Headlines

Usiseme kauli hizi

BAADHI YA KAULI UNAZOPASWA KUZIEPUKA ,UNAPOKUWA UMEUMIZWA NA KUJERUHIWA  MOYO WAKO.

1.U SISEME,  "Sitaoa/Kuolewa tena " Maana katika Maisha ndoa inayo nafasi yake kukusaidia kutimiza ndoto za Maisha yako, ndiyo Maana Mungu akasema "Si Vyema mtu awe peke yake, NA wawili ni bora kuliko mmoja ," kuoa /Kuolewa ni nguzo Muhimu inayoshikilia Maono yako.

2.USISEME,  "Hautamsaidia tena Mtu ",Kwa sababu uliowasaidia wamekujeruhi. Kwa sababu wapo watu wema  NA wenye fadhili  wanaouhitaji msaada wako ambao MUNGU ANAUPITISHA MAISHANI MWAKO UWEZE KUWAFIKIA HUKO WALIPO, KUWAFUNGIA MLANGO NI SAWA NA KUWAFUNGIA MUNGU MLANGO KUWA  ASIPITISHE VITU KWAKO.

3. USISEME , "Sitasamehe" ,Maana Mbinguni hauwezi kuingia kama haujamsamehe mtu, Mbona Mungu amekusemehe dhambi zako tena nyekundu sana, na pia  kutokusamehe kunamfanya MUNGU AKUFUNGIE MLANGO YA MBINGUNI UUPATE UZIMA NA MAFANIKIO.

4.USISEME,  "Utakufa/ Umeumbiwa mabaya tu " ,Hata kama iweje usijitamkie kifo au mambo mabaya,  Kwa sababu  MANENO YA KINYWA CHAKO  YATAKUFUNGA NA IPO SIKU YATATIMIA.

5.USISEME, "Nitalipiza kisasi " Kwa sababu  kisasi huwa analipa Mungu Tu, wewe kutaka kulipa kisasi nikumwingilia Mungu majukumu yake, MUNGU AKIKULIPIA NDIYE ATAKAYE KULIPIA VIZURI  NA KIKAMILIFU KULIKO WEWE UKILIPA.

6.USISEME, "Namwombea yamkute mabaya", Maana imeandikwa, msichoke kutenda mema na waombeeni adui zenu, NA WEWE KAMA MKRISTO WA KWELI, LAZIMA UJIFUNZE KUISHI MAISHA YA ZIADA, Yatakayo mfanya mkosaji ajue kosa lake kwa wema wako  na aseme ,hakika  una Mungu .Ushinde ubaya Kwa Kutenda Mema.

7.USISEME,  "Sitapenda tena ", Maana si kila mwanadamu ni mjeruhi /mkatili  kama huyo aliye kujeruhi, cha msingi kaa Magotini, MUNGU ATAKUPA ATAKAYE KUPENDA,NA UTAKAYE MPENDA KAMA KRISTO  ALIVYOLIPENDA KANISA. 
EV.MCHOME
0672870833

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes