Headlines

Entertainment

Fun & Fashion

International

Latest Updates

Mch.Eliona kimaro Kijitonyama

January 18, 2023

 

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama Dk Eliona Kimaro kupewa likizo, ibada ya asubuhi (Morning glory) imefanyika huku idadi ya waumini ikiwa ndogo tofauti na ilivyozoeleka.


Licha ya uchache huo wa waumini pia baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wamehakikisha ibada hiyo inafanyika kutokana na baadhi ya waumini kuzuia jana ibada ya jioni (evening glory) kufanyika baada ya kuandamana na mabango wakimtaka mchungaji wao Dk Kimaro.

Mapema jana Jumanne asubuhi, Januari 16, 2023 ilisambaa video katika mitandao ikimuonyesha mchungaji huyo akiwaeleza waumini wake kuwa amepewa likizo ya siku 60 baada ya kuitwa katika ofisi ya msaidizi wa askofu na kufanya kikao na mkuu wa Jimbo la Kaskazini.

"Semina yetu ni ya wiki mbili (Semina ya neno la Mungu), lakini niliitwa ofisi ya msaidizi wa askofu, tulikuwa na kikao na Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchungaji (Jacob) Mwangomola. Nimepewa barua ya likizo ya siku 60 kesho asubuhi (leo Jumatano) atahubiri Mchungaji Anna na ataendelea kuwa Mchungaji wenu," amenukuliwa kwenye video hiyo.

“Kwa mujibu wa barua nitarudi Machi 17 (2023) na sitakuja hapa, barua inanilekeza kuripoti Makao Makuu ya Dayosisi. Kwa hiyo mimi ni Mchungaji wa Lutherani nina heshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo na maadili…

“Pia kwa neema ya Mungu kwa sababu hiyo imenilazimu kutii na kwenda kwenye hiyo likizo na baadaye kuripoti kwenye ofisi ya askofu kama nilivyoelekezwa,” anasema Mchungaji Kimaro katika video hiyo.

Mbali ya video hiyo, ipo nyingine iliyosambaa ikiwaonyesha baadhi ya waumini wa usharika huo wakiangua vilio, wakati mchungaji huyo akifanya maombi ndani ya kanisa hilo wakati akiaga.

Mwananchi ilifika kanisani hapo leo Jumatano Januari 18, 2023 saa 12:25 asubuhi na kukuta ibada hiyo ikiendelea huku baadhi ya viongozi wakiwa kwenye lango kuu wakitaka kufahamu baadhi ya taarifa za waumini ikiwemo jumuiya anayosali na kama ana namba.

Hata hivyo, mmoja wa waumini ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, watu wamevunjika moyo kutokana na kilichofanyika haiwezekani mchungaji apewe likizo ya siku 60, wakati ndio mwanzo wa semina.

“Pamoja na kuwepo mgawanyiko kila mtu ana imani yake siyo wote waliokuja kusali hapa wanafurahishwa na kilichotokea, ndio maana hata viongozi wanajitahidi ibada hii isivurugike kama ile ya jioni watu ni wachache,”alisema muumini huyo.

Muumini mwingine Helleni Minja anayefanya biashara nje ya kanisa hilo amesema, asubuhi ni vigumu kuzuia ibada kutokana na watu wengi kwenda kazini lakini ibada ya jioni na Jumapili hazitafanyika hadi mwafaka upatikane.


Msimamo wa waumini

Jana baada ya kushindikana kufanyika kwa ibada ya jioni waumini hao walifanya kikao cha pamoja na kukubaliana kutoingia ndani ya Kanisa hilo hadi watakaporudishiwa Mchungaji wao Dk Kimaro.

Uamuzi huo ulifikiwa na waumini hao baada ya kukubaliana kukutana chini ya mti katika viwanja hivyo kila siku saa 11:00 jioni hadi pale mchungaji atakaporudishwa.

 "Tumesimama hapa kwa kuwa tuna maumivu yanayogonga mioyo yetu. Tuko hapa kwa kuwa hatujui kuhani wetu alipo,"alisema mmoja wa waumini.

Walisema utaratibu uliotumika kumsimamisha mchungaji huyo siyo sahihi kwani aliyemsimamisha alipaswa kufika usharikani hapo na kuwaeleza waumini kilichotokea.

Mateso

January 12, 2023

 Kwanini mateso yakupate

Magumu 

Yawe fungu lako?

Kushindwa kudharauliwa 

Kushushwa kuonewa!!!!

Ooooh 

Hayo yanakupata kwa sababu 

Mungu anataka umpe utukufu 

Mungu anataka kutukuzwa 

Kama hutapata magumu itakuwa ngumu kwako kumpa Mungu utukufu.

Sasa 

Dawa ni nini 

Ni 

Kumshukuru Mungu kwa kila jambo 

KUTOKWENDA NYUMBA ZA IBADA NI DALILI YA KUMWACHA MUNGU.

May 15, 2020
KUTOKWENDA NYUMBA ZA IBADA NI DALILI YA KUMWACHA MUNGU.
Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
Isaya 1:4

Taifa lenye dhambi
Ni watu wanao mkosea Mungu kwa mawazo
Maneno na matendo.
Watu hawa wanachukua mizigo ya uovu
Wanaikumbatia dhambi.
Uzao wa wana wao ni wakutenda mabaya.
#Kumwacha #Mungu #ni #dhambi
#Kuto #kwenda #nyumba #za #ibada #ni #DALILI #ya #kumwacha #Mungu.
Na
Nidalili ya kamdharau Muumba wako.
Na
Niishara humwamini Mungu wako unaye muomba kila siku .
Na
Niishara ya kufarakana na Mungu.
Na
Niishara ya kurudi Nyuma kiimani.

#Wakristo.
Sisi hatuongozwi na hali halisi.
#Sisi #tunaongozwa #na #NENO #LA #MUNGU.
Naamini katika Mungu hakuna
Linalo shindikana.
By
MWJ.WILLIAM S. MCHOME
MAN OF GOD
✝️🔯
May 12, 2020

Njaa inaweza
Kukuua hata kabla ya korona.
Huu
Msemo wa
Stay home huu
Unafanya watu kuwa wavivu
Wa kufanya kazi.
Wengine wakiwa
Wamejifungia.
Wengine
Wanapiga pesa za kufa mtu
Mtazame Mr.Jeff Bezos.
Mfanya biashara bilionea namba moja Duniani kwa sasa aliye kataa kujifungia ndani kisa korona.
Tangu janga hili lianze la korona utajiri wake unazidi Kupaa na kushikilia rekodi ya kuwa bilionea namba moja duniani
Why
Anatumia korona kama Fulsa na sio tatizo.
Huyu ni mwasisi wa AMAZON
biashara mtandaoni .
Ameajiri watu mara mbili ya mwanzo
Ameongeza muda wa kupiga kazi.
Anavuna pesaa.
Tu
Wewe unakufa na njaa kisa korona
Mwingine anatajirika kisa korona.
Kaa mkao
Tatizo ukiniona ni tatizo
Hakika litakutesa
Chukulia tatizo kama Fulsa
Litakuneemesha.
Korona ni tatizo
Lililobeba Fulsa
Tumia Fulsa katika tatizo
Utakuwa heri na mwenye mafanikio.
Usijifunze kwa wenye maneo mengi
Jifunze kwa wanao fanya mengi.
Malengo yako Wakuyapigania
Mpaka yatimie ni wewe mwenyewe.
Wakuua mipango yako
Sio korona
Bali ni Mungu
Usitishike .(chukua tahadhari)
Usikubali kukataa tamaa Simama
Tenaa
Kipekee utashindaaa na
Tutashinda.
By
Mwnj.WILLIAM S.MCHOME
MAN OF GOD
✝️🔯

Dawa ya Covid 19 korona na uchumi

May 11, 2020
MTOTO WA MUNGU 
upendwaye sanaaah.
Na Mungu.
Fahamu
COVID 19
Inaua
Ni gonjwa ambalo
Nyuma yake limebeba Roho ya Mauti.
Shida sio Gonjwa
Shida ni Roho ya mauti iliyo
Nyuma ya Gonjwa hili.
Muhimu ujue
Unapo
Ingia katika maombi
Pambana
Kukataa  *ROHO YA MAUTI*
pili
Tahadhari ni Muhimu
Lazima
Uvae barakoa
Nawa na sabuni vyema
Ukihisi umegusa maeneo
Hatarishi.
Usipeane Mikono na watu.
Usikumbatiane na mtu .
Tatu
Jipende
Mwenyewe
Jilinde utalinda na wengine.
Pia
Usisahau
*HOFU YA KORONA INAUA KULIKO KORONA YENYEWE*
simama kidete
Katika imani
Utauona
Mkono  wa
Mungu.
Cha mwisho
Mwj.william mchome nasema.
*kujifungia ndani na kuto kutoka njee kutafuta pesa kisa korona ni kualika njaa nyumbani*
*Toka kafanye kazi usiangamie kwa kukisa maarifa*
Hakikisha unachukua
Tahadhari.
Na maombi kwa
Mungu ndio
Silaha pekee
Amini katika Neno la Mungu
Hakika tutashinda.
By
*Mwj.William S.Mchome*
✝️🔯
*Injili kwa kila kiumbe*

May 09, 2020

Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja la kuvukia!

Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja la kuvukia!
"Matatizo ni alama ya mkato, matatizo ni fursa zenye miiba, matatizo ni changamoto, matatizo ni ufunguo wa maisha, matatizo ni giza la kusaidia kuona nyota, matatizo ni mawe ya kuvukia, matatizo ni mtihani, matatizo ni msalaba, matatizo ni mawimbi katika bahari, matatizo ni mtazamo, matatizo ni ujumbe, matatizo ni mwisho wa sura si mwisho wa kitabu, matatizo ni weusi ulioko nyuma mbele kweupe, matatizo ni sumaku inayokuvuta uwe karibu na Mungu, matatizo ni mapito, matatizo ni matuta katika bara bara kuu ya maisha, matatizo ni ufunuo wa uwepo wa Mungu, matatizo ni somo, matatizo ni masahihisho, ni kinga, ni ishara ya uhai" ni maneno yenye kila aina ya busara, elimu na mafunzo katika kitabu kiitwacho, "Matatizo si Tatizo Matatizo ni Daraja"kimechoandikwa na Fr. Faustin Kamugisha, mkuu wa SAUT Songea.
Wakati wewe unaendelea kulialia na matatizo lukuki uliyonayo, wenzako wanafanya matatizo hayo kuwa fursa na kuvunja rekodi maishani. Watu walimshangaa mtu mmoja akitokea gerezani na lundo la karatasi maarufu kama "Toilet Papers". Zilikuwa nyingi kiasi kwamba alipozipanga kwenda juu zilimzidi urefu. Karatasi ambazo zilitengeneza kitabu kiitwacho, "Shetani Msalabani" . Huyo si mwingine. Ni ni Ngugi wa Thiongo'o. Aliandika kitabu hicho akiwa gerezani. Ndiyo maana Fr. Kamugisha anakwambia matatizo ni fursa. Wakati wengine wakiwa gerezani wanawaza mbinu mpya za kuiba, wenye akili wanawaza namna ya kufaidika kutokana na kifungo.
Kama nchi tunapitia matatizo lukuki ambayo tukiyabadilisha na kuwa fursa, walahi Ulaya haita ona ndani kimaendeleo. Tunahitaji kuwa na mtazamo hasi kwa matatizo hasa ya kimfumo yanayowanyong'onyesha watanzania. Mtu mwenye mtazamo hasi ni mtu ambaye anafanya fursa zake ziwe matatizo na mtu mwenye mtazamo chanya ni mtu anayefanya matatizo yake yawe fursa amesema Fr. Kamugisha kupitia kitabu chake, uk. 13.
Unapovurunda katika kazi ulizoaminiwa, kubali kuwajibika na kuachana na kasumba ya kulalamika kwamba wamekuonea. Wakuonee ili iweje? La msingi hapa, rudi nyuma, tafakari kwa sauti kuu na ujue ulikosea wapi. Hivi karibuni Rais amefanya mabadiliko katika nafasi za ukuu wa wilaya, kunawalioondolewa kabisa. Sasa badala ya kujiuliza kwa nini wameondolewa, kunamabifu yameanza kujitokeza kwamba wamepigwa majungu. Kuondolewa katika uongozi ni ishara ni tatizo ambalo walengwa wote wanatakiwa walipokee katika mtazamo chanya na kutafakari kwa kina, kwa nini imekuwa hivyo.
Maisha ni changamoto. Changamoto ndizo zinazofanya maisha yavutie, kuzishinda ndiko kunakufanya maisha yawe na maana ameandika Fr. Kamugisha uk 15. Kupata changamoto ni sawa na kukalia msumari, huwezi kutulia lazima usimame ufanye kitu Fulani. Watanzania tumekalia misumari kwa muda mrefu, hebu sasa tuamke na tufanye kitu. Tusiwe kama vijana wanaokubali kutumika huku wakiendelea kukalia misumari. Kumbuka unapoona tatizo basi ujue suluhisho haliko mbali.
Matatizo ni giza la kukusaidia kuona nyota. Matumaini yetu yawe kama nywele na kucha.Haijalishi unazikata mara ngapi, haziachi kuota, ameandika Fr. Kamugisha uk 19 wa kitabu, "Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja". Vizuizi viko vingi lakini ni mwiko kukata tamaa. Askari watapiga mabomu sana, lakini chukua maji, nawa uso, endelea kudai haki yao. "Unaweza kulala chini na kufa, au unaweza kusimama na kupigana, lakini hakuna kurudi nyuma". Ili punje ya ngano iweze kuota, haina budi kuzikwa mpaka ioze alisema Ngugi wa Thiong'o kupitia riwaya yake ya "Grain of Wheat". Bila matatizo akili haiwezi kukomaa. Utabaki kubwa jinga. Huwa ni kiyakumbuka maneno ya Mch. Mpemba wa kanisa la kwa Neema Mwanza, nacheka sana, eti, ‘Kichwa kikubwa, macho makubwa, akili finyu".
Matatizo ni weusi ulioko nyuma, mbele ni kweupe, usikubali kurudi gizani (nyuma). Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Jifunze kusamehe na kusonga mbele. Kumbuka huwezi kuleta mabadiliko kwa takwimu za nyuma, alisema Mch. Msigwa, Mbunge machachari kutoka Iringa. Usiwe mpumbavu kama mwanamume mmoja kuongea hadharani kwamba mke wake akikonda sana kupitiliza anamrudisha nyumbani. Ili iweje?
Matatizo ni mawe ya kuvukia. Ukifanya kosa, litumie kama jiwe la kuvukia kwenda kwenye wazo jipya ambalo usingeligundua kama kungekuwepo na kosa ameandika Fr. Kamugisha uk 21 wa kitabu, "Matatizo si Tatizo, Matatizo ni Daraja".
Matatizo ni matuta katika barabara kuu ya maisha. "Njia ya kwenda kwenye mafanikio haikunyooka. Kunakona inayoitwa kushindwa, sura ya kitanzi inayoitwa kuchanganyikiwa, matuta ya kupunguza spidi yanayoitwa marafiki, taa nyekundu zinazoitwa adui, taa za kutoa onyo zinazoitwa familia, taili zenye pancha zinazoitwa zinazoitwa pancha, lakini ukiwa na tairi la akiba linaloitwa kupania kitu, na injini inayoitwa uvumilivu, dereva anayeitwa nguvu ya nia, utaweza kufika mahali panapotwa mafanikio" ni maneno kuntu kutoka kwa Fr. Kamugisha. Kwakweli padri kaandika.
Jamaa mmoja nyumba yake iliungua na kuteketea, badala ya kujiua, yeye akasema, "haya ni matuta ya kupunguza spidi kwenye barabara kuu ya maisha". Matatizo yanatupa nafasi ya kufikiri. Matatizo yanaimarisha ubongo. Matatizo ni mapumziko ya shughuli tunazozifanya. Matatizo ni kituo siyo alama ya nukta. Matatizo ni vituo vya kutufanya tutafakari na kuwa makini zaidi. Matokeo mabaya uliyoyapata kidato cha nne yasikufanye ujiue. Ni muda wa kujipanga upya. Kama dhamira yako ni kusoma, nenda karudie. Fr. Kamugisha anatupa mfano huu, uk. 49, " Mfanyabiashara mmoja aliweka maneno yafuatayo kwenye fremu ya duka lake na kila aliyekuja kwake na maneno ya kukata tamaa alimuonesha maneno hayo kwenye fremu na yalisomeka hivi, "Alishindwa katika biashara mwaka 1831. Alishindwa tena katika biashara mwaka 1833.. Alichaguliwa kuwa mmoja wa watunga sheria mwaka 1834. Mpendwa wake wa moyo, yaani mke wake aliaga dunia mwaka 1835. Alichanganyikikwa mwaka 1836. Alishindwa nafasi ya spika 1838. Alishindwa kuingia kwenye Congress mwaka 1848. Alishindwa kuchaguliwa kuwa Elector mwaka 1840. Alishindwa kuingia kwenye Congress mwaka 1843. Alishindwa kuingia kwenye Congress Mwaka 1848. Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1860. Jina chini ya rekodi hii ni Abraham Lincoln".
Picha tunayoipata hapa ni kwamba kila alipokuwa anakumbana na tatizo hakukata tama, aliendelea kuthubutu na mwisho wa siku akaibuka kuwa mshindi. Kumbe unapopata tatizo suluhisho siyo kujiua, bali kukaa chini na kupata muafaka.
Maneno yangu yangu yangekuwa ni sheria, basi kila mtanzania LAZIMA angesoma kitabu hiki na hakika kama nchi tungeona mabadiliko makuu katika kila sekta. Lakini basi kwa ridhaa yako nakushauri fanya juu chini ujisomee k

Tumia akili acha ulevi

February 07, 2020
Kila ukinywa bia 1 umekunywa tofali 2 za kujengea. Bia 1 kwa bei ya kawaida ni Tsh.2500/= na tofali 1 la inch 6 kwa maeneo mengi ya nchi ni bei isiyozidi Tsh.1300/=. Kama unakunywa wastani wa bia 5 kwa siku (kipimo cha kawaida) it means unakunywa bia 1,825 kwa mwaka sawa na tofali 3,650. Tofali 3,650 zinatosha kujenga nyumba 1 ya room 3 self contained ya kisasa. Kama unakuwa na kidosho, atakuwa amekunywa gharama za ufundi. wapambe wamekunywa za bati na misumari. hii inamaanisha kuwa kama wewe ni mnywaji basi kila mwaka unakunywa angalau nyumba 1 au 2. Sasa hebu jiulize tangu umeanza bia hadi leo umeshakunywa nyumba ngapi?

 Anyway.. tuache kufananisha nyumba na vitu vya maana kama bia.
Wewe kunywa tuyuuuuh
✝️🔯
EV.MCHOME
 
Copyright © Yote Yanawezekana Kwa Yesu. Designed by OddThemes