Headlines

Hatua za maisha


Hatua za maisha
1. Hatua ya kwanza ni hatua ya kujifunza. Hii inategemewa kuangukia kati ya Siku ya kwanza ya maisha yako mpaka Miaka ishirini na tano.  0-25 ni hatua unayotegemewa kujifunza mambo yote yahusuyo maisha, na uwe umepata sifa zote kwa ajili ya hatua inayofuata katika maisha

Unapaswa uwe umeunganika na Mungu
Unapaswa uwe umepevuka na kujua mambo ya Msingi kuhusu maisha
Unategemewa uwe umemaliza mfumo rasmi wa elimu na uwe mhitimu, au uelewa unaozidi mfumo rasmi wa Elimu.
Unapaswa uwe umejua maono na Makusudi ya kuwepo kwako katika maisha.
Unapaswa uwe tayari kwa ukamilifu wa hatua inayofuata.

Kama kwenye Miaka ishirini na tano Hauna maono Wala makusudi ya maisha yako, eti  Bado unasubiri kujiunga na Chuo,au chuo kikuu, Hauna taaluma au ujuzi au hujatambua Kipawa au karama yako, na kujua uwezo wa utendaji wako.
Ujue unaendesha maisha yako Nyuma ya ratiba, unapaswa kuepuka vipingamizi na uongeze mwendo,
Nimeona watu amabo wako zaidi ya Miaka ishrini na tano Bado wanajaribu Kuhangaika kujiunga na chuo kikuu huku wakidhani wanao muda wote wa dunia.

Usichezee muda na maisha yako na kuharibu maisha yako ya baadaye. Hebu uwe makini na mwenye kutaka kufanikiwa. Na ukitoka hatua hii bila kumjua Mungu unaweza kupata changamoto sana hatu inayofuata.

2. Hatua ya pili ni hatua ya kupata. Hii ni hatua inayoangukia kati ya miaka ishirini na tano mpaka miaka hamsini. Hii ni hatua unayotegemewa uwe unakipato, katika umri huu unapaswa uwe unafanyia Kazi yale uliyojifunza hatua ya nyuma yaani ile hatua ya kwanza. Unategemewa uwe unapata matunda.

Unategemewa uwe na shauku na kuishi kwa ajili ya Mungu
Unategemewa kuwa utakuwa umeoa au kuolewa
Unategemewa uwe mzazi na kukuza watoto
Unategemewa kutumia ujuzi wa kifedha vizuri ili maisha yako ya uzeeni yawe salama
Unategemewa kwa kiwango cha juu kuwa maisha yako yawe na tija kwako na Jamii kwa ujumla.

Kama katika hatua hii Bado unahangaika kutafuta degree au taaluma, au unachukulia maisha kimchezo mchezo. Utakuwa unaishi chini ya Kiwango na utakuwa uko nyuma ya wakati.

Ukioa au kuolewa ukiwa na umri wa Miaka arobaini ni lini utaanza kuwatunza hao watoto na kuwasomesha?
Unataka uwe unabadilisha nepi au diapers ukiwa na umri wa Miaka sitini? Na kupeleka watoto shule?
Ipate hii vizuri.
Mzaliwa wako wa mwisho ukijumlisha Miaka ishirini au therathini ni muda wa kuwa huru. Kama Mtoto wako wa mwisho jumlisha ishirini au therathini kwenye umri wako, huo ndio muda ambao hupaswi kuhangaika na maswala ya ada.`
Umri huu Kama bado hujamjua Mungu utakuwa umeishi maisha yasio na maana na umeyapoteza.

3. Hatua ya Tatu ni hatua ya kugeuka , ni hii inaangukia kati ya Miaka hamsini mpaka sabini na tano. Na kuendelea inategemeana ni Miaka mingapi utaishi.
Unategemewa katika umri huu uko imara kiuchumi na umetulia, huu ni wakati unaogeuka unaanza kufundisha na kulea kizazi kinachofuata kwa uwezo wako na uzoefu .
 Umri huu sio wa kulea vichanga
Umri huu sio wa kutafuta Kazi au taaluma
Hupaswi kuwa darasani katika umri , labda kwa kujifurahisha tu.
Hupaswi kuwa hujaoa au kuoelewa katika umri huu vinginevyo uwe umeamua kuto kuoa au kuolewa.
Hupaswi kuwa maskini katika umri huu.
Hupaswi kuwa umepanga katika umri huu.
Hupaswi kuwa adui wa Mungu katika umri huu, vinginevyo utakufa na Kutengwa na Mungu milele na maisha yako yote yanakuwa hayana maana.

Sijui unaangukia wapi katika hatua hizi za maisha , ni matarajio yangu utagundua umhimu wa kupanga maisha yako ili Siku za baadaye au uzeeni usisumbuke.

Narudia tena hakuna anayeweza kukupangia maisha kwa ajili ya siku za baadaye Kama huwezi kupanga mwenyewe.

Ewe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!
Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,
 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?
Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi
Mithali 6:6-11

Bila kuwa na mipango kutakuwa na umaskini
EV.MCHOME
0672870833
✝️🔯

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes