (wafuasi)
c. Walioshinda, yaani watu wakuu.
Jamii ya walioshinda wanajua wanawaza nini, wanaongea nini, na wanafanya nini. Wanachowaza ndicho wanachoongea na ndicho wanachofanya.
Ubaadae wa mtu huenda mpaka vizazi vinne:
I. Miaka 0-30 ni kipindi cha kuweka mtazamo wa unayotaka kufanya (mindset and focus)
II. Miaka 31-60 ni kipindi cha kufanya
III. Miaka 61-90 ni kipindi cha kufanya utathmini.
IV. Miaka 91-120 ni kipindi cha kumshukuru Mungu.
Jitahidi ili ufikie mahali pa kuwa mtu mkuu, maana ukiwa mtu mdogo hakuna mtu anayekutambua, na ni rahisi kusukumwa.
Home > Maisha ya kila siku > Mambo ya kufanya ili uwe mkuu
Mambo ya kufanya ili uwe mkuu
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • December 04, 2019 • Maisha ya kila siku • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment