SOMO: Ufunuo Wa Ndoto Na Tafsiri Zake
Zifuatazo ni aina za ndoto na tafsiri zake. Angalia aina ya ndoto umeota halafu, tafuta na uangalie tafsiri zake katika ukurasa huu wa kitabu hiki;
Aina Ya Ndoto Ufunuo na Tafsiri Yake
Ukiota unafukuzwa na mbwa Unafuatiliwa na roho za uzinzi
Ukiota unafunga harusi Unafuatiliwa na roho za mauti
Ukiota uko ndani ya maji mengi Magomvi na machafuko yanakufuatilia
Ukiota unawaona watu waliokufa zamani Ujue unafuatiliwa na mizimu
Ukiota umelala juu ya kitanda kichafu sana Unashambuliwa au unafatiliwa na mawazo machafu na fikra mbaya
Ukiona mti Umeona mtu mkuu
Ukiona miti Ni watu wengi
Ukiona paka Ni roho za uchawi
Ukiona kuku mbele yako Ni ujumbe kwamba acha kutoa siri zako
Ukiona bata Ni ujumbe kwamba acha kujikanyaga ovyoovyo
Ukiona kobe Unaelezwa na Mungu uache kiburi
Ukiona majani mabichi Umeona ustawi wako
Ukiona mbegu Ujue kuwa Mungu anataka uzingatie neno lake
Ukiona muhuri wa ofisi Mungu amekuthibitisha
Ukiona mnyama chui Mungu anakueleza kuwa ndani yako unayo hasira ya kipepo
Ukiona umevaa gunia Mungu anataka ufanye toba
Ukiona uko uchi Ujue makosa yako yamejulikana
Ukiona mnyama simba mbele yako au nyuma yako Ujue roho za vitisho au kukutishia mambo Fulani zinakufuatilia
Ukiona mnyama tembo Ujue kiongozi wako atakuonea na kukunyanyasa maeneo Fulani
Ukimwona mnyama twiga Ujue wewe ni mtu unayependa kusifiwa sana na watu
Ukiona ndege aina ya njiwa Roho Mtakatifu
Ukiona jicho au macho Mungu anakuambia kuwa yuko pamoja na wewe
Ukiona kitabu Umepewa neno la uzima
Ukiona mkono Uponyaji umekujilia
Ukiona samaki Umeona watu
Ukiona mlima Utapata majaribu
Ukiona bonde Ujue shetani anakuwinda akuangushe katika wokovu
Ukiona nyumba Utakutana na mtu mkubwa mwenye uwezo wa kifedha
Ukona bahari Hali ya machafuko inakuwinda
Ukiona kisima mbele yako Ujue umepata mahali ambapo utasaidika au makimbilio salama
Ukiona unakula asali Ni wakati wa kupata mambo yatakayo kuletea furaha, na mambo magumu yameisha sasa
Ukiona jangwa mbele yako Kipindi cha ukame kinakuja mbele yako.
Ukiona malaika Ujumbe wako unakuja
Ukiona uko miguu mitupu Ndani yako hakuna utayari
Ukiona mawimbi ya bahari Uharibifu unakufuatilia
Ukiona unaoga maji Ujue umetakaswa
Ukiona umevaa nguo nzuri sana Mungu ameamua kukuheshimu
Ukiona unaogelea baharini au mtoni Jaribu ulilonalo halitakuweza
Ukiona unavuka mto Utashinda majaribu au vikwazo
Ukiona majani mengi yameota Uharibifu umekusudiwa dhidi yako
Ukiona unaendeshwa katika pikipiki au baiskeli Weka nyumba yako vizuri
Ukiona giza mbele yako Ujue wewe ni mtu usiye eleweka mbele za Mungu
Ukiona majengo ya shule Ujue Mungu mwenyewe atakufundisha
Ukiona umebeba samaki Ujue utawasaidia kifedha watumishi
Ukiona upinde wa mvua angani Mungu amekukumbuka
Ukiona unakimbizwa na nyoka Shetani anakuwinda
Ukiona umevaa nguo ya ndani tu Ujue unaelezwa ufiche siri zako
Ukiona unafukuzwa baadaye ukapanda juu ya mti. Inatakiwa tatizo ulilonalo umshirikishe mwingine
Ukiona kofia Wokovu wako unatambulika
Ukiona mvua inanyesha Utaingia mahali pa chakula tele
Ukiona nyoka juu ya mti Ujue kuwa shetani atatumia mtu kupambana na wewe
Ukiona umepanda basi Unatakiwa uwe na umoja na wenzako
Ukiona ndege ya abiria inaruka Ujue kuwa jambo lile unalolitafakari sana litadumu
Ukiona ndege ya abiria inatua Ni ishara kusema; jambo ulilokuwa unalitafakari limefika mwisho
Ukiona samaki wameoza Waumini wameanguka dhambini
Ukiona umevaa viatu Umepata utayari wa utumishi
Ukiona unajisaidia haja kubwa Mawazo yako machafu yametoka
Ukiona ngamia mbele yako Unatakiwa uwe mvumilivu
Ukiona umevaa sidiria peke yake Ujue BWANA ameliona hitaji lako la kuolewa na atakufungulia mlango
Ukiona unakunywa maziwa Unatakiwa ushike mausia
Ukiona nyumba imeanguka Ujue tegemeo lako limeharibika
Ukimwona Rais wa nchi Ujue kuwa BWANA atakupa haki yako unayoitafuta
Ukiota unafukuza panya Wokovu wako umeingia kasoro
Ukiota umeshika bendera Umeshinda na umefanikiwa
Ukiota unapanda ngazi Kipawa chako kimeinuka
Ukiota umekaa mezani Umeandaliwa mema
Ukiona samaki mkubwa Mtu mkubwa ataokoka
Ukiona unafundisha Ujue umethibitika katika ualimu
Ukiona barabara ya lami Wakati wako wa kufanikiwa umefika
Ukiota unawaona wazee wameketi Ujue umepewa kipawa cha hekima
Ukiota mawingu yanakufunukia Ujue Mungu amekukubali
Ukiona kabati kubwa Ujue wewe ni wakili wa siri ufalme wa mbinguni
Ukiona uko shimoni Umefungwa na vifungo vya kichawi
Ukiona uko shimoni na unashushiwa kamba ili uokolewe Ujue wakati wako wa kufunguliwa na kuwekwa huru umewadia
EV.MCHOME
0672870833
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment