Headlines

Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja la kuvukia!

Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja la kuvukia!
"Matatizo ni alama ya mkato, matatizo ni fursa zenye miiba, matatizo ni changamoto, matatizo ni ufunguo wa maisha, matatizo ni giza la kusaidia kuona nyota, matatizo ni mawe ya kuvukia, matatizo ni mtihani, matatizo ni msalaba, matatizo ni mawimbi katika bahari, matatizo ni mtazamo, matatizo ni ujumbe, matatizo ni mwisho wa sura si mwisho wa kitabu, matatizo ni weusi ulioko nyuma mbele kweupe, matatizo ni sumaku inayokuvuta uwe karibu na Mungu, matatizo ni mapito, matatizo ni matuta katika bara bara kuu ya maisha, matatizo ni ufunuo wa uwepo wa Mungu, matatizo ni somo, matatizo ni masahihisho, ni kinga, ni ishara ya uhai" ni maneno yenye kila aina ya busara, elimu na mafunzo katika kitabu kiitwacho, "Matatizo si Tatizo Matatizo ni Daraja"kimechoandikwa na Fr. Faustin Kamugisha, mkuu wa SAUT Songea.
Wakati wewe unaendelea kulialia na matatizo lukuki uliyonayo, wenzako wanafanya matatizo hayo kuwa fursa na kuvunja rekodi maishani. Watu walimshangaa mtu mmoja akitokea gerezani na lundo la karatasi maarufu kama "Toilet Papers". Zilikuwa nyingi kiasi kwamba alipozipanga kwenda juu zilimzidi urefu. Karatasi ambazo zilitengeneza kitabu kiitwacho, "Shetani Msalabani" . Huyo si mwingine. Ni ni Ngugi wa Thiongo'o. Aliandika kitabu hicho akiwa gerezani. Ndiyo maana Fr. Kamugisha anakwambia matatizo ni fursa. Wakati wengine wakiwa gerezani wanawaza mbinu mpya za kuiba, wenye akili wanawaza namna ya kufaidika kutokana na kifungo.
Kama nchi tunapitia matatizo lukuki ambayo tukiyabadilisha na kuwa fursa, walahi Ulaya haita ona ndani kimaendeleo. Tunahitaji kuwa na mtazamo hasi kwa matatizo hasa ya kimfumo yanayowanyong'onyesha watanzania. Mtu mwenye mtazamo hasi ni mtu ambaye anafanya fursa zake ziwe matatizo na mtu mwenye mtazamo chanya ni mtu anayefanya matatizo yake yawe fursa amesema Fr. Kamugisha kupitia kitabu chake, uk. 13.
Unapovurunda katika kazi ulizoaminiwa, kubali kuwajibika na kuachana na kasumba ya kulalamika kwamba wamekuonea. Wakuonee ili iweje? La msingi hapa, rudi nyuma, tafakari kwa sauti kuu na ujue ulikosea wapi. Hivi karibuni Rais amefanya mabadiliko katika nafasi za ukuu wa wilaya, kunawalioondolewa kabisa. Sasa badala ya kujiuliza kwa nini wameondolewa, kunamabifu yameanza kujitokeza kwamba wamepigwa majungu. Kuondolewa katika uongozi ni ishara ni tatizo ambalo walengwa wote wanatakiwa walipokee katika mtazamo chanya na kutafakari kwa kina, kwa nini imekuwa hivyo.
Maisha ni changamoto. Changamoto ndizo zinazofanya maisha yavutie, kuzishinda ndiko kunakufanya maisha yawe na maana ameandika Fr. Kamugisha uk 15. Kupata changamoto ni sawa na kukalia msumari, huwezi kutulia lazima usimame ufanye kitu Fulani. Watanzania tumekalia misumari kwa muda mrefu, hebu sasa tuamke na tufanye kitu. Tusiwe kama vijana wanaokubali kutumika huku wakiendelea kukalia misumari. Kumbuka unapoona tatizo basi ujue suluhisho haliko mbali.
Matatizo ni giza la kukusaidia kuona nyota. Matumaini yetu yawe kama nywele na kucha.Haijalishi unazikata mara ngapi, haziachi kuota, ameandika Fr. Kamugisha uk 19 wa kitabu, "Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja". Vizuizi viko vingi lakini ni mwiko kukata tamaa. Askari watapiga mabomu sana, lakini chukua maji, nawa uso, endelea kudai haki yao. "Unaweza kulala chini na kufa, au unaweza kusimama na kupigana, lakini hakuna kurudi nyuma". Ili punje ya ngano iweze kuota, haina budi kuzikwa mpaka ioze alisema Ngugi wa Thiong'o kupitia riwaya yake ya "Grain of Wheat". Bila matatizo akili haiwezi kukomaa. Utabaki kubwa jinga. Huwa ni kiyakumbuka maneno ya Mch. Mpemba wa kanisa la kwa Neema Mwanza, nacheka sana, eti, ‘Kichwa kikubwa, macho makubwa, akili finyu".
Matatizo ni weusi ulioko nyuma, mbele ni kweupe, usikubali kurudi gizani (nyuma). Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Jifunze kusamehe na kusonga mbele. Kumbuka huwezi kuleta mabadiliko kwa takwimu za nyuma, alisema Mch. Msigwa, Mbunge machachari kutoka Iringa. Usiwe mpumbavu kama mwanamume mmoja kuongea hadharani kwamba mke wake akikonda sana kupitiliza anamrudisha nyumbani. Ili iweje?
Matatizo ni mawe ya kuvukia. Ukifanya kosa, litumie kama jiwe la kuvukia kwenda kwenye wazo jipya ambalo usingeligundua kama kungekuwepo na kosa ameandika Fr. Kamugisha uk 21 wa kitabu, "Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja".
Matatizo ni matuta katika barabara kuu ya maisha. "Njia ya kwenda kwenye mafanikio haikunyooka. Kunakona inayoitwa kushindwa, sura ya kitanzi inayoitwa kuchanganyikiwa, matuta ya kupunguza spidi yanayoitwa marafiki, taa nyekundu zinazoitwa adui, taa za kutoa onyo zinazoitwa familia, taili zenye pancha zinazoitwa zinazoitwa pancha, lakini ukiwa na tairi la akiba linaloitwa kupania kitu, na injini inayoitwa uvumilivu, dereva anayeitwa nguvu ya nia, utaweza kufika mahali panapotwa mafanikio" ni maneno kuntu kutoka kwa Fr. Kamugisha. Kwakweli padri kaandika.
Jamaa mmoja nyumba yake iliungua na kuteketea, badala ya kujiua, yeye akasema, "haya ni matuta ya kupunguza spidi kwenye barabara kuu ya maisha". Matatizo yanatupa nafasi ya kufikiri. Matatizo yanaimarisha ubongo. Matatizo ni mapumziko ya shughuli tunazozifanya. Matatizo ni kituo siyo alama ya nukta. Matatizo ni vituo vya kutufanya tutafakari na kuwa makini zaidi. Matokeo mabaya uliyoyapata kidato cha nne yasikufanye ujiue. Ni muda wa kujipanga upya. Kama dhamira yako ni kusoma, nenda karudie. Fr. Kamugisha anatupa mfano huu, uk. 49, " Mfanyabiashara mmoja aliweka maneno yafuatayo kwenye fremu ya duka lake na kila aliyekuja kwake na maneno ya kukata tamaa alimuonesha maneno hayo kwenye fremu na yalisomeka hivi, "Alishindwa katika biashara mwaka 1831. Alishindwa tena katika biashara mwaka 1833.. Alichaguliwa kuwa mmoja wa watunga sheria mwaka 1834. Mpendwa wake wa moyo, yaani mke wake aliaga dunia mwaka 1835. Alichanganyikikwa mwaka 1836. Alishindwa nafasi ya spika 1838. Alishindwa kuingia kwenye Congress mwaka 1848. Alishindwa kuchaguliwa kuwa Elector mwaka 1840. Alishindwa kuingia kwenye Congress mwaka 1843. Alishindwa kuingia kwenye Congress Mwaka 1848. Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1860. Jina chini ya rekodi hii ni Abraham Lincoln".
Picha tunayoipata hapa ni kwamba kila alipokuwa anakumbana na tatizo hakukata tama, aliendelea kuthubutu na mwisho wa siku akaibuka kuwa mshindi. Kumbe unapopata tatizo suluhisho siyo kujiua, bali kukaa chini na kupata muafaka.
Maneno yangu yangu yangekuwa ni sheria, basi kila mtanzania LAZIMA angesoma kitabu hiki na hakika kama nchi tungeona mabadiliko makuu katika kila sekta. Lakini basi kwa ridhaa yako nakushauri fanya juu chini ujisomee k

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes