Headlines

TAMBUA DALILI ZA KIBURI


*KIBURI* ni kati ya tabia ngumu sana kujigundua kama unayo au la.

Na kwa sababu ya ugumu wa kujigundua, ndio maana imeliza watu wengi

*Naweka hapa mambo kadhaa TUJIPIME SOTE KAMA TUNA DALILI ZA KIBURI AU LA:-*

*1. UKIONA, KILA UKIONYWA UNAKASIRIKA NA KUNUNA AU KUSUSA, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.*

- Yaani unaona karipio au onyo badala ya kuona tatizo lako, au hata ukiona tatizo lako huwezi kujizuia KUKASIRIKA AU KUNUNA UKIONYWA.

*2. UKIONA, KILA MKIKOSANA NA MTU, HUONI KOSA LAKO, UNAONA MAKOSA YA MWINGINE TU, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.*

- Kiburi siku zote NI KIDOLE KUKUONYESHA KOSA LA MWINGINE.

- Nilichojifunza, kwenye kila kwenye wawili au zaidi kukosana na kutokuelewana, kila mmoja ana mahali pa kujirekebisha, hakuna asiye na jambo la kujirekebisha

*3. UKIONA, KILA UNALOFANYA, UNATAKA KUJILINGANISH NA WENGINE, AU KILA WANACHOFANYA UNAJILINGANISHA NAO, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.*
- Kiburi siku zote KINATAKA WEWE UJIONE UKO JUU YA WENGINE....
Wewe mzuri zaidi ya wengine... Msomi zidi ya... Una pesa zaidi ya... Unafundisha zaidi ya... Unahubiri zaidi ya... Unaomba zaidi ya..._

_Siku zote "Wahesabu wengine kuwa bora..." :_

_*4. UKIONA, KILA UNALOFANYA UNAFANYA KWA LENGO LA KUSHINDANA.* :_

- _Unafanya jambo zuri ndio, lakini Adhma (Motive) yako ni mashindano, hata kama hujasema hivyo..._

_Unafanya ili kumshinda fulani hata kama fulani hajui, yaani utoshelevu wako wa ndani sio kutimiza jambo fulani, bali ni kugundua KWA KUTIMIZA HILO UMEMSHINDA FULANI_

_*5. UKIONA, UNAPENDA KUSIFIWA KWA KILA UNALOFANYA, kwa lugha nyingine kuwa RECOGNIZED AND APPRECIATED.*_

- _Kutambulika na kushukuriwa (to be recognized and appreciated) si jambo baya kabisa, lakini ukiona ukikosa hicho kitu unakosa amani kabisa na unatumia gharama yoyote utambulike na kushukuriwa, HICHO NI KIBURI KINAKUSUKUMA. ::_

_6. UKIONA, KILA ZURI UNALOLIFANYA SIRINI, UNATAKA LIJULIKANE NA WATU HATA KAMA SI MUHIMU KWAO na si kwa lengo la KUJIFUNZA, hiyo ni dalili ya KIBURI.*_

_Ukiomba, hauridhiki mpaka watu wajue uliomba, UKIFUNGA, mpaka watu wajue ulifunga au huwa unafunga, UKIFANYA JAMBO ZURI KWA MUNGU WAKO, mpaka watu wajue ndio unasikia kuridhika... Kinachokusukuma ndani ni KIBURI._

_*. UKIONA, HAUKO HURU(COMFORTABLE) KABISA KUTUMIA LUGHA YA PAMOJA(tuta.., tume..) UNAPENDA ZAIDI KUTUMIA LUGHA YA BINAFSI (Nita.., nime.. ) UNAPOONGELEA MAMBO AU UMILIKI WA VITU, hiyo yaweza kuwa dalili ya KIBURI.*_

_Hupendi kutumia lugha kama, vitu vyetu, jambo letu, huduma yetu... Sisi... nk, unapoongelea jambo ambalo na wengine wana mchango hata kama ni mdogo sana, hasa kama mwewe ni muanzilishi wa jambo au una mchango mkubwa juu ya jambo._

_Kumbuka *"KIBURI HUTANGULIA ANGUKO"*_

_Lakini pia, *"KIBURI HUTANGULIA MAUTI"*_

Nukta..
0672870833 kwa maombi na maombezi

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes