Headlines

BIBLIA ILITOKA WAPI

Biblia ilitoka wapi?

Kabla ya kuiamini na kuitumia Bibilia ni vizuri kujua tuliipokeaje au ilitoka wapi?
Neno Biblia ni neno la kigiriki "Biblos"

Baadae kidogo kidogo likabadilika "books of books" yaani kitabu cha vitabu, kitabu kinachojumuisha vitabu vingi.

Biblia ya kiprostestanti ina vitabu 66 kati ya hivyo 39 ni agano la kale na 27 ni agano jipya.

Biblia ya kikatoliki ina vitabu 72. leo sitaenda huko, ilikuwaje vitabu 72 na wengine 66.

Ilichukua karibu miaka 1600, kuandika Biblia. Ilianza kuandikwq miaka 1500 kabla ya Kristo kuzaliwa na ikaendelea miaka 100 baada ya Kristo kuzaliwa pale Mtume Yohana alipomaliza kazi katika kisima cha Patimo.

Biblia iliandikwa na kundi kubwa la watu waliochaguliwa. kulikuwa na watu 40 walioandika Biblia na walikuwa tofauti; wachungaji wa mifugo mpaka wafalme, wakulima mpaka manabii, wavuvi mpaka madaktari na mitume.N.K Ingawa mwandishi mkuu alikuwa Roho Mtakatifu ambaye ndiye aliyewavuvia wote.

Maandiko ya kale (original) yaliyoandikwa kwa mkono hayapo tena kwa sasa ingawa nakala za mwanzo zipo. Waandishi wa kiyahudi wa nyakati zile walifunzwa kuzinakili kwa uangalifu sana;
1. Walitamka kwa sauti
2. Walipaswa kusafisha kalamu zao kabla hawajaandika jina la Mungu mahali popote
3. Kabla ya kuandika Yehova walipaswa wajioshe kwanza wasije wakanajisika
4. Walipomaliza kuandika kazi kwa uangalifu walilinganisha na maandiko original  kama kulitokea kosa moja kwa moja, maandiko yote yaliharibiwa na walipaswa kuanza upya.
Unaweza kuona jinsi Mungu mwenyewe alivyosimamia uandishi wa maandiko na neno limekuja kwetu kama Mungu alivyokusudia.

- Haitoshi kusoma tu Biblia ni muhimu kujifunza, tafiti ambayo inahitaji nguvu nyingi kwa sababu;
1.Ni hazina kubwa mno. Zaburi 119:162, Ayubu 11:7-9 hazina haipatikani kirahisi lazima uichimbe

2.Utapata kama  Ayubu alivyosema hakuna ukomo ukichunguza kwa undani vitu vya Mungu

3. Neno la Mungu ni Hazina na kitu cha thamani kuliko vyote duniani

Kama nilivyosema Jumapili iliyopita kuna umuhimu mkubwa wa kufanya utafiti wa namna ya kutafsiri maandiko

1. Mwanzoni Biblia iliandikwa kwa lugha ya kiebrania, kigiriki, kialamaik. kuna lugha ya kisasa kwa siku za sasa kwa maneno mengine lugha hizo zimebadilika tofauti na awali

2. Muktadha wa utamaduni wa wakati ule wanaandika Biblia ni tofauti na sasa

3. Muktadha wa Jiografia ya Biblia wakati inaandikwa ni kitu kigeni kwa wakati wa sasa

4. Muktadha wa kihistoria wa nyakati zile ni tofauti na sasa

Changamoto hizo nne namna ya kuielewa Biblia ni kama gema ama pengo kubwa ambalo lipo kati ya waandishi wa Biblia na wanafunzi wa biblia au wanoisoma Biblia.

Kwa hiyo ili kuielewa Biblia lazima lijengwe daraja ili kuziba hilo gema au pengo hivyo inatupasa kujua namna ya kutafsiri Biblia.

Kutafsri ni kutafiti na kujua maana halisi ya mwandishi. Nawasikia watu wanasema kila mtu ana tafsiri yake ya Biblia.

Kuna vitu viwili ambavyo watu hawawezi kukubaliana navyo ni Dini na siasa kakini hii yote ni kwa sababu ya ufinyu wetu wa kulielewa neno la Mungu.

Biblia kila siku iko sahihi ni ufinyu wa uelewa wa mwanadamu ndio unaleta tofauti. kwa mfano kwa kutokuilewa Biblia wengine waliitumia kuhalalisha utumwa.

kule Marekani kwa mfano mwaka 1807 ilichapwa Biblia ya watumwa (Slave Bible) ambayo iliondoa baadhi ya maeneo ikiwemo kitabu cha kutoka kwani waliamini watumwa wakisoma watahamasika kutoroka au kuwa na fikra za uhasi. Mpaka sasa Biblia hiyo iko kwenye (Washingtons Museum of the Bible display)

Afrika Kusini Biblia ilitumika kutetea ubaguzi wa rangi N.K kama ambavyo leo watu wanatumia Biblia vibaya kwa maslahi yao kwa sababu ama kwa ujinga au kwa makusudi kinyume na malengo ya Biblia yenyewe.

Hebu  tuiendee Biblia kwa usahihi Biblia ina mamlaka na mara zote lazima iaminiwe. Biblia ina kanuni zake au sheria zake namna ya kutafsiri ikieleweka vizuri na ikatumika kwa usahihi italeta matokeo chanya katika maisha ya watu.

Maandiko yanatafsiri maandiko (General rule; scripture interprate scripture)

Kuna mambo ya msingi unapoiendea Biblia
Chunguza iendee biblia kama mchunguzi, hakuna ndani ya biblia kisicho na umuhimu. Usiache jiwe halijageuzwa.

Tafsiri(Interprates) Swali hapa hiki kifungu kina maana gani. kiendee kifungu kwa maswali ili upate majibu. kwa Mfano lazima ujiulize hii ilikuwa na maana gani kwa watu waliopokea mwanzoni?

Kwa nini alisema hivyo?
Hii inawezaje kufanya kazi wakati wa sasa?
Dhana kuu hapa ni ipi?

Lazima utafsiri maandiko katika Muktadha wa andiko lilivyotolewa.

Kusoma kwamba Biblia ndiyo Mamlaka yetu kuu haimainishi kuwa tuko sahihi wakati wote. Fikiria kwa mfano mashahidi wa Yehova au waumini wengine wanaodai kuyafuata maandiko, lakini bado wako kinyume sana katika baadhi mienendo yao.

Ni huduma ya Roho Mtakatifu inayomjenga mtu kuwa Mkiristu Mkweli, anayeutafuta muongozo wa Mungu, anayetazama vitu kwa mtazamo wa kimungu. Kwa hiyo, ni lazima tuokoke na tujazwe roho Mtakatifu ili tuweze kutafsiri kwa usahihi maandiko.

Inapotokea watu wawili au zaidi mnatofautiana katika tafsiri yenu ya maandiko, basi kila mmoja aachane na tafsiri yake ili kumcha Mungu. Eph. 5:21na kwa pamoja utafuteni ufunuo sahihi wa ukweli wa maandiko yake.

*Kanisa silo linaloelekeza nini Biblia ifundishe; Biblia ndiyo inayoelekeza nini Kanisa lifundishe*

Sababu na Mila vina mamlaka yenye nguvu lakini ni lazima vyote vitii mamlaka ya maandiko. Kunapokuwa na mgongano baina ya aina tatu za mamlaka (mila, sababu na maandiko), maandiko lazima yawe na mamlaka ya mwisho wakati wote.

*Kila kifungu cha maandiko kina maana moja ya msingi, tafsiri moja*

Mungu hakukusudia neno lake liwe na maana nyingi, bali maana moja tu iliyodhahiri kabisa. Mattayo 5:17-18 na Wagalatia 3:16

Kumbuka hata hivyo kifungu cha maandiko kinaweza kuwa na matumizi zaidi ya moja. Mfano 2 Wakorinto 6:14

*Maandiko ni sharti yachukuliwe kwa uhalisia kadri inavyowezekana*

Hakuna mwandishi wa habari ambaye angependa kuandika kuhusu baa la njaa na mateso yanayoisibu nchi kama India halafu habari yake itafsiriwe kuwa njaa kubwa itawafika watu wa India. Lakini hivi ndivyo watu wengi wanavyotafsiri neno la Mungu. Wakati 1 Wakorinto.15 inapozungumzia kufufuliwa kutoka katika wafu - husema *Hapana, hiyo inamaanisha ufufuo wa kiroho*. Vivyo hivyo hata kurudi kwa Bwana Yesu, baadhi husema *Hapana, Yesu amesharudi, ndani ya walio wake*, n.k

*Yatafsirini Maandiko kwa kuzingatia maana yake halisi (ile maana iliyokusudiwa wakati yanaandikwa*

1) Luka 15:8-10. Mfano wa Sarafu Iliyopotea. Mwanzoni ingeonekana hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya kalamu kwasababu alishapata sarafu yake iliyopotea. Lakini ni muhimu kuzingatia kuwa sarafu hii ilikuwa na ina muunganiko muhimu sana kwa sarafu nyingine zilizokuwepo.

*Mifano inahitaji kutafsiriwa kwa Kanuni maalum*

1. Dhumuni la mifano iliyotumika katika Biblia ni kuweka msisitizo wa kufafanua ukweli mahsusi wa kiroho

2. Hatupaswi kuongeza chumvi juu ya kile kilichokusudiwa kusemwa. Ni hatari mno kuyapatia maandiko tafsiri kwa kuegemea kwenye lugha ya picha ya mifano pekee.

Baadhi ya miongozo muhimu katika kutafsiri mifano ya kibiblia ni:

a)Tambua dhumuni kuu la mfano.

b) Hakikisha unafafanua sehemu tofauti tofauti za mfano kwa kulingana na msingi wake

C)Tumia sehemu kuu tuu za mfano kupata hitimisho la maana au funzo kuu la huo mfano. Katika mfano huu mtu anaweza kusema *mafuta na mvinyo* katika aya 34 inamaanisha *roho na damu* mambo mawili muhimu kwa uokozi. Lakini hii ni kwenda mbali kupindukia na dhumuni kusudiwa la mfano huo.

Ni vizuri unaposoma vitabu ndani ya  Bibilia ukajiuliza maswali mhimu na ya msingi sana
 Lini iliandikwa? Kujua watu waliishije wakati huo ,
Nani aliandika? Kumjua mwandishi na mahusiano yake na Mungu wakati anaandika.
Aliandika kwa nani? Aliowaandikia walimuwlewaje?
Kwa nini aliandika ? Kulikuwa na shida gani?
Jibu lake linawezaje kutumika na  kutusaidia katika Ulimwengu wa sasa?
 Kwa sababu nimesema hapo awali Kuwa Bibilia ni KITABU cha vitabu hivyo basi unapaswa kujua Kuwa

Muktadha wa msitari katika Bibilia ni kifungu, muktadha wa kifungu ni kitabu, kwa mfano kama unasoma kitabu cha “ Wagalatia” muktadha wa wa kitabu ni agano , na muktadha wa agano ni Bibilia nzima.
 Ngoja nifafanue vizuri
Ili uelewe msitari katika bibilia lazima uelewe kifungu , (kumbuka kifungu hapa sio ile tunaita milango) kifungu kinaweza Kuwa zaidi ya milango kwa mfano kifungu cha hotuba ya Mlimani kinaanzia mlango wa tano mpka wa saba. Na ili uelewe kifungu lazima usome kitabu , na ili uelewe kitabu lazima ujue muktadha wa agano kama ni la kale au agano jipya.
Kwa maneno mengine mstari mmoja kwenye Bibilia hauwezi kuamua bibilia inasema nini, Bali Bibilia inaamua mstari unasema nini!
Na ili Haya yaeleweke lazima kuzielewa kanuni za namna ya kuiendea bibilia.
0672870833
EV.MCHOME
✝️🔯

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes