Headlines

Uchumi na maendeleo ya kanisa

MAARIFA YA KIUCHUMI KWA  MAKANISA AU HUDUMA:=.

Mwaka 1999 mwezi wa tisa, Askofu David Olaniyi Oyedepo kiongozi wa huduma ya “Winners Chapel” aliongoza ibada katika jingo la kanisa lake lenye uwezo wa kuchukua watu elfu hamsini (50,000) walio kaa. Mwezi Januari mwaka huu (2018), kitabu cha rekodi za dunia yaani “Guiness Book of world records” iliweka kanisa hilo kuwa miongoni mwa kanisa kubwa linalo chukua watu wengi zaidi duniani.

Sasa ni miaka kumi tu baada ya tukio hilo, mtumishi wa Mungu na kiongozi wa huduma ya “Dunamis International” Paul Idoko Enenche anakwenda kuzindua kanisa lake lenye uwezo wa kuchukua watu laki moja walio kaa, Novemba 24 mwaka huu 2018, pale Abuja Nigeria.

Katika tukio hilo lenye utukufu wa Mungu, mtumishi Reinhard Bonke, Dr Morris Cerullo, Askofu David Abioye na mchungaji W.F Kumuyi watahudhuria tukio hilo.
 Huyu mtumishi Paul Idoko Enenche ni mtoto wa kiroho wa Askofu David Olaniyi Oyedepo. Amefanya mara mbili ya baba yake wa kiroho, ni jambo jema.

HOJA YANGU NI IPI HASA??

Hoja yangu kwa watumishi wa Mungu ni kujifunza kuwa na maono makubwa kama haya au hata zaidi. Ni mara nyingi sana na inataka kuwa kama mazoea Fulani, kwamba makanisa mengi yana jengwa kama vibanda, kanisa likichukua watu “mia kadhaa” watumishi tunatosheka kabisa……!!!!! Lakini tazama ni jinsi gani wenzetu na hasa hizi nchi za Afrika Magharibi (kama umewahi kufika huko au unawafahamu vizuri) unaweza kutiwa wivu kupitia wao.

Na wakati mwingine hali ya majengo yetu inaonyesha uduni wa watu tulio nao… Tuwafundishe watu wetu kumiliki uchumi, tuwafundishe watu wetu kuujenga mwili wa Kristo, watu wajengwe katika misingi ya maarifa na ufahamu siyo “kuombewa ombewa kila wakati” (sikatai na sidharau maombi, nisinukuliwe vibaya).

NINI KIMEFANYIKA AFRIKA MAGHARIBI??

Kuna mambo kadhaa ambayo watu (walokole) wa Afrika Magharibi wamejengwa au kutambua:

1. Unyenyekevu na kuiheshimu ibada. Tazama ibada za watu hao, utaona kuna jambo la ziada wanafanya. Wamefundishwa sana kumhofu Mungu, wengi wao hawana mazoea kwenye ibada. Hii inamfanya Mungu kuwabariki na ndiyo maana wana idadi kubwa ya watumishi (wahubiri) kuliko nchi nyingine yoyote (ukilinganisha na hapa kwetu).

Ngoja nitoe mfano halisi, hapa nchini Tanzania, mkoa wa Mbeya ndiyo unaongoza kwa kuwa na watumishi (waimbaji na wahubiri) wengi na makanisa mengi zaidi kuliko mkoa mwingine wowote, vivyo hivyo kwa nchi ya Nigeria, hofu ya Mungu imewafanya kufika hapo.

2. Kuheshimu na kutunza watumishi wa Mungu. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia sana shuhuda za watumishi wa Mungu wa Afrika Magharibi, kila mmoja kwa nafasi yake ametoa ushuhuda wa namna watu wake walivyo barikiwa kwa kuheshimu “mpakwa mafuta” wa Mungu.

Mtumishi hana “stress” akiwa madhabahuni, hawazi atakula nini au atavaa nini maana wapo wanao jishughulisha kwa ajili yake. Maana yake nini?? Hii inampa nafasi mtumishi huyo kumtafuta Mungu kwa ajili ya watu wake lakini pia kuwa na “moyo mweupe” wenye kubariki siyo kunung’unika.

3. Watumishi kufundisha washirika kuhusu uchumi, utawala, uongozi na umuhimu wa mafanikio kwa mwamini. Hapa kuna siri nzito kidogo, Zaburi 24:1, Hagai 2:8 maandiko haya yana onyesha kuwa fedha, dhahabu na vitu vyote ni mali ya Bwana. Sisi tulio okoka ni wana wa Mungu hivyo tuna haki ya kumiliki na kutawala kama tulivyo barikiwa na Mungu, kwanini bado wengi ni masikini??

Watu wanafundishwa kuhusu kutubu na kwenda mbinguni, well and good. Lakini hizi mali huku duniani amiliki nani?? Tukubali kuwa watumwa?? Injili ni gharama, inahitaji fedha siyo maombi, kama hatujamiliki uchumi mkubwa, wahubiri watahubiri vipi??

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes