Headlines

Thamani ya Muda


THAMANI YA MUDA .

Muda ni Mali.
Ukiweza kuutumia muda wako vizuri hasa katika mambo ya Mungu, hautaacha kuwa mkuu hata kama mizimu ya Kwenu inakataa.

Kila MTU ana masaa 24 Kwa siku. Haya masaa lazima uyapangilie.

Katika haya masaa 24 kuna masaa 2 na dakika 40 ambayo ni zaka ya Mungu.

Kama ujuavyo, unapohesabu moja mpaka tisa, ya kumi ni ya Mungu.

Ndiyo maana siku ya mwisho hautaweza kujitetea Kwa kusema kwamba haukuwa na muda wa kumwabudu Mungu au kumtumikia.

Kihalisia kabla ya nyongeza ya muda wowote, una masaa 2:40 ambayo hautakiwa kuyatumia Kwa lolote na ni Kwa kila siku. Haya masaa ni maalumu Sana Kwa ajili ya mambo ya Mungu pekeee yake.

Mpendwa wangu:
Muda ukipotea, hauwezi kusema utaurudisha, ndiyo maana neno linasema tufanye mambo yetu Kwa kuukomboa WAKATI maana hizi ni zama za uovu.

Shetani alipoteza nafasi ya kumwabudu Mungu Kwa sababu ya ulevi wa madaraka. Mpaka SASA hajawahi kuipata tena.

Neno linasema ndani yake kilionekana kiburi, kujisikia, kudharau sauti ya Mungu kama ambavyo hata wewe usipojiangalia ndiko unakoelekea.

Kabla ya kuolewa ulikuwa mwimbaji, mwanamaombi na mkeshaji mzuri. Baada ya ndoa, umebweteka maana unafikiri ulishapata unachotaka na hauhitaji tena kuomba.

Ndugu, kama mumeo ulimpata Kwa maombi, inabidi umshikilie Kwa maombi. Kilichozaliwa Kwa mwili ni mwili, kilichozaliwa Kwa Roho ni roho, kadhalika kilichozaliwa Kwa maombi kinatunzwa na kulindwa Kwa maombi.

Zamani kabla ya hicho cheo na hiyo kazi uliyonayo, uliheshimu watumishi wa Mungu. Na uliamini ni wajumbe wa Mungu na wamewekwa na Mungu mbele yako ili wakupe mwongozo wa namna au jinsi ya wewe kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

Ila siku hizi, Kwa kuwa hawana nyumba kama yako, hawana gari kama wewe, yamkini hata ndege hawajapanda, na Kwa kuwa wewe unazipanda kila siku hauna muda nao tena na wala maombi yao kwako si kitu.

Nimetumwa nikuambie, fanya yote lakini usiutumie muda wa Mungu katika mambo yako binafsi.

Ni dhambi Kwa mkristo kama wewe, kukosa muda wa ibada kila siku. Nimekuonesha kwamba una masaa mawili na dakika arobaini ya kumwabudu na kumtumikia Mungu kila siku.

Unakumbuka mara ya mwisho ulipowahi kanisani na kudeki kanisa, ulipowahi na kupanga viti vya ibada, unakumbuka mara ya mwisho ulishiriki lini kubadili mwonekano wa nyumba ya ibada Kwa kununua viti au mapambo ya kisasa?

Kama Mungu anaheshimu muda wako wa kazi, mbona wewe hauheshimu muda wake wa ibada.

Wachungaji Mungu awatie nguvu, tuna waumini ambao miezi sita au saba hajafika kanisani na bado anakuita mchungaji wake, sadaka hatoi wala mafungu ya kumi ili yaendelezee kazi ya Mungu na kumfanya aonekane muumini hai.

MTU huyu huyu alipokuwa Hana kazi, ulitenga muda WA kumwombea, kumshauri ili asipate msongo wa mawazo huku ukimwambia kwamba Mungu atamtokea siku moja na kweli Mungu akamtokea.

Ila leo badaa ya hiyo Neema, simu za mchungaji hapokei, wala meseji za mchungaji hajibu tena. Anatangaza Kwa watu kwamba ni Mungu aliyempa hicho alichonacho Jambo ambalo ni kweli,lakini Mungu amekupa kupitia Kwa mtumishi wake aliyemweka mbele yako

Nawahimiza wana wa Mungu. Kama unataka kupona, kufunguliwa na kuwekwa huru mbali na vifungo vya Yule mwovu, thamini muda wa Mungu.

Msikilize mchungaji aliyewekwa mbele yako.

Wengine kama siyo maombi ya watumishi wa Mungu, usingekuwa kwenye hiyo ndoa. Mara ngapi ulitaka kuondoka ili mchungaji akakusihi ubaki Kwa maombi na machozi mengi?

Kama Mungu amekuhurumia na kukupa kazi, ndoa, isitoshe na zawadi ya watoto juu, unashindwaje kumwabudu Kwa moyo wako wote, Kwa Mali zako na vyote alivyokupa?

Usisahau, ulizaliwa uchi wengine wakakivalisha ukiwa haujitambui.

Mungu anakutaka madhabahuni.

Mungu anataka umtumikie.

Punguza kujitetea na kutafuta sababu ya kutomtumikia Mungu eti kisa wewe siyo pastor. Katika nafasi hiyo hiyo uliyonayo, unatazamiwa uzae matunda.

Mchungaji wako ana upako, ila Kwa sababu haonekani kwenye TV au hasikikii rwdioni unafikiri Hana neno.

Kabla ukimbilie huko kwa wenye TV ni yeye aliyekuombea ukapona ule ugonjwa, kazi yako ilitokana na maombi yake. Na kama TV ndo upako na nguvu za Mungu kamlipie kipindi Star TV au TV yoyote na ikibidi umnunulie yake uone,

Utagundua kwamba ana Neema kubwa kuliko unavyofikiria.

Narudia tena.
Mungu anataka REHEMA na si sadaka.
Anataka moyo wa ibada.
Anakutaka madhabahuni.
Anakuita madhabahuni.
Anataka kukuona madhabahuni.
Muda unao, amua sasa kuuelekeza kwenye mambo ya Mungu ili na yeye akuelekezee baraka zake.

#EV.MCHOME# 0672870822
Mtumwa wa Yesu Kristo Kwa kanisa na Taifa.
#Madhabahu Isiyoshindwa#

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes