Headlines

Imani mpate Yesu na kile alicho nacho ukipate


Imani ni nini? Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo, imani inatenda kupitia Tumaini kama unalo Tumaini ni rahisi sana kuipata Imani.
Unapaswa kufahamu kuwa imani ni Roho iliyo umba dunia, kama unayo imani unaweza kuumba chochote kile hapa duniani na kikawa.

Marko 9:22 “Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia.”

Ni vyema kumpokea Yesu na kuwa na kile alichonacho, mfano kuwa na nguvu za kuponya, waamini wengi wamempokea Yesu lakini hawana kile Yesu alichonacho.

Wokovu ni uhusiano, je unaupataje huo wokovu? Ni kwa wewe kutunza uhusiano kati yako na mwana wa Mungu aliye hai na si kutunza uhusiano wako na Mungu kwa sababu hata ibilisi anaweza kufanya hivyo, ibilisi anaweza kumsikia Mungu lakini hawezi kumsikia Yesu.
Yesu hawezi kutembea pamoja na ibilisi lakini Mungu anaweza na ndiyo sababu ukisoma Biblia maeneo mengi utaona Mungu akimuuliza ibilisi unatoka wapi? Naye anajibu “nimetoka huku na kule” na ndipo Mungu kama anataka kumnyoosha mtu anamuagiza, hii inamaana kuwa ibilisi ni mtumishi mwaminifu sana kwa Mungu lakini si mtumishi wa Yesu sasa kwa sisi ili tuweze kumshinda inatubidi tujiunganishe kwa Yesu.

Wana wa Israel walimwabudu Mungu na walimheshimu Mungu lakini walimdharau Yesu matokeo yake wakakosea. Mpate Yesu na upate kile Yesu alichonacho ili uweze kusaidia wengine.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes