Home >Unlabelled >
By Yote Yanawezekana Kwa Yesu • November 08, 2019 • • Comments : 0
Tahadhari...
SIKU UKIANZA KUFIKIRI KWAMBA KAZI YA MUNGU INAKUTEGEMEA WEWE AU KUFIKIRI KWAMBA KAZI YA MUNGU HAITAFANIKIWA BILA NGUVU YAKO; HAPO UJUE TAYARI KIBURI KIMESHAANZA NDANI YAKO...
KUMBUKA: Kumtumikia Mungu ni fursa; Lakini hata bila wewe kazi ya MUNGU haiwezi kukwama.
MUNGU ANAO WATUMISHI WENGI...Na ukileta mgomo, kiburi au majivuno, MUNGU atakuondoa na kuweka mwingine.
JIFUNZE TOKA KWA NABII ELIYA MTISHBI... aliamini kwamba ni yeye tu aliyebakia ndani ya Taifa la Israel. Lakini Mungu akamwambia kwamba wapo wengine kama yeye 7000!!
Matokeo yake MUNGU akainua watu wengine wachukue nafasi ya ELIYA; yaani NABII ELISHA na YEHU; Kisha ELIYA akatwaliwa!
1 WAFALME 19:16-18; “Naye Yehu, mwana wa Nimshi, mpake mafuta awe mfalme wa Israeli. Elisha, mwana wa Shafati, wa Abel-mehola, utampaka mafuta awe NABII MAHALI PAKO. Basi, yeyote atakayenusurika upanga wa Hazaeli, Yehu atamuua, na yeyote atakayenusurika upanga wa Yehu, Elisha atamuua. Lakini, nitaacha hai watu 7,000 nchini Israeli, ambao hawajamwinamia Baali, wala kuibusu sanamu yake.”
MTUMIKIE MUNGU KWA UNYENYEKEVU MKUBWA; KAMWE USIFIKIRI BILA WEWE KAZI ITASIMAMA.
By the way, ELISHA ALIFANYA MAMBO MAKUBWA ZAIDI YA ELIYA...!!!
Share
Maombi na maombezi
0672870833
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment